Ni kwanini amri ya kuiabudu siku ya sabato tangu enzi za Musa hadi sasa ni jumamosi lakini makanisa mengine huabudu jumapili?

Ni kwanini amri ya kuiabudu siku ya sabato tangu enzi za Musa hadi sasa ni jumamosi lakini makanisa mengine huabudu jumapili?

Kifo cha Yesu ndio ilikuwa mwisho wa sheria, na hata zile kanuni za siku ya sabato hakuna hata msabato mmoja anayezifuata
Kufa kwa Yesu kulikuwa mwisho wa Amri 10 ?

ni ruhusa kuua ?
Ni ruhusa kuiba ?
Ni ruhusa kuabudu miungu mingine?
Ni ruhusa kuzini ?
 
Moja ya amri kumi ni kuabudu siku ya sabato, Siku takatifu iliyotengwa kila wiki kwa ajili ya KUPUMZIKA NA KUABUDU, Sabato haiwezi kuwa kila siku kwasababu sabato ni siku ya mapumziko, huwezi kupumzika kila siku kwa kisingizio cha sabato.

Ni tangu enzi za Nabii Musa alieshuka na amri 10 aliabudu sabato siku ya Jumamosi, Hata Yesu aliikuta siku hio na kuiabudu na hadi sasa ukienda Israel siku ya jumamosi maduka hufungwa.

Inashangaza kuona baadhi ya wakristo wanaabudu jumapili wakati sio siku ya sabato
Kumbuka kuna kitu kinaitwa Agano... and kila siku ni siku ya Mungu.. hizo ni community tu watu wanasali kila siku.. Kasome Injili hautapata shida na Sabato kwani Sabato ni for Men not Men for Sabato.

Jesus alipomwaga damu ndio aliweka Agano Jipya kufuata mafundisho yake ili msipotee... Ng;ombe wako akitumbukia shimoni siku ya sabato mtoe, Hamas wakikuvamia kukuangamiza ingia vitani pigana uwashinde na sio kushindwa.. ndio maana Netanyau kakomaa nao
 
Shida ni kua wengi tunasali/tunafata Imani kimapokea ,Lakini ukweli wa siku sahihi ya Ibada mapadri maparoko na papa wanajua ni jumamosi na wanakiri kua ilibadilishwa .

Kwa sasa Cha muhimu ni kusali kwa roho na kweli siku Haina pakutupeleka mkuu.
Ukiijua histori ya dakika,saa,siku,wiki,mwezi hadi mwaka , utaachana na hizo hadithi za sabato ya jumamosi sijui jumapili na siku gani sijui.
 
Kama mpaka leo kichwani kwako unawaza siku fulani ndo sahihi kuabudu basi pole sana.
 
Kumbuka kuna kitu kinaitwa Agano... and kila siku ni siku ya Mungu.. hizo ni community tu watu wanasali kila siku.. Kasome Injili hautapata shida na Sabato kwani Sabato ni for Men not Men for Sabato
Kila siku ni siku ya Mungu lakini sio kila siku ni sabato kwasababu Huwezi kupumzika kila siku
 
Siku ya sabato sio Mila wala Tamaduni, NI AMRI !!
70 ya yaliyoandikwa kwenye again la kale ni mila za zamani za kiyahudi. Kama manabii na mitume wasingeibukia maneno hayo usingeyaona kwenye maandiko, vitu kama divai, MKATE, kutokula nguruwe, sabato , ubani , kanzu yote hayo ni tamaduni manabii walizokuta jamii zao Wana practice na wao wakaishi nazo. Ni Yesu pekee aliyetenganisha kati ya neno la Mungu na Mila za kiyahudi hadi wakakasirika na kumuua
 
Kila siku ni siku ya Mungu lakini sio kila siku ni sabato kwasababu Huwezi kupumzika kila siku
Unajua hesabu za siku zinavyo hesabiwa? Ukisheherekea Siku yako ya kuzaliwa monday 1st January basi next year utasheherekea 31st December so actuary utakuwa unasheherekea the wrong day according to rotation ya dunia kuzunguka Jua.. Kifupi Sabato ni ya Mungu wa Musa aliwaagiza waisrael waikumbuke na kuitakasa.. kwa hesabu zetu za kuzunguka Jua kuhesabu siku na mwaka tupo nje kabisa tokea siku ya kwanza.. kuna wakati tuna siku 365 na robo na kuna time mwaka mfupi na kama tokea dunia iumbwe siku zilihesabika 1 to 7 hadi leo hii sabato ingekuwa inangukia siku yeyote either Monday tuesday n.k
 
Moja ya amri kumi ni kuabudu siku ya sabato, Siku takatifu iliyotengwa kila wiki kwa ajili ya KUPUMZIKA NA KUABUDU, ni siku aliyoiweka Mungu kuturuhusu tupumzike nasi tunamshukuru kwa kujumuika kwenye nyumba za ibada kumuabudu kisha tunarudi kwetu kupumzika,

Ni tangu enzi za Nabii Musa alieshuka na amri 10 aliabudu sabato siku ya Jumamosi, Hata Yesu aliikuta siku hio na kuiabudu na hadi sasa ukienda Israel siku ya jumamosi maduka hufungwa.

Inashangaza kuona baadhi ya wakristo wanaabudu jumapili wakati sio siku ya sabato

MUHIMU: Kila siku ni siku ya Mungu lakini sio kila siku ni sabato kwasababu siku nyingine ni za kazi.
Uneacha dhambi zote za uzinzi, uasherati, uongo. Umeona hii tu ya Sabato ndiyo ya kukomaa nayo? Kitu gani so special sana kuhusu sabato?

Je nikishika hiyo sabato nikawa mzinzi ina maana yoyote?
 
70 ya yaliyoandikwa kwenye again la kale ni mila za zamani za kiyahudi. Kama manabii na mitume wasingeibukia maneno hayo usingeyaona kwenye maandiko, vitu kama divai, MKATE, kutokula nguruwe, sabato , ubani , kanzu yote hayo ni tamaduni manabii walizokuta jamii zao Wana practice na wao wakaishi nazo. Ni Yesu pekee aliyetenganisha kati ya neno la Mungu na Mila za kiyahudi hadi wakakasirika na kumuua
Huo ni mjadala mwengine kabisa fungulia uzi wake, hapa kinachozungumziwa ni sabato, Siku aliyoitoa Mungu kuturuhusu kupumzika nasi kwa kumshukuru tunajumuika nyumba za ibada kumshukuru kisha kurudi majumbani kupumzika.

Siku, Siku, Siku !!!!
 
Uneacha dhambi zote za uzinzi, uasherati, uongo. Umeona hii tu ya Sabato ndiyo ya kukomaa nayo? Kitu gani so special sana kuhusu sabato?

Je nikishika hiyo sabato nikawa mzinzi ina maana yoyote?
Ni uamuzi wako wala huzuiwi kuzini ama kutenda dhambi yoyote, umepewa uhuru wa kuyafanya lakini pia umepewa utimamu wa kujua unachofanya sio sahihi ni dhambi.
 
Iwe jumamosi ,iwe jumapili, wewe inakusaidia nini? Alafu mna uhakika gani kuwa siku ya 7 ni jumamosi, hamjui kuwa kalenda ilikwisha badirishwa mara nyingi na huwezi kujua ni lini hao wayahudi waliabudu siku ya 7, hakuna mwenye ushahidi kuwa siku ya 7 ni jmos,

Alafu huyo Mungu alisema siku ya 7 upumzike maana yake siku yoyote ndani ya siku7 unaweza kuitumia kama mapumziko, lkn kuna vilaza hawa waliounda dini wanafosi mambo ya kutumia akili zitumike nguvu kuwa jambo fulani lazima liwe wanavyotaka wao.

Mnawapinga wakatolic wakati wao ndio waliowapeni biblia, mifumo yote ya kidini mnatumia yao wenyewe ambayo hamna nguvu za kuibadiri.

Ni ngumu kuwahukumu waliowapa hivyo vitabu maana ni wao wanajua lipi sahihi na lipi sahihi kwakuwa ni wao pia waliozitafsiri na ni wao chanzo cha hayo magenge mengine mnayoita madhehebu.

La mwisho, ijapokuwa dini ni uzushi na utapeli, lkn huyo Mungu wenu hana time na hayo makanisa yenu ya wakati huu maana kibiblia kanisa ni wewe Mtu/mwanadamu na sio hayo magenge yenu ya Jpili&jmos, hakuna ktk biblia kumeandikwa wala kuhalalisha ibada za makanisa, acheni utapeli enyi watumwa wa wazungu.
 
Iwe jumamosi ,iwe jumapili, wewe inakusaidia nini? Alafu mna uhakika gani kuwa siku ya 7 ni jumamosi, hamjui kuwa kalenda ilikwisha badirishwa mara nyingi na huwezi kujua ni lini hao wayahudi waliabudu siku ya 7, hakuna mwenye ushahidi kuwa siku ya 7 ni jmos,
Ni tangu enzi za Musa, Yesu mpaka sasa ukienda Israel siku ya Sabato ni ile ile miaka nenda rudi, JUMAMOSI
 
Mwenye amri zake 10 aliempa Musa azilete tuziabudu (akiwemo na Yesu aliezitii)
Najua ila why jumamosi??
Sidhani kama wayahudi walikua wanaziita jumatatu/jumanne mpaka jumapili walikua na lugha yao!
Sasa nataka kujua aliekuja kuvumbua kwamba sabato ni jumamosi isiwe ijumaa au juma3 ni nani? Maana sabato maana yake siku ya saba ya awali ambayo Mungu alipumzika baada ya kukamilisha uumbaji . Hakuna mahala ilitajwa ni jumamosi ama lazima iwe jumamosi!
 
Back
Top Bottom