Ni kwanini bado Waarabu wanatubagua, hata Mwafrika anapokuwa Muislam wanamkatalia kumuoa binti yao?

Ni kwanini bado Waarabu wanatubagua, hata Mwafrika anapokuwa Muislam wanamkatalia kumuoa binti yao?

@FaizaFoxy bahati mbaya hukuzaliwa mwarabu, ungekuwa mbaguzi hatari. Umekuwa ukiuishi kwa kuunakili tu.

Ungejua hata hili neno 'ustaarabu' asili yake ni ubaguzi usingejinadi nalo huku. Hivi hujui mababu zako ndiyo waliokuwa wakitukanwa na waarabu kuwa hawajastaarabika 'being not culturally arabized'.

Pengine ungejifunza kutofautisha kati ya kuwa 'being arabized' na 'being civilized'
Cha kushangaza huwa anajidai nayeye ni Muarabu kumbe ni Mbantu wa Mkuranga hapo
 
Umemaanisha nini kusema mkristo wa kweli ni muislam?
Namaanisha nilichokisema, Waislam ndiyo wanafata mafundisho ya Yesu Kristo to the dot.

Wanaojiita wakristo hawafati mafundisho ya Yesu wanafata mafundisho ya paulo na kanisa.

Kumbuka kuwa Uislam haubagui mitume wa Mwenyezi Mungu na Uislam unatufundisha kuwa mitume wote walikuja na ujumbe mmoja kila mmoja wao kwa wakati wake na Yesu Kristo ni mtume kwa Waislam.
 
Anha nimekuelewa,Sasa kwanini mafundisho ya ukristo yanapingana na uislam? Mfano swala la ndoa ya wake wengi hairuhusiwi na Yesu Kristo mwenyewe alilisema,swala la vyakula Yesu aliruhusu kula chochote lakini naskia waislam hamruhisiwi baadhi ya vyakula, kiufupi Kuna mambo mengi sana yanayotofautiana kati ya uislam na ukristo
 
Wayahudi ndio wanaoongoza Kuoana wenyewe Kwa wenyewe,achilia mbali mtu mweusi hata hao wazungu wenzao hawapewi kuoa mabinti wa kiyahudi.
 
Hivi unajua hata umeme uligunduliwa lini hadi useme waliepeleka na taa za barabarani?
Huku tunapenda kuelezana kwa hoja na siyo hadithi. Nipe ushahidi wa ulichokisema.
Waisilamu walivyoenda Spain walisambaza civilization kwa kiasi kikubwa
1. Utaratibu wa kuoga
2. Utaratibu wa kupiga mswaki
3. Utaratibu wa kuwa na maji taka
4. Walipekeka karatasi
5. Walipeleka taa za barabarani
6. Walipeleka maktaba
7. Walipeleka universities etc

Haimaanishi watu hawakuwa wakioga kabisa ama mtu wa kwanza kupiga mswaki alikua Muisilamu Bali uisilamu ndio umeleta ile tabia ya kuoga Kila siku ama kuoga mara 2 ama mara 3 kwa siku.

Wakati huo waarabu wanaenda Spain wafalme wa Ulaya walikua wakijisifa kutokuoga, kina Elizabeth wa kwanza anajisifia kabisa yeye kaoga mara 2 tu maisha yake alivyozaliwa na alivyoolewa.

Kanisa Kuna wakati lilipiga kabisa marufuku kuoga uchi, na Hata Waisilamu walivyopigwa Spain na kufukuzwa Queen Isabela wa Spain Bado alijisifia kutokuoga (ili kuonesha Waisilamu walikua wrong kwa kuoga oga Kila mara) wengine waliamini kuoga kunaleta magonjwa. Wakati huu ndio Ulaya ilisumbuliwa sana na Tauni.

Kuna mpaka Tafiti za kisayansi zinaonesha Crusaders (toka Ulaya) walikua wachafu kupita maelezo na walikua na magonjwa mengi yanayotokana na uchafu.

Kuna vitabu kibao vinaelezea hii issue kama lengo lako ni kutaka kujua nitakuekea.
 
Unafuatilia nini ?!!!

Hivi ukijiamini unabaguliwaje ?!!

Unaanzaje kubaguliwa??!!!

Iwe na mwarabu ,mhindi ,mzungu ama mchina?!!!

Waafrika tu wako wabaguzi dhidi ya wenzao....kikabila ,rangi ,kipato....ssmbuse watu wenye rangi nyeupe?!!!

Dunia ya sasa ya SOKO HURIA na MAARIFA mapana...vilio vya kubaguliwa havina maana....

Unakuwa wapi mpaka mtu anakubagua?!!

Mfukoni mwake ?!!! [emoji15][emoji1787][emoji1787]

Kwanini uwe mfukoni mwake ?!!

Why desperation?!!!

Umesema kuwa mwafrika hata awe muislam na kuwa (Qari) fundi wa kusoma Quran hawezi kuoa hao waarabu...right?!!!

Nisikilize....watu wengi hawana imani ya dini vile wanavyojionyesha ukubwa wa kuwa nayo....iwe hao waarabu ama wengineo....[emoji1787]

Sasa unataka mwarabu asiye na IMANI kubwa ya dini akupe binti yake kwa kuwa tu wewe "una sauti " kinanda ya kusoma Quran ?!!!

Hao waarabu wengi ni wafanyabiashara....akili zao ziko katika biashara na KUPATA FEDHA eti wakuhusudu wewe MRANGI ,MDIGO ,MUHA uliyehifadhi msahafu kwa kichwa na huna kitu wakupe BINTI YAO kwa kigezo hicho tu [emoji15][emoji15][emoji15][emoji15] labda zamani....sikatai..ziko familia chache ila wengi wakitaka KUZISIKIA HIZO SAUTI NZURI zikisoma QURAN(tajweed ,tartil na hukumu zake) wanawaita walimu wa madrassa wakitoa elfu 50...walimu hao wanakuja na vitoto vya madrassah na kuanza kusoma Quran tukufu ,ikifuatiwa na WASSILATU SHAFI ,Kitabu cha Maulid Barzanji ,wanapiga madufu na nari zake wakimaliza wanajipiga BIRIANI chuzi zitooo...nyumba ya mwarabu tena ,kitonga mseleleko....shughuli ikiisha wanawaaga mpaka siku nyingine...ustadh anakwenda kutamba kijiwe cha kahawa na Al Kasus....[emoji1787][emoji1787]
Ya nini mwarabu "afuge mkwe" wa kirangi ,kiha ,kisambaa ,kinyaturu ,kimeru kisa tu NI FUNDI WA KUSOMA QURAN?!!![emoji1787][emoji1787]

Dunia imebadilika....fedha fedha fedha si hao waarabu si wewe Mngoni.....[emoji1787]

#SiempreJMT[emoji7]
#MamaAnaupigaMwingi[emoji7]

#DP World ndio habari ya mjini [emoji7][emoji7]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Hili povu lote linatoka kwenye tecno F1 😂😂😂...

Ama kweli mama anaupiga mwingi
 
Sasa hata kama wakarashi 'quraysh' huwajui mimi nitakufundisha nini. Nikikutajia waberiberi 'berbers' utasema mimi nawagawa waarabu
Mimi mwenyewe mwarabu wa Oman haya nifundishe makabila yangu yapoje na nisichokijua.
 
Hivi unajua hata umeme uligunduliwa lini hadi useme waliepeleka na taa za barabarani?
Huku tunapenda kuelezana kwa hoja na siyo hadithi. Nipe ushahidi wa ulichokisema.
Nani kakudanganya taa za barabarani zilianza na Umeme? Watu wanatumia mafuta na gesi karne na karne, unaijua karabai?

images (5).jpeg

Hio ni taa ya barabarani ambayo ipo preserved toka miaka hio ya Ottoman.

Kitu Gani hapo juu hukiamini weka nikuwekee Ushahidi wake kuwepo.
 
Kwa wazungu ndoa za waafrika na wazungu zipo nyingi tu, ni kawaida.

Shida inakuja kwa waarabu, yani hata uwe muislam uliekariri aya nyingi za korani na sauti nzuri ya kuzinukuu hawawezi kukupa binti yao labda kama utaweza kutumika kimaslahi aidha uwe na cheo kikubwa serikalini ama uwe na pesa nyingi sana.

Na hapa navomaanisha waafrika ni hadi wazanzibari ambao hufanana na wasomali, hali ni hivyo hivyo tu, japo wao hupenda kujiweka kundi moja na waarabu ila waarabu huwaona ni zao la watumwa

Nani atakuozesha mtoto wake kwa tabia hizi za kupenda vya bure??
 
Anha nimekuelewa,Sasa kwanini mafundisho ya ukristo yanapingana na uislam? Mfano swala la ndoa ya wake wengi hairuhusiwi na Yesu Kristo mwenyewe alilisema,swala la vyakula Yesu aliruhusu kula chochote lakini naskia waislam hamruhisiwi baadhi ya vyakula, kiufupi Kuna mambo mengi sana yanayotofautiana kati ya uislam na ukristo
Weka nistari siyo ya kwako, ya Yesu.

Unayo?
 
Anyway, umeeleza kwa papara nyingi sana. Simple fact ni kuwa, you are brainwashed.

Nani aliyekuambia aliyeleta utaratibu wa kutawaza na maji ni waarabu? Hivi kati ya uislam na uyahudi ni ipi dini kongwe? Au kati ya ubudha na uislam ni ipi dini kongwe? Ni kipi kilichovumbuliwa na uislam? Unajua kuwa wajapan siyo waislam lakini wanatawazia maji toka hata kabla ya kuwepo imani yako duniani? Unajua kuwa hata hivi vyoo tunavyotumia hakuna hata kimoja kinachoitwa Arabian toilets? Ni aidha Indian or European, why? Unajua kuwa kama siyo teknolojia za wazungu kuwasaidia kuchuja maji ya bahari waarabu mpaka leo wangekuwa wanaenda kutawazia visimani au baharini?

Unajua kwa nini nilikuambia utofautishe kati ya 'being arabized' na 'being civilized'? Hili nalo umeshindwa?
Wewe chukulia unavyopenda, Chukulia kuwa Islam ni dini mpya kabisa kamanutakavyo. Hilo lisikupe shida.

Kwa hiyo unanambia nirudi kwenye dunia ya analog niwachane na dunia ya digital?

Uislam ni mwema sana.
 
Weka nistari siyo ya kwako, ya Tesu.

Unayo?
Marko7:17-23 "Alipouacha umati Yesu akaingia ndani ya nyumba,na wanafunzi wakaanza kumuuliza kuhusu mfano huo,Basi akawaambia je ninyi hamwelewi kama wao? Je hamjuwi mtu hawezi kuchafuliwa na kitu kinachoingia ndani yake? kwakuwa hakiingi moyoni mwake bali tumboni,Kisha hutoka na kuingia chooni? KWAHIYO AKATANGAZA VYAKULA VYOTE KUWA SAFI,Tena akasema kile kinachotoka ndani ya mtu ndicho humchafua,kwamaana kutoka ndani moyoni mwa mtu,hutoka mawazo mabaya,uasherati,wizi,mauwaji,uzinzi,pupa,uwovu,udanganyifu,mwenendo mpotovu,jicho lenye wivu,makufuru,majivuno,na ukosefu wa akili.Mambo yote hayo maovu hutoka ndani nayo humchafua mtu". Kulingana na haya maandiko kwa wakristo ni halali kula chakula chochote lakini kwa waislam naskia nguruwe ni halam,so hapo tu unaona utofauti wa ukristo na uislam,Bado sijagusia kuhusu ndoa ya wake wengi,pombe n.k
 
Wacha kudanganya watu .
Andiko la MARKO sio la YESU mwana wa MARIA.

MARK SIO MMOJA KTK WANAFUNZI WA YESU. Sasa lini alimsikia Yesu akitamka chochote?
Nafahamu hili litakukuchanganya uanze kutoa mapovu ovyo manake siku zote umedanganywa .

Anza na hii kwanza.

Waandishi wa AGANO JIPYA ndio wanadai Yesu kasema hivi na vile.
Sasa ili tupate kuwafahamu hao waandishi tuanze na MAJINA YAO KWANZA.
JE Hawa waandishi wa BIBLIA BABA ZAO NI NANI?

Matthew who?
Mark who?
Luke who?
and John who?
Umeshawahi kuona MUANDISHI YYT DUNIANI ANA JINA MOJA TU?

Bila kujua majina ya WAZAZI WAO vipi tutaweza kukubali wanachosema kuwa ni KWELI? Na hali ya kuwa HAKUNA YYT ktk hao ALIWAHI KUWA MWANAFUNZI WA YESU?

Naomba Jibu. Acha mapovu
 
Ubaguzi ni hulka
Na kila jamii ina ubaguzi
Mwarabu wa saudia anambagua Al burush yaani mwarabu wa Iran
Mwarabu wa dubai au UAE anamuona mwarabu wa Africa sio muarabu ni muafrica
 
Wacha kudanganya watu .
Andiko la MARKO sio la YESU mwana wa MARIA.

MARK SIO MMOJA KTK WANAFUNZI WA YESU. Sasa lini alimsikia Yesu akitamka chochote?
Nafahamu hili litakukuchanganya uanze kutoa mapovu ovyo manake siku zote umedanganywa .

Anza na hii kwanza.

Waandishi wa AGANO JIPYA ndio wanadai Yesu kasema hivi na vile.
Sasa ili tupate kuwafahamu hao waandishi tuanze na MAJINA YAO KWANZA.
JE Hawa waandishi wa BIBLIA BABA ZAO NI NANI?

Matthew who?
Mark who?
Luke who?
and John who?
Umeshawahi kuona MUANDISHI YYT DUNIANI ANA JINA MOJA TU?

Bila kujua majina ya WAZAZI WAO vipi tutaweza kukubali wanachosema kuwa ni KWELI? Na hali ya kuwa HAKUNA YYT ktk hao ALIWAHI KUWA MWANAFUNZI WA YESU?

Naomba Jibu. Acha mapovu
Hufaham lolote kuhusu Biblia inaonyesha,ungekuwa unafaham maana ya injili usingekurupuka kuleta ubishi wako,na ww sio mkristo ndiomaana hufaham hao waandishi wa injili ni wakina nani,wakristo wote Dunian wanatumia Biblia kama reference,Sasa kama unabishana na maandiko basi ni wazi huujuwi ukristo,na aliyeuliza alitaka nimpe vifungu vya Bible kama reference,fikiri kabla ya kutenda
 
Back
Top Bottom