Na cha Kushangaza zaidi karibia 85% ya Bidhaa zao hizo za Electronics ni Original kabisa lakini bado wanaziuza / zinauzwa kwa Gharama nafuu sana wakati huko Tanzania ( Nyumbani ) bidhaa nyingi ambazo tunauziwa kwa Gharama Kubwa hapa Uganda bado ni Feki pia.
Haya Mangwena ( Wabobezi ) wa Uchumi tu hebu tafadhalini njooni hapa mtupe sababu kwani inashangaza sana.
Jamaa yangu katoka huko mwezi jana, alikua anatafuta vifaa vya umeme vya tronic kuitaja tu wakaanza kucheka, ikabidi wampe vifaa og vya kampuni nyingine kabisa wakamshauri tronic ya afrika ni fake kupita maelezo

Kuna uwezekano mkubwa ama Wafanyabishara wa Tanzania wanatuibia sana Sisi Wateja wao au basi Watu wa TRA kwa Makusudi wanapandisha Tozo za Bidhaa kwa Wafanyabiashara wa Tanzania kwa maagizo ya CCM Serikali ili kuwaminya zaidi Kimapato na kuwafanya Watanzania wayaone Maisha ni magumu.
Haiingii Akilini kabisa Uganda ambayo ni Landlocked Country huku kwa 50% wakitegemea Bandari ya Mombasa na 50% yetu ya Dar es Salaam ukienda kununua Bidhaa zao za Electronics ( hasa Kampala ) ni vya Bei nafuu, halafu ni Imara na Original kabisa. Nadhani kuna tatizo mahala Mtani wangu au?