Ni kwanini Commando huwa ni jasusi mzuri kuliko yule mtu wa kawaida tu aliyepitia mafunzo ya Usalama wa Taifa?

Ni kwanini Commando huwa ni jasusi mzuri kuliko yule mtu wa kawaida tu aliyepitia mafunzo ya Usalama wa Taifa?

Sijawahi kuwa karibu na hao watu. Hivyo siwezi kujua ubora wao katika hizo shughuli zao. Miziziology inahusika kwa hao wenye uwezo wa kupotea katikati ya upepo.

Nami zamani nilikuwa naamini hivi hivi kama Wewe ila baada ya Kukutana na Mmoja Wao na Kunielimisha vyema hiyo Dhana imeshanitoka rasmi.
 
Majibu ya namna hii yanafanya watu wapuuzie uzi wako mkuu, tupingane kwa hoja..mbona jamaa anareply kwa hekima

Kwani Uzi wangu ukipuuzwa kuna chochote kile Kinapungua katika Mwili wangu / katika Akaunti yangu ya Kimuamala? Hebu nitolee Upuuzi huu.
 
Nami zamani nilikuwa naamini hivi hivi kama Wewe ila baada ya Kukutana na Mmoja Wao na Kunielimisha vyema hiyo Dhana imeshanitoka rasmi.

Itabidi na mimi nitafute mtu wa kunielimisha mkuu.
 
Nimesikia mahala kuwa COMMANDO (si lazima awe wa Tanzania) ana uwezo wa kupata taarifa nyeti hata kuliko Mwana Usalama Taifa mwenyewe. Kwa mfano; COMMANDO wa Malawi anaweza akaenda nchini Zimbabwe katika maeneo yao muhimu na akapata akitakacho na wala asishtukiwe, lakini kwa Usalama wa Taifa wa Malawi anaweza kwenda ila atagundulika kwa haraka sana tu.

Wajuvi wa haya Masuala mliojazana hapa Jamvini JamiiForums, karibuni mtuelimishe na sisi akina Mzukulu ili nasi tuwe na Maarifa kama nyie pia.

kwa kweli hata sijui itakusaidia vipi kimaisha ukitakajua haya mambo, lakini sio mbaya kama burudani, kwanza hizi nchi za kiafrica hao hawana umuhumimu wowote, awe watanzania au malawi.
Ni wa muhimu kwenye nchi zenye maslahi fulani kwenye nchi fulani mfano nchi za mabeberu, ofisi za balozi zao zote zina hawa watu.
Lakini kwa burudani yako angalia hizi series zinaitwa THE UNIT

Sasa kama umeshajua kuwa nilichokiuliza hakitanisaidia chochote imekuwaje Wewe tena umenijibu na kwa Ufafanuzi zaidi? Nikueleweje labda?
 
Mkuu hii comment imenifanya nicheke sana. Maana kuna dogo hapa anapenda kuvaa jezi za Yanga anasemaga yeye ni usalama wa taifa! Kwa hiyo atakuwa ni commando!?
Kumbe anasema sasa wewe unaamini?
 
Sema chief una dharau sana [emoji23][emoji23][emoji23]

Nina Historia yoyote labda ya Mimi Mzukulu a.k.a Brainy Chap ya Kukudharau Wewe Ndugu? Kama ipo ninakuomba uiweke hapa hadharani upesi.
 
Wewe kuna maafisa usalama hawajui hata kurusha ngumi

Nilikuwa natafuta na ninangojea post / comment ya Mtu ambayo itanifanya nicheke sana ili nilale zangu kwa Furaha nadhani sasa nimeshaipata.
 
Komandoo/kikosi maalum(special tactical military force) ni kikundi maalum cha jeshi kinachojishughulisha na operesheni maalum za siri zisizohitaji kikosi kizima cha jeshi. Hawa jamaa wanafanya operation kwa kutumia info za secret agent (usalama).

Usalama wa taifa /vizuri hapa aitwe intelligence officer Yeye anatoka TISS Lkn kama field agent. Hafahamiki na yeyote isipokuwa na handler wake na maofisa wachache sana wa juu. Si kazi yake kufanya operation ila ye ni mchora ramani wa namna gani makomandoo wanapaswa kufanya. Hufanya yote haya pasipo hata kuonana na makomandoo hao.

Hivyo hakuna uhalisia wa nani ni rahis kukamatwa kuliko mwingine. Kwanza ukikamatwa Nchi yako inakukana pia. Sheria ni hakuna kukamatwa na ukikamatwa hakuna kutoa siri.

Hili ni eneo Pana sana na hapa bongo ni jambo la Siri, haya na wengine watakayoyaleta yatatupanua zaidi.
 
Back
Top Bottom