Mkuu wangu hizi taaluma zina uzito eake kulingana na majukumu husika kwa wkt huo. Komando hii ni nafasi ambayo kwanza lazima uwe ni askari jeshi kwa hapa Tz ni TPDF, wanajeshi hupitia mafunzo mbali mbali ya kikakamavu mpka kupewa kazi au kupangiwa kituo cha kazi na mpka anakua komando kunahatua anapitia kufika pale. Usalama wataifa ni chombo au taasisi ya kiusalama inayojumuisha kada zote za utumishi wa umma nia ni kupata taarifa na kujua nna gsni ya kuzikabili isitokee au kuleta janga kwa taifa, hawa hupatikana kulingana na historia zao, familia zao, makuzi yao na hata utendaji wao wa kazi hapo baadae. Pia hii taasisi haichagui kazi husika ya mtu wao mfano ina wanajeshi, polisi, walimu, wafanyabiashara, wakulima na hata watu ambao kijamii huona hawajitambui na hawa hupewa mafunzo namna gani ya kufanya majukumu yao ya kila siku. Sasa utofauti wao unakuja ktk namna ya ufanyaji wa kazi husika, Komando atafuata alichoambiwa ktk kazi ila pia atakua na ujuzi binafsi ukumbuke huyu ni askari jeshi alie komaa kimafunzo hivyo kukamatwa kwake pia kunataka umakini sana. Jasusi au mwana usalama pia ni m'bibezi ktk fani yake ya kupata taarifa ingawa hawa ni ngumu kuwafamahu kwan hawatokei tu bali ni pandikizi kwa muda fulani na wana kua na uthibitisho sahihi mahali wanapofanyia kazi, mfano hawezi kupangiwa ubalozini bila kua ma kigezo cha kua pale kama afisa ibalozi husika. Suala la nani anaweza kukamatwa kwa urahisi hiz zinakua ni makosa ya kibinaadamu ktk kazi ndo hupelekea kugundulika kwa wahusika na hata ukamataji wake sio sawa na kutuma defender ya polisi. Nani yuko makini zaidi ya?????? Hiko swali bado linabaki kwa watendaji husika.