Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Siku chache zilizopita DC wa Hai, Ole Sabaya alijitokeza mbele ya vyombo vya habari akiwatuhumu wamiliki wa mabasi ya Limu Safaris na Machame Safaris kuwa wameunda magenge ya kiuhalifu ya uhalifu ya kuhujumu reli kati ya Moshi na Arusha na hivyo akawataka wamiliki wa mabasi hayo wajisalimishe kituo cha polisi cha Boma ng'ombe ili wajibu tuhuma zao
Wamiliki hao wa mabasi walitii amri hiyo ya DC Sabaya ya kuripoti kituo cha Boma ng'ombe kwa wakati alioagiza DC huyo Sabaya
Baada ya wamiliki hao wa mabasi kuripoti Polisi, RPC wa Kilimanjaro, Salum Hamdun, alijitokeza hadharani kueleza namna wamiliki hao waliivyoweza kutii amri bila shuruti na akaeleza pia namna Polisi hao waliivyofungua jalada la uchunguzi na namna uchunguzi wao ulivyoenda
RPC huyo akaeleza waziwazi kuwa baada ya uchunguzi wao, wamebaini kuwa hakuna hujuma yoyote iliyofanyika katika kipande hicho cha reli kati ya Moshi na Arusha kama aliivyodai DC Ole Sabaya
Ndipo hapo ninapojiuliza ni kwanini Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli, hamfukuzi kazi DC Sabaya kwa kusababisha usumbufu mkubwa kwa wamiliki hao wa mabasi ambao imekuja kuonekana kuwa tuhuma ambazo walipewa na Mkuu huyo wa wilaya kuthibitidhwa kuwa ni za uwongo?
Vile vile hii si Mara ya kwanza kwa Mkuu huyo wa wilaya ya Hai kukumbwa na kashfa za aina hiyo za kuwasingiziia wafanyibiashara kuwa wanahujumu uchumi kwa kukwepa kulipa kodi na baadaye kuja bainika kuwa ni uwongo aliowazushia
Hivi tutaendelea kufanya kazi na wakuu wa wilaya wa "dizaini" ya huyo Mkuu wa wilaya ya Hai hadi lini?
Tafsiri tunayoipata wananchi ni kuwa kumbe baadhi ya wateule wa Rais wana "impunity" na hawawezi wajibishwa kwa makosa ya wazi kabisa wanayowafanyia wananchi kwa chuki tu kwa kutumia vyombo vyetu vya dola, kama vile Jeshi letu la Polisi kuhalalisha uharamia huo!