Ni kwanini DC Sabaya hajawajibishwa baada ya kubainika kuwa tuhuma alizotoa kwa wamiliki wa mabasi kuhujumu miundo mbinu ya reli ni za uongo?

Ni kwanini DC Sabaya hajawajibishwa baada ya kubainika kuwa tuhuma alizotoa kwa wamiliki wa mabasi kuhujumu miundo mbinu ya reli ni za uongo?

Na sabaya atakuwa na maadui wengi sana maana wale watu ni watu wameajiri vijana wengi sana kutokana na hizo biashara zao

Sent using Jamii Forums mobile app
Yeye anachojiamini ni kuwa yupo karibu na Rais......

Ajaribu kumuuliza mwenzake Lugola, ambaye kila siku alikuwa akimpamba Mkuu, hata hivyo mwisho wa siku akamtumbua hadharani kwa aibu!
 
Anamshughulikia Mbowe Hai huko. Hawezi tumbuliwa.
Amshughukikie akitenda haki........

Lakini kwa njia hii anayoitumia ya "Bashite style" hakika kuna siku ataangukia pua
 
Kama huyu alifoji kitu hii na bado yupo.
View attachment 1333780
Kitendo cha kufoji kitambulisho cha TISS na mpaka sasa bado yuko kazini ni uthibitisho kuwa kitambulisho hicho sio forgery, ila ni kawaida kwa TISS kuwakana watu wao cover zao zikiwa blown, hata yule mpuuzi aliyemtishia Nape bastola, naye walimkana, Mwigulu mchemba akajifanya polisi inamsaka.
P
 
Mkuu Bana likasi ndiyo sababu tunamwambia Magufuli kuwa sheria haiaangalii sura ya mtu, ni kama msumeno unakata huku na kule........

Kwa hiyo anachofanya Rais wetu cha kuwajengea "impunity" baadhi ya wateule wake, kinaleta chuki na visasi ndani ya jamii
hao wapo kwa mlengo wa kisiasa zaidi kuliko utendaji wamewekwa kuhakikisha chadema awapumui hata wao wanajua kwamba ni special
 
sabaya with bashite style mwsiho wake utakuwa mbaya kama jina lake,sijui baba yake alikosa jina la kumpa
 
Sure..
Yule wa nape namfahamu alikuwa mlinzi wa bashite anaitwa herry kisanduku.
Kama ni kweli jamaa ni TISS, hata kumtaja hapa ni kosa la jinai, sheria ya usalama wa taifa inakataza kumtaja in public ofisa yoyote wa TISS, huko ni ku blow his cover!, kutokujua sheria sio excuse ya kutokutenda kosa kwa kuivunja sheria usio ijua!.
P
 
Kama ni kweli jamaa ni TISS, hata kumtaja hapa ni kosa la jinai, sheria ya usalama wa taifa inakataza kumtaja in public ofisa yoyote wa TISS, huko ni ku blow his cover!, kutokujua sheria sio excuse ya kutokutenda kosa kwa kuivunja sheria usio ijua!.
P
Mbona president huwa anawa expose hadharani? Umesahau ile ya Diwani Athumani .oh au kwa vile rais wa TZ yuko juu ya sheria
 
Siku chache zilizopita DC wa Hai, Ole Sabaya alijitokeza mbele ya vyombo vya habari akiwatuhumu wamiliki wa mabasi ya Limu Safaris na Machame Safaris kuwa wameunda magenge ya kiuhalifu ya uhalifu ya kuhujumu reli kati ya Moshi na Arusha na hivyo akawataka wamiliki wa mabasi hayo wajisalimishe kituo cha polisi cha Boma ng'ombe ili wajibu tuhuma zao

Wamiliki hao wa mabasi walitii amri hiyo ya DC Sabaya ya kuripoti kituo cha Boma ng'ombe kwa wakati alioagiza DC huyo Sabaya

Baada ya wamiliki hao wa mabasi kuripoti Polisi, RPC wa Kilimanjaro, Salum Hamdun, alijitokeza hadharani kueleza namna wamiliki hao waliivyoweza kutii amri bila shuruti na akaeleza pia namna Polisi hao waliivyofungua jalada la uchunguzi na namna uchunguzi wao ulivyoenda

RPC huyo akaeleza waziwazi kuwa baada ya uchunguzi wao, wamebaini kuwa hakuna hujuma yoyote iliyofanyika katika kipande hicho cha reli kati ya Moshi na Arusha kama aliivyodai DC Ole Sabaya

Ndipo hapo ninapojiuliza ni kwanini Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli, hamfukuzi kazi DC Sabaya kwa kusababisha usumbufu mkubwa kwa wamiliki hao wa mabasi ambao imekuja kuonekana kuwa tuhuma ambazo walipewa na Mkuu huyo wa wilaya kuthibitidhwa kuwa ni za uwongo?

Vile vile hii si Mara ya kwanza kwa Mkuu huyo wa wilaya ya Hai kukumbwa na kashfa za aina hiyo za kuwasingiziia wafanyibiashara kuwa wanahujumu uchumi kwa kukwepa kulipa kodi na baadaye kuja bainika kuwa ni uwongo aliowazushia

Hivi tutaendelea kufanya kazi na wakuu wa wilaya wa "dizaini" ya huyo Mkuu wa wilaya ya Hai hadi lini?

Tafsiri tunayoipata wananchi ni kuwa kumbe baadhi ya wateule wa Rais wana "impunity" na hawawezi wajibishwa kwa makosa ya wazi kabisa wanayowafanyia wananchi kwa visa tu kwa kutumia vyombo vyetu vya dola, kama vile Jeshi letu la Polisi kuhalalisha uharamia huo!
Umesahau kuwa mwenzake Blasius Byakanwa alipoharibu miundombinu ya shamba la Mbowe ndipo alipopandishwa cheo na kuw RC? Soon utasikia naye kapewa cheo cha juu zaidi
 
Wateule wa rais, hawafanani, kuna ambao hata wakikoseshwa wanatumbuliwa na wengine hata wakosee vipi wataendelea.

P
Inategemea na zama
 
Kusema uongo na kubambikia watu makosa kwa kichaka cha uzalendo, ni moja ya sifa kubwa kwa sasa ndani ya hii nchi. Hakuna hatua yoyote atachukuliwa maana huo ndio utamaduni wa sasa.
Kwenye yale mashtaka haliwezi ongezeka likawa shitaka la Saba
 
sabaya with bashite style mwsiho wake utakuwa mbaya kama jina lake,sijui baba yake alikosa jina la kumpa
It's true

Kwa kuwa hivi sasa huyo Sabaya anasota katika gereza la Kisongo.

Alidhani mwendazake ataishi milele!
 
Back
Top Bottom