Yule Mzee ana hoja za msingi sana. Siku likiwakuta yanga watamkumbuka. Leo hii likitokea la KUTOKEA Hersi atalinda maslahi ya GSM na sio ya club...ndo hivyo wabongo wengi vichwa maji na hawawapendi watu wenye maono na akili.
Na hii ipo Kila mahala na ndo MAANA tuko hapa tulipo.
Magoma alindwe na ajilinde asije akapotea...anagusa maslahi ya marenga
Mbona mzee Kilomoni aliyekuwa analinda maslahi ya Simba mlimuona takataka? Ukiona jambo la Yanga, Simba wanalisapoti ujue lina manufaa kwao Simba na ukiona jambo la Simba, Yanga wanalisapoti ujue lina manufaa kwao Yanga. Hivi vilabu vuwili hakuna anayefurahia kufanikiwa kwa mwenzie.
Ni kweli Hersi anapigania maslahi ya GSM, ila Yanga ipo hapa sababu ya GSM na mashabiki na wanachama wameridhika kwasababu wanaamini katika mchakato uliopo chini ya GSM.
Hatua ya kwanza ilikuwa namna ya uendeshaji wa klabu hilo limefanyika kwa msaada wa La Liga.
Hatua ya pili ni uadaji wa katiba hilo tayari na imepitishwa na hiyo katiba ndiyo inayotoa kibali kuwe na raisi, na raisi alichaguliwa kupitia mkutano mkuu wa wanachama.
Hatua inayofuata ni kuisajili Yanga kuwa kampuni na kuithaminisha Yanga ili kupata wawekezaji wasiopungua watatu.
Wakati mchakato wa transformation unaendelea kufanyika, GSM wanaendelea kuisimamia klabu ila mimi kama shabiki sioni jambo baya mpaka sasa hata kama GSM na Hersi wakiwa wanapata maslahi. Sababu ya kusema hivyo ni
1) Yanga wameipandisha thamani Africa hata ikitokea wawekezaji wakaja, wanakuja kuikuta Yanga ikiwa ni brand kubwa Africa. Saivi ukienda Africa kusini wanaijua Yanga na wanaizungumzia Yanga, ukienda Congo hivyo hivyo tofauti na zamani.
2) Kufanya vizuri katika mashindano ya CAF hakuna shabiki wa Yanga na mwanachama asiyependa, hakuna shabiki anayetegemea apate mgawo wa pesa kupitia timu bali ni mataji na kufanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali ikiwemo ya kimataifa.
3) Tunaona wachezaji wenye viwango na ubora pamoja na benchi la ufundi lenye ubora. Hata kama mtu anaiba ila anazingatia kufanya kitu kwa usahihi kwa zaidi ya asilimia 75 sio mbaya kwasababu tuona pesa inatumika kufanya mambo mazuri na makubwa na matokeo yake tunayaona viwanjani.