Ni kwanini Hayati Magufuli alipata Mental na Spiritual Immortality?

RNA

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2013
Posts
1,647
Reaction score
2,803
Habari JF,

Mwezi March mwaka 2021 tulimpoteza moja ya Kiongozi Bora kuwahi kutokea katika Taifa letu.

Lakini Sasa hivi ni kama Mwaka na Nusu lakini huyu Kiongozi ni kama kaondoka Juzi, yaani haiwezi pita siku Mbili hujakuta akizungumzwa au ukakutana na kitu na kitu au mazingira ambayo yatakufanya Umkumbuke.

Binafsi nliamua kufanya Juhudi kujua kwanini huyu asitoke vinywani na akilini mwa watu. Nilifanikiwa kukutana na Mzee Mmoja mtu wa Imani sana alinijibu Kiongozi huyu alitoweka Kimwili ila kiakili na kiroho ataendelea Kuishi - hatokufa, alienda mbali akasema na kuna baadhi ya watu watakuwa wanawasiliana nae kabisa.

Swali kwanini huyu kiongozi alipata hii Mental na Spiritual Immortality?

Ni mtu wa Mungu?

Alikuwa Mioyoni mwa watu?

Alifanya vitu/matendo yaligusa sana Wananchi?
 
Kuondoka kwake kunatia Mashaka sana. Hata hivyo wananchi bado wanaamini angekuwa hai mambo yangekuwa yamepamba moto.

Tuendelee kuomba tupate kiongozi anae beba njozi na mwenye uchu na rasilimali za nchi.

Utouh amesema 1.2t imepigwa kipindi cha dhalimu. Sasa hizo Njozi na uchu na raslimali unatoka wapi? Yule alikuwa mzalendo wa mdomoni, lakini kiuhalisia alikuwa mumiani.
 
Hiyo yote inasababishwa na uzwazwa & ukilaza wa watanzania bara

Mtu kakopa mikopo yenye riba za kibayport halafu bado mnamsifia eti kwa sababu alowaziba midomo wote waliokuwa na uwezo wa kiwaelezea watanzania kuwa hata ATCL na mindege yake iliyolipiwa cash ni jipu lililotakiwa kutumbuliwa haraka
 
Kuondoka kwake kunatia Mashaka sana. Hata hivyo wananchi bado wanaamini angekuwa hai mambo yangekuwa yamepamba moto.

Tuendelee kuomba tupate kiongozi anae beba njozi na mwenye uchu na rasilimali za nchi.

Tatizo Magufuli alitaka kupambana na nguvu ya Lissu. Kamtwanga Lissu risasi akapona. Kwenye uchaguzi katumia hila zote Lissu asipate chochote, lakini kaambulia miezi mitatu tu madarakani. Kamuacha Lissu yupo hai na analipwa stahiki zake na marupurupu yake aliyotaja kumnyima.
 
Ongezea
Mnyeti Alexander
Kheri James
Doto James
Na wasijulikana
 

Kuna watu huwa wanadakia chorus bila kujua mtunzi ni Nani. Huwezi kupoteza raia wako mwenyewe ukaitwa shujaa. Alikuwa muoga ndio maana katumia nguvu nyingi kuiba kura Ila akuambulia chochote zaidi ya kukaa miezi mitatu tu madarakani.
 
Kila jambo na wakati wake.

Lissu alikuwa mhujumu uchumi na hilo Halina mjadala.

Lissu alikuwa anatumia njia za kijanja kutaka nchi ipite kwenye umasikini. Bila Magufuli kusimama imara hata hizo ndege aambazo tunapanda leo tusingekuwa nazo.

Kwahiyo kumtetea Lissu aliyetaka taifa zima liingie kwenye shida inahitaji moyo. Ila kwa sababu nae ni binadamu twendelee.
 
... katika imani zetu Shetani hutajwa sana kuliko malaika na watakatifu wa Mungu. Maonyo yote ni dhidi ya Shetani; Amri Kumi, indirectly ni dhidi ya Shetani. So, sometimes kutajwa sana inaweza isiwe ni ishara njema au kwamba anayetajwa ni mwema sana. Huweza kutajwa sana kwa sababu ya ubaya wake pia.
 
Utouh amesema 1.2t imepigwa kipindi cha dhalimu. Sasa hizo Njozi na uchu na raslimali unatoka wapi? Yule alikuwa mzalendo wa mdomoni, lakini kiuhalisia alikuwa mumiani.
Mbwembwe tu. JPM angetaka pesa angekuwa juu Sana. Lakini pesa zilienda zote kwenye miradi ambayo hadi Sasa wanahaha kuimalizia.

Ni ngumu sana kuuamunisha umma kwamba JPM alikuwa fisadi.
 

Kama muhujumu uchumi anapigwa risasi, tutajie waliopigwa risasi kwenye fedha za escrow, Kagoda nk. Kuna 1.2t zimepigwa kipindi cha dhalimu former CAG Utouh kasema. Onyesha waliopigwa risasi kwa upotevu wa fedha nyingi kiasi hicho.
 
Mbwembwe tu. JPM angetaka pesa angekuwa juu Sana. Lakini pesa zilienda zote kwenye miradi ambayo hadi Sasa wanahaha kuimalizia.

Ni ngumu sana kuuamunisha umma kwamba JPM alikuwa fisadi.

Kaacha deni kubwa kuliko miradi aliyoinzisha. Labda kama ulikuwa unaamini propaganda zake, huku akiwa ameziba mdomo vyombo vya habari.
 
Na huyu aliyepo ndiyo siyo wa hovyo;anateua wahuni wanazurura vijijini kusambaza mitungi ya Gesi,hiyo ndiyo kazi ya Waziri?Mo mwenyewe anazalisha bidhaa nyingi Ila hatujawahi kumuona akisambaza vijijini 🤣🤣.
Hakuna serikali isiyo ua Duniani,ata wewe ukitaka show chezea serikali ya Hangaya.Mzee wa Msoga aliwafanya nini Dr Ulimboka, Mwandishi wa Habari Mwangosi na Kibanda.Au ulikuwa bado unanyonya ziwa la Mama?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…