Ni kwanini Introverts wana asilimia kubwa kwenye kutoboa?

Ni kwanini Introverts wana asilimia kubwa kwenye kutoboa?

Kufanikiwa ni juhudi tu, uwe mpiga domo au mtu wa mikausho mikali. Kama unajuhudi utafanikiwa tu ila kama ni mvivu hata uwe na michuno kiasi gani utakufa kapuku tu.
Unakaa mwenyewe mwenyewe na huna unachokiongeza kwenye mafanikio zaidi ya kujichua.
 
Nikupongeze kwani nami nikiwa kama Extroverts ni kweli nimeshaanza Kufanikiwa na namiini nitafanikiwa zaidi kabisa.
Huwa tuna enjoy sana post zako unazowekaga humu za waganga wa simba, zinakuwaga na ujazo wa kutosha 🙂

au na wewe umejiingiza huko umeanza kunenepa kwa mbuzi za kafara ? 🙂
 
Usichokijua Wachawi ni wengi kuliko unavyofikiri, wengine hawabebi hata Matunguli hawapai na Ungo Ila wanawanga kinoma tena wanakuwangia Mchana kweupe pee hivi unawaona nimeshuhudia mara nyingi sana wakiwa wanawanga, mtu yeyote anaekuwekea kauzibe katika Jambo lako huyo ni Mchawi
Kabisa mkuu, ndio maana jandoni tulifundishwa ukitaka kununua gari nyamaza kimya, ukitaka kununua kiwanja nyamaza kimya, ukitaka kujenga nyumba nyamaza kimya.
 
Unakaa mwenyewe mwenyewe na huna unachokiongeza kwenye mafanikio zaidi ya kujichua.
Hahaha, alafu unaishi kwa kusema introvert wanafanikiwa. Kuna watu ni wakimya sehemu wanazoishi, ila niwazungumzaji na wachangamfu sana maeneo ya kazi au biashara zao.

Acha watu wajichanganye tu!.
 
Hahaha, alafu unaishi kwa kusema introvert wanafanikiwa. Kuna watu ni wakimya sehemu wanazoishi, ila niwazungumzaji na wachangamfu sana maeneo ya kazi au biashara zao.

Acha watu wajichanganye tu!.
Sidhani kama kwenye kazi za dunia ya leo kuna mambo ya kuwa introvert. Lazima uzungumze na soko lako. Unless unatengeneza software za kurusha vibebeo vya nuclear.
 
Usichokijua Wachawi ni wengi kuliko unavyofikiri, wengine hawabebi hata Matunguli hawapai na Ungo Ila wanawanga kinoma tena wanakuwangia Mchana kweupe pee hivi unawaona nimeshuhudia mara nyingi sana wakiwa wanawanga, mtu yeyote anaekuwekea kauzibe katika Jambo lako huyo ni Mchawi
Jambo lenyewe liwe halali,sio unataka kuiba,kutapeli au kudhulumu halafu anatokea mtu anakuzuia kutimiza malengo yako unaanza kumuita mchawi.
Kuna mtu anakuja kwenye biashara au kazi yako anataka umpe taarifa muhimu, ukimpa anazitumia taarifa hizo kukumaliza,usipompa anaanza kukuita mchawi.
 
Upo sahihi mkuu, piga picha umezungukwa na nyumba za udongo au nyasi halafu unasema utajenga ghorofa katika hayo maeneo!
Kabisa, imagine umenunua gari jirani zako wote hawana, hapo lazima uwe dereva wa mtaa na ukijifanya introvert tu utaambiwa unaringa na utawekewa hata mawe barabarani. Kuna mmoja aliibiwa mchana kweupe, wezi nasikia walikuja na lori wakapakia, jioni majirani wanasema kumbe wezi,? tulijua unahama, Aisee.
 
Sasa wambeya watafanikiwa wapi na kutwa wapo busy kutafuta ya watu, huku introverts wapo busy kuleta maendeleo kwenye maisha yao.
 
Introvert ni upumbavu tu utafanikiwa kutokana na juhudi zako Hakuna cha introvert wala nini
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Sababu hawana mambo mengi,
Hawapendelei drama drama zisizo na maana,
Ni independent hawategemei company katika kufanikisha majambo yao
Endapo wakiwa na malengo kupitia tabia hizo hapo juu wanakuwa rahisi kufikia ndoto zao
 
Jambo lenyewe liwe halali,sio unataka kuiba,kutapeli au kudhulumu halafu anatokea mtu anakuzuia kutimiza malengo yako unaanza kumuita mchawi.
Kuna mtu anakuja kwenye biashara au kazi yako anataka umpe taarifa muhimu, ukimpa anazitumia taarifa hizo kukumaliza,usipompa anaanza kukuita mchawi.
Mimi nimemaliza wewe umenielewa Ila unataka nikueleweshe zaidi mchawi ni snitch kwa Kimakonde maana yake wizard witch kigagula
 
Kabisa, imagine umenunua gari jirani zako wote hawana, hapo lazima uwe dereva wa mtaa na ukijifanya introvert tu utaambiwa unaringa na utawekewa hata mawe barabarani.
Aisee noma sana, umenikumbusha jamaa yangu alinunua gari yake, kitaa yeye ndio ana usafiri. Siku ndio gari imefika majirani wakaja na mtoto kama wa miaka mitano hivi wanaomba apelekwe kituo cha afya kutibiwa na usafiri wa jamaa.
Bahati nzuri jamaa akawauliza kwani mtoto anaumwa nini? Wakamwambia ana jipu, jamaa akawauliza jipu la mtoto lina muda gani? Wakamwambia lina muda zaidi ya siku nne.
Mwamba akashtuka akajua wamekuja kumuwangia, akasema hawa wajinga nitawaonyesha!
Akawaambia waingie kwenye gari, walipoingia gari ilikuwa ni automatic gear, alichofanya akachomeka funguo switch akaweka gear kwenye drive akawa anajaribu kuiwasha gari , funguo haiwashi gari, akazuga zuga kama gari imegoma baadae akawaambia washuke gari imegoma kuwaka, majirani wakasepa zao.

Jiulize hilo jipu la mtoto ni emergency kumpeleka mtoto usiku zahanati? Na je mchana wote walikuwa wapi?
 
Kufanikiwa ni juhudi tu, uwe mpiga domo au mtu wa mikausho mikali. Kama unajuhudi utafanikiwa tu ila kama ni mvivu hata uwe na michuno kiasi gani utakufa kapuku tu.
Oya FM kuna watu wana juhudi za kupasua mawe kule machimbo Ila wapo wapi? Hivi unataka kuniambia wale ni wavivu mtu anapasua mawe kuanzia asubuhi mpaka jioni ndoo 1 kubwa 3000 kwa hio anajitahidi kwa siku walau apasue ndoo 10 arudi nyumbani na 30,000 Ila ameshapondeka mikono na vidole vibaya sana
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Oya FM kuna watu wana juhudi za kupasua mawe kule machimbo Ila wapo wapi? Hivi unataka kuniambia wale ni wavivu mtu anapasua mawe kuanzia asubuhi mpaka jioni ndoo 1 kubwa 3000
Kitu sahihi na muda sahihi vinaendana mkuu.
 
Aisee noma sana, umenikumbusha jamaa yangu alinunua gari yake, kitaa yeye ndio ana usafiri. Siku ndio gari imefika majirani wakaja na mtoto kama wa miaka mitano hivi wanaomba apelekwe kituo cha afya kutibiwa na usafiri wa jamaa.
Bahati nzuri jamaa akawauliza kwani mtoto anaumwa nini? Wakamwambia ana jipu, jamaa akawauliza jipu la mtoto lina muda gani? Wakamwambia lina muda zaidi ya siku nne.
Mwamba akashtuka akajua wamekuja kumuwangia, akasema hawa wajinga nitawaonyesha!
Akawaambia waingie kwenye gari, walipoingia gari ilikuwa ni automatic gear, alichofanya akachomeka funguo switch akaweka gear kwenye drive akawa anajaribu kuiwasha gari , funguo haiwashi gari, akazuga zuga kama gari imegoma baadae akawaambia washuke gari imegoma kuwaka, majirani wakasepa zao.

Jiulize hilo jipu la mtoto ni emergency kumpeleka mtoto usiku zahanati? Na je mchana wote walikuwa wapi?
Hahaha, Hapo unaweza kukuta mchana wote waliona wasitumie nauli sababu kuna jirani ana gari. Unajua kuna watu wa ajabu kwenye jamii zetu, kuna mtu hajisumbui kutafuta ada anajua upo atakuomba msaada sababu unafanya kazi bank. Na hata akipata hiyo ada inaelekezwa kwenye mambo mengine sababu jirani upo utamuelewa tu.
 
Kitu sahihi na muda sahihi vinaendana mkuu.
Yes of course Ila hakuna juhudi zisizo na faida sema unaweza ukawa unafanya juhudi kubwa sana ukawa unapata faida KIDOGO sana alafu kuna mwenzio hafanyi juhudi zozote zile Ila anaingiza faida kubwa sana, wewe unaenda kuhangaika na Jua asubuhi mpaka usiku mijasho inakutoka full kunuka kikwapa wakati mwenzio anaingia kwenye kiyoyozi anatoka kwenye kiyoyozi anaingia kwenye kiyoyozi tena alafu hakuna kazi anayoifanya zaidi ya kugusagusa tu makaratasi na keyboard basi siku imeisha huyo anarudi nyumbani na Mwisho wa Mwezi wanamlipa Bonge la Mshahara kwa kazi hewa hafanyi kazi ni anazuga tu na analipwa vizuri tu na anaishi vizuri tu
 
Back
Top Bottom