Ni kwanini Introverts wana asilimia kubwa kwenye kutoboa?

Ni kwanini Introverts wana asilimia kubwa kwenye kutoboa?

Oya FM kuna watu wana juhudi za kupasua mawe kule machimbo Ila wapo wapi? Hivi unataka kuniambia wale ni wavivu mtu anapasua mawe kuanzia asubuhi mpaka jioni ndoo 1 kubwa 3000
Juhudi, kutumia fursa na bahati. Ukichunguza usishangae kukutana na mnunuzi wa mawe kwa wapasuaji ana lori na huenda alianza na kupasua na kuuza hayo mawe kwa ndoo ndoo.

Kuna kipindi huko nyuma nilikuwa napita pori kwa pori kutafiti fursa za mazao huko vijijini mikoa ya kaskazini Nikakutana na kijiwe kimoja kuna jamaa yeye alikuwa dalali wa mazao tena mdogo anapambana adalalie 20 mpaka 50 juu ya kilo za gunia za mahindi na maharage. Sasa siku moja wakaja watu kutoka nchi nyingine jirani, aisee sijui ilikuaje wakamwamini, walimpa fedha za kutosha awakusanyie mazao na wakatengeneza network yao hawaji tena wanatuma tu yeye anapakia. Alikuwa anawekewa mpaka M600. Sasa huyo ni bahati imemtoa kwenye umaskini katikati ya kupambana.
 
Kufanikiwa huwa kunategemea zaidi utakavuokuwa unazingatia haya mambo.

Get
Manage
Multiply

Kuna watu hupata hela (Get ) Ila huishia katika kuzipoteza zote ktk anasa

Pia kwenye manage -sio kila MTU anaweza kumiliki anachokipata

Na katika multiply - wapo watu wachache Sana hufanikiwa kukizalisha au kukizidisha walichonacho.

Doesn't matter ur introvert or extrovert if you can't handle these principals you will end up being broke and dumber
 
Oya FM kuna watu wana juhudi za kupasua mawe kule machimbo Ila wapo wapi? Hivi unataka kuniambia wale ni wavivu mtu anapasua mawe kuanzia asubuhi mpaka jioni ndoo 1 kubwa 3000 kwa hio anajitahidi kwa siku walau apasue ndoo 10 arudi nyumbani na 30,000 Ila ameshapondeka mikono na vidole vibaya sana
Hiyo sio juhudi, huko ni kutumia nguvu za mwili. Juhudi na matumizi ya nfuvu za mwili ni vitu viwili tofauti Mkuu.

Inahitajika juhudi kujifunza na kutafuta maarifa, je hao wapasua kokoto wanafanya hivyo?. Na mifano mingi ya kutofautisha.

Ila, kufanya kazi ngumu sio kigezo cha kufanikiwa, kuvuja jasho hakukupi uhakika wa kufanikiwa, juhudi sio kuutesa mwili bila faida na mwisho kabisa, kuamka mapema sio kigezo cha kufanikiwa ikiwa utaamka saa 11 asubuhi halafu hauna mchongo wa kufanya.
 
Muhimu: Elewa neno asilimia kubwa haimanishi ni wote, hata wazaramo wakimya wapo lakini asilimia kubwa ni waongeaji.

Introverts ni watu ambao wanapenda kuwa peke yao muda mwingi, mkikutana mnasalimiana, anaweza kukusaidia, n.k. wepo waongeaji wazuri tu lakini bado wanapenda muda mwingi kukaa wenyewe, ni tofauti na mtu ambae hajibu salamu, hataki kusaidia wengine, n.k.

Introverts ni wachache sana lakini wana asilimia kubwa kwenye kufanikiwa kupitia masomo, ubunifu, teknolojia, n.k.

Kwenye uwanja wa teknolojia wengi ni introverts kina Elon Musk, Bill Gates, Mark Zuckbereg, Jeff Bezos, Steve Jobs (rip), n.k. pia ni mabilionea.

Wanasayansi wengi walioleta magueuzi kama Isaac Newton, Albert Einsten, n.k. ni introverts.

Wale kina John Kisomo wa shuleni ilikuwa kawaida kukuta ni introverts, mtu kapata 98% anaenda kulalamika kwa mwalimu kapunjwa, huko vyuoni waliendelea kugonga gpa za juu kiasi cha kubakizwa kuwa lecturers.

Messi ni Introvert ni mchezaji bora kuwahi kutokea kwenye mpira, Wachezaji wanakiri wenyewe kwamba wanalazimika kukusanyika hata sita kumkaba yeye tu.
Hata mwekezaji maarufu, Warren Buffett ni INTROVERT!
 
Unajua alafu huna mtaji alafu hapo hapo huna wa kukushika Mkono alafu kuna mshenzi anakuona kabisa wewe unajua Ila kwa sababu unajua kumzidi yeye anasema ngoja afe kivyake siku ukipasua mawingu namjua namjua zinakuaga nyingi sana hata wakikuona kwenye Shideo utasikia "nilisoma nae yule"
Yeah iko ndo nilichopitia ila kinafikia mwishoni soon watakuja kunilamba miguu nawawekea pilipili ***** zao
 
Hahaha, alafu unaishi kwa kusema introvert wanafanikiwa. Kuna watu ni wakimya sehemu wanazoishi, ila niwazungumzaji na wachangamfu sana maeneo ya kazi au biashara zao.

Acha watu wajichanganye tu!.
Nafikiri uintrovert na uextrovert bado haujaeleweka vizuri kwa watu wengi.

Kuwa introvert au extrovert si hali ya kujitakia. Ni ya Kisaikolojia/Kibaiolojia.

Haimaanishi introvert hawezi kuwa muongeaji au mtu wa kujichanganya na wengine, bali yeye hana uhitaji huo kama extrovert.

Extrovert hupata nguvu zaidi (hamasa n.k.) anapokuwa na watu, wakati yeye introvert amejitosheleza. Akiwa na watu ni kama vile unamuovercharge. Baada ya muda atahitaji kujitenga na kuwa peke yake kwa ajili ya kujipooza/ kurudi katika normal energy

Kwa kawaida, yeye akikaa muda mrefu penye kusanyiko la watu, baada ya muda hutamani kuondoka.

Kwenye mikusanyiko ya watu wengi kama sherehe, ni introvert ndiyo mara nyingi wanaokuwa wa kwanza kuondoka, hata kabla ya sherehe kuisha.

Introvert anaweza kuongea sana akiamua, na anaweza kujichanganya na watu bila shida, ila hajisikii kuwa comfortable kuwa kwenye kundi la watu wengi kama ilivyo kwa extrovert.

Anayamuda mazingira yote, ya kuongea, kujichanganya na watu, ya ukimya na ya kukaa peke yake, lakini aliyo comfortable nayo zaidi ni ya kukaa peke yake na ya ukimya.
 
Wapo ambao hawajafanikiwa kabisa, wapo wapo tu mitaani wala hawatengenezi networking. Nadhani haya mambo ya mafanikio siri ni bahati, kutumia fursa na kuwa na bidii bila kujali sana mambo mengine. Halafu most of time unavyopata mafanikio ndivyo unavyopunguza circle ya marafiki na unaonekana introvert.
bonge la fact mkuu
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Ukijua nguvu ya meditation huu uzi haupaswi kuwa mrefu. Hao watu ni meditators wazuri sana na meditation huamsha idea ambazo huenda hazijawahi andikwa mahala popote pale.
 
Back
Top Bottom