Mchango wake kwenye sanaa ya bongo sio wa kubeza lakini alichukuliwa poa.
Hakuwa msanii aliebahatisha kutoa Hit moja au mbili akapotea, Alihusika kwenye Hits 5, Ni wasanii wa kike wachache sana waliweza kutoa hits zaidi ya 3 (Ray C, Jide, Enika, n.k.), Sio rahisi !!
Zifuatazo ni hits zake 5 alizowahi kutu bless kwenye bongo fleva
- Nikipata wangu
- Crazy over you ft Squeezer
- Nalia kwa furaha ft Bushoke
- Nishike mkono ft Blue
- Chochote utapata ft Noorah
Kwa mtazamo wangu sina ushahidi lakini navyoona K Lyn alikuwa na pesa nje ya muziki, alikataa unyanyasaji na unyonyaji wa media kubwa, mapromota wanyonyaji nao walishindwa kumnasa hivyo ikapelekea kupewa airtime kidogo kinyume na ukubwa wa hits zake pamoja na kuwa shows chache ambazo hazikuendana na kiu ya mashabiki, Muziki aliufanya kama hobby ya kufurahisha mashabiki zake kuzidi maslahi.