Ni kwanini kila migogoro ikitokea Dangote Cement lazima Obasanjo atue nchini?

Ni kwanini kila migogoro ikitokea Dangote Cement lazima Obasanjo atue nchini?

FisadiKuu

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2015
Posts
8,169
Reaction score
13,455
Wasalaam Wakuu,

Hivi ni kwanini kila kunapotokea changamoto/ mgogoro kwenye kiwanda cha Dangote Cement Mtwara basi ndani ya siku chache tu lazima Rais Mstaafu wa Nigeria Obasanjo atue nchini na kuzungumza na Mkuu wa Nchi?

Ilitokea hili mara mbili wakati wa Rais Hayati Magufuli, na hivi majuzi badala ya mgogoro wa kiwanda na madereva nasikia leo hii Obasanjo ameonana na kufanya mazungumzo na Rais Mama Samia.

Kuna nini nyuma ya pazia Kati ya Dangote Group na Obasanjo?
 
Ninakumbuka awamu ya nne kuna mama Mtanzania alisema yeye ni mke wa Mzee Obasanjo na alitapeliwa kiwanja wakati anataka kuwekeza Tanzania.

Lakini katika profile ya Obasanjo hakuna maelezo ya kuwa na mke Mtanzania. Inawezekana mama ni mpango wa kando.

Huyu mzee ni shemeji yetu.
 
Obasanjo ni rais mstaafu wa Nigeria ili kukwepa kunyooshewa kidole na wananchi kuwa na ukwasi uliopindukia akashikana na nduye Dangote kuwekeza huko kwao na nchi zingine kwenye uwezekano wa kukuza biashara hiyo ya simenti.

Hata hapa kwetu kuna baadhi ya makampuni ukiyagusa kwa nia njema lakini inayohatarisha ustawi wake wa kiuchumi , kuna viongozi waandamizi wa kisiasa watatafuta niia kwenda mkuu wa nchi kulegeza.

Endapo atagomewa anaweza kushawishi kuhamisha mitaji kwenda nchi nyingine kisha kuanza kupiga kelele kupitia vyombo vya habari kwamba kuna unyanyasaji, dhuluma na uonevu pamoja na mazingira yasiyo rafiki kwa biashara.

Hilo litambue leo na kuendelea, wana maslahi humo
 
1620056952755.png

FisadiKuu

huenda madereva wa Dangote sasa wakalipwa, hapo hakuna kudhulumiwa, labda na makaa ya mawe mchuchuma na gasi vikatolewa kwa punguzo ili uendeshaji kiwanda uwe nafuu
 
View attachment 1772376

FisadiKuu

huenda madereva wa Dangote sasa wakalipwa, hapo hakuna kudhulumiwa, labda na makaa ya mawe mchuchuma na gasi vikatolewa kwa punguzo ili uendeshaji kiwanda uwe nafuu
Kipindi cha Mzee Magufuli Dangote waliyumba na kusuasua sana kwenye biashara yao.. Nadhani sasa bei ya Cement itarudi kule ambako Dangote waliplan ifike.. Na hilo la makaa sina shaka lazima limezungumzwa.

Muda ni wakati mzuri sana Mkuu, ngoja tuone..
 
Use

Uwe unaangalia na aina ya utani mkuu ukiona huwezi nyamaza tu...unaweza kujiletea shida siku nyingine ohooo..yule sio rika yako..

Umemkaripia vema. Ni vizuri kuwepo na mipaka ya utani.

Asante mkuu kumbe na wewe umeona kuna aina za utani na watu na mahali pa utani.

Vijana wa JF bwana mnapigana jeki naona

Sasa unadhani huyo mama hakusema kuwa ni mke wa Olisegun au??

Au mlikua hamfwatilii bado maswala ya nchi ndo mmeanza juzi???

Halafu mnajua umri wa Sky Eclat ???

Wengine humu wanamtania Obasanjo ndo rika lao......kaeni kwa kutulia

NB: Hata mimi nilimshuhudia huyo maza akilalamika. Na anakaa mbezi beach mpaka leo hii yupo Tanzania hii
 
Wala hukuelewa nili

Wala hukuelewa nilichoongea asikiaye na afahamu acha kudandia gari kwa mbele.
 
Back
Top Bottom