Ninachojua kwa Afrika hii hakuna Tajiri ( Bilionea ) ambaye ameibuka tu Mwenyewe bila Nguvu wa Kiongozi wa nchi.
Inasemekana Utajiri wa Dangote una mkono mkubwa wa huyo Rais Mstaafu wa Nigeria Obasanjo.
Inasemekana Utajiri alionao Mukwano ( si Jina lake halisi bali ni Brand Name yake tu ) wa Uganda una mkono mkubwa wa Familia ya Rais Museveni.
Inasemekana Utajiri mkubwa wa Familia ya akina Gupta huko Afrika Kusini ina mkono mkubwa wa aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma.
Inasemekana Utajiri mkubwa alionao Salim Said Bakhressa una mkono mkubwa wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa ( zamani OAU ) Balozi Salim Ahmed Salim ( japo pia Wameoleana ) vile vile.
Ilisemekana kuwa Utajiri mkubwa aliokuwa nao Yusuph Manji ulikuwa na mkono mkubwa wa Rais Mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete.
Inasemekana Utajiri mkubwa alionao Patrice Motsepe ( Rais wa CAF ) na pia Mmiliki wa Klabu kubwa na Tajiri sana Afrika Kusini ya Mamelodi Sundowns una mkono mkubwa wa Rais wa sasa wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa.
Inasemekana hata Utajiri aliokuwa nao Hayati Reginald Mengi una mkono mkubwa wa Waandamizi Watatu ( 3 ) wa Chama Tawala ( CCM ) na Mmoja sasa ni Marehemu.
Na inasemekana pia Utajiri mkubwa alionao Mo Dewji ( ambao ameurithi kutoka kwa Baba yake Mzee Ghullum ) nao pia una mkono wa aliyekuwa Rais wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi.
Ni vigumu mno kwa Bara hili la Afrika Mtu 'Kuibuka' tu kuwa Tajiri ( Bilionea ) bila kupigwa 'Tafu' na Marais wa nchi zao husika.