Ni kwanini kila migogoro ikitokea Dangote Cement lazima Obasanjo atue nchini?

Jaribu kuwa na fikra hata kidogo.
 
Afanye yote lakini ajue kwamba ata colombia na haiti kulikuwa na madini leo kuna mashimo tu na hao wanaoitwa wawekezaji hawapo tena.
 
Punguza utundu.
 
Matajiri wengi huwa wanawapa hisa au vyeo Marais wastaafu au mawaziri wakuu kwa mambo kama haya na pia kampuni kuaminika zaidi.

Jambo la kawaida sana wakubwa kuwa Directors.
GAZPRON na bomba la mafuta huko Ujerumani kutoka Russia, Mwenyekiti wa Bomba ni Chancelor Mstaff Shoda.
 
Vijana wa JF walizani unamaanisha huyo Mama alikua Mama Samia,kumbe ni Mwanamke mwingine sema nae ni Mtanzania!!,kwa jinsi nilivyokuelewa Mimi!!
Ndio hivyo mkuu....wasijifungie kwenye boksi na tafsiri zisizo sahihi

Huyo mama ni mfanyabiashara tu
 
GAZPRON na bomba la mafuta huko Ujerumani kutoka Russia, Mwenyekiti wa Bomba ni Chancelor Mstaff Shoda.

Yaani viongozi wengi lazima wawe kwenye makampuni makubwa
Nakumbuka kina John Major na hata Gordon Brown ni wamoja wa wanufaika wa makampuni makubwa
Yaani jamaa wanakula hela taratibu
 
Hawa ni marafiki kwelikweli. Dangote alifadhili kampeni za Obasanjo. Ni wazi alipata mikataba minono ya serikali.
 
Na popote aingiapo Dangote, anapenda kuanzia nyumba kuu, kisha anakuwa na nguvu ya kiimla kwa mwenye nyumba baada ya kufanikisha ya mwenye nyumba.

Aliletwa na nani umesema? Amefanyaje hii wiki umesema?

Kazi iendelee
 
Kama aliiba na kuwekeza hapa hapa Afrika hio hela inasaidia waafrika wao ni umiliki na maaamuzi tu.
Khadaf i aliiba akaenda kuficha ufaransa kilichojiri mnakijua, kuna matrilioni ya dola yaliibwa na viongozi wa Afrika na kufichwa ulaya yanawasaidia wazungu.
 
Ukiwa na kampuni lazima uwe na Public Relation team itakayokusaidia kufanya lobbying kwa viongozi wa juu wa nchi wenye maamuzi ili kufanikisha malengo ya kampuni ndiyo maana Dangoti hapati shida kumwona Rais.
 
Uchumi ni siasa,Dangote ni home grown company ya Nigeria,imeitangaza nigeria duniani,Ili mambo ya Dangote yanyooke lazima uwatumie watu kama Obasanjo Rais mstaafu katika PR,na mahusiano ya nje na wakuu wa nchi nyingine,
Ebu fikiria Kikwete akipewa Kazi ya kuitafutia Wasafi media deal marekani,China,UK,kitendo Cha kumtimua mtu kama Raisi mstaafu katika mambo ya kibiashara Ili kufanikisha deals ni akili kubwa.
 
Ukiwa na kampuni lazima uwe na Public Relation team itakayokusaidia kufanya lobbying kwa viongozi wa juu wa nchi wenye maamuzi ili kufanikisha malengo ya kampuni ndiyo maana Dangoti hapati shida kumwona Rais.

Yaani kama kina Kikwete wangekuwa na shareholders tuseme kwa mfano sekta binafsi ya madini au biashara kubwa kama kina bakhressa
Hapo kuingiza biashara moja kwa moja kwenye soko la dunia bila mikwara ni kawaida sana

Tatizo viongozi wetu hawaoni hizo fursa ila wote wanaishia Kulima mihogo na kufuga ng’ombe tu
 
Mzee Obasanjo hanaga shuguli maalumu..anazurura tu. Hata wewe ukiwa na harusi unaweza kumualika
Nafasi aliyoshika inamfanya kuwa PR mzuri kutengeneza mahusiano na kampuni na nchi mbalimbali, ndiyo maana makampuni kama Pepsi.Nike au Adidas wanawatumia Messi au Ronaldo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…