Mkuu unamjua genius? Hao ni watu special sana. Nchi nzima wanaweza wasifike watano. Nafikiri wewe unaongelea waliokua wanaongoza darasani. Olevel na alevel nimesoma special schools nimesoma nao hao watu. Ambao ninafahamiana nao mpaka leo wengi ni diaspora na waliopo hapa nchini wapo vyema kiuchumi na wengine wana kampuni zao binafsi
Watu waliosoma hawanaga makelele ndio maana hata wakitoboa wanakua ile low key, tofauti na ambao hawajasoma wakianza kushika hela wana makelele sana. Ni rahisi kumjua dotto magari kuliko kumjua benjamin fernandez. Hii ndio imepelekea jamii kujenga taswira kwamba hawa wanaoongozaga darasani wakifika mtaani huwa wanafeli kimaisha, lakini sio kweli. Wengi wanafanya vyema kwenye field zao sema wapo low key sana