Ni kwanini Makonda anakagua miradi iliyotekelezwa na Serikali na kisha kuikabidhi kwa CCM?

Ni kwanini Makonda anakagua miradi iliyotekelezwa na Serikali na kisha kuikabidhi kwa CCM?

Ncha Kali

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2019
Posts
15,335
Reaction score
29,114
Ndugu zangu, au mimi tu sielewi hii kitu!

Nauliza ili nipate kujua, nimekuwa nikishangaa huu mkakati wa Paulo Makonda, RC Dar es Salaam. Sijawahi kuona kabla, pengine ni kwa vile sijui!

Kama hiyo haitoshi, anatumia nafasi hiyo kuwadhihaki watu na kuwananga ikiwa mbunge wa eneo la mradi hatokani na chama chake.

Pamoja na ukweli kuwa serikali iliyopo madarakani inatekeleza ilani ya chama chake, ni nini kinawapa umiliki namna hii?

Miradi ya maendeleo, miradi ya serikali, ni vipi inakabidhiwa kwa chama? Je, ni mali ya chama?

Maendeleo hayana vyama!

Wasalaam,

Ncha Kali.
 
Chama cha mapinduzi ndicho kinaisimamia serikali kwa hiyo ikikamilika inakabidhiwa ripoti kwa chama na kukabidhiwa kwa chama kuwa sisi kazi mliyoyututuma serikali tufanye hiyo hapo tunawakabidhi.
Safi kabisa
 
Miradi yote iko chini ya chama cha mapinduzi
Ulitakiwa kuhisi aibu kwa kauli kama hiyo.CCM iliandaa ilani,walipotangazwa washindi 2015 waliikabidhi ilani hiyo kwa serikali,ambayo inatekeleza. Hivyo hiyo miradi ni ya umma/serikali na chama hakuna nafasi humo zaidi ya usanii. Ni bahati mbaya haya yanafanyika kwa gharama za walipa kodi.

Yote hiyo kimsingi ni hofu ya CCM dhidi ya kukataliwa na Wananchi pamoja na kujimwambafy kwa miaka 5 bila misukosuko. Wapinzani wanaokejeliwa bado ni tishio kwa CCM ndiyo maana wamejaa hofu(fear&stress).
 
Ncha Kali,

Mbunge anaulizwa KUHUSU barabara na stendi anasema hivyo si VIPAUMBELE VYAKE
Makonda akawauliza CCM juu ya ilani yao iliyopita jimboni hapo...akajibiwa ipo hivi;

1. Kujenga barabara kila chochoro
2. Kuipanua mitaro ya Jimbo kwa kiwango Bora.

Makonda akasukuma hayo na Leo alhamdulillah amefanikisha kwa yafuatayo;

1. Mpango wa kilomita 111 jimboni ubungo.
2. Mpango wa kilomita 40 za kuipanua vyema njia za mito inayotiririka jimboni na wilayani hapo.

UKITAFAKARI UNAYAELEWA VYEMA.
 
Ncha Kali,

Huyu anasubiri firing squad come 2020!

Sababu mauaji ya Ben Saanane, Utekaji wa kina Roma mkatoliki, Mauaji ya Diwani wa Hananasifu na mengine mengi. Uzuri ni kwamba tayari yuko kwenye list ya No-fly -Ban anakikanyaga tu kwenye international airport yoyote duniani anakula bangili za chuma!! Mwacheni atapetape!
 
Back
Top Bottom