Ni kwanini Makonda anakagua miradi iliyotekelezwa na Serikali na kisha kuikabidhi kwa CCM?

Yaani huyu anaharibu kabisa natamani nimwambie Raisi huyu anakuharibia hicho anachokifanya ni rabish matokeo yake anawapigia campaign wapinzani kwa kuonyesha kuwa CCM hawajafanya kitu huku akiwataja taja CHADEMA.Yaani Katibu mkuu ,review hiki anachokifanya Makonda please
 

Hapa kila mtu anakushangaa small-minded person. Na watu wa aina hii ni wengi sana na ndio shida ya nchi hii. Nchii hii itasonga mbele kadiri akili kama zako zinavozidi kupungua.

Umeshindwa kutambua kuwa point hapa si nani anaongoza serikali. Bali β€œkuikabithi CCM miradi”. Nakukumbusha - ona tofauti kati ya CCM na serikali. Serikali (inayoongozwa na CCM) hii inafanya kazi kwa niaba ya watanzania!! Miradi ya CCM ni ile iliyogharimiwa kwa fedha za CCM. Mambo yanayofanywa kwa kodi ni mali za watanzania kwa ujumla wao!!

Makabidhiano kati ya RC na CCM ni propaganda. Miradi hii si ya CCM, ni ya waTanzania!!
 

Mi sina mashaka na mtazamo wangu juu yako, una uelewa mdogo mno kiasi kwamba sitarajii kitu kikubwa kutoka kwenye mchango wako... siwezi tu kukupuuza.

Na hata hapo ni kwamba umejitahidi sana, unastahili pongezi mno... tuko tofauti ila tunavumiliana.

Uko sahihi!
 

Akili yako na ya Mpuuzi Mchezaji na Nahodha wa Azam FC Frank Domayo aliyemuumiza vibaya leo Beki wa Simba SC Shomari Kapombe ni sawa tu.
 
Kama ilivyo kwa Iran kutoa hati ya kukamtwa Trump na kuomba Interpol isaidie kwa kosa la kumuua mkuu wao wa operation za mafunzo ya kijeshi, waliyotoa wiki iliyopita.

Nami natoa hati ya kukamatwa kwa mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda kwa kosa la kufanya ziara ya ki-serikali akiwa amevalia mavazi ya kichama akiongozana na wana-CCM kwa kutumia gharama za serikali, huku akionekana kufanya zaidi siasa kuliko kufanya kazi ya umma, haya ni matumizi mabaya ya pesa za umma na naagiza akamatwe.

IGP Sirro, saidia hili.

Usiniulize mimi ni nani, mpaka niagize hivi? Kwani Iran amewazaje?

Ebooo 😎
 
Nakuombea pia kwenye hili... Nakuombea sana
 
Tatizo la Makonda limeanzia mbali, kumbe hii kukabidhi miradi alikuwa anakabidhi kila kitu!
 
Alikabidhi miradi yetu pamoja na dhamana tuliyomwazima, sasa apumzike kwa amani.
 
Kwa sasa unaweza kumshitaki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…