Ni Kwanini Mdude Nyagali hakamatwi na hachukuliwi Hatua Kali Kwa Kuendelea Kumchafua Rais Samia Bila Ushahidi?

Mkuu, Afrika huwa tunakosea sana kuamini kuwa Rais ana immunity ya maisha! Tukumbuke naye ni binadamu, anakosea kama tunavyokosea wengine! Anakwenda msalani kama sisi, na ana kila kitu cha ubinadamu kama wewe vile, idadi sawa ya vidole, meno, na mifupa. Tunapata wapi ujasiri na nguvu ya kumuona mtumishi wa umma kama mungu?! Samia sio Aphrodite wala Athena ni binadamu kama binadamu wengine.

Akikosea lazma aambiwe kwa sababu ni tabia na asili ya kila mwanadamu kukosea. Wengi wanafanya kumuogopa na kumtukuza ila bado atabakia kuwa mwanadamu tu. Kina Mobutu Sese Seko na fujo zake sasa hivi yupo wapi!? Joseph Stalin na ubabe wake wote sasa hivi yupo wapi!? Unataka kusema Samia huwa hafanyi makosa, hatukani watu, hana mawazo mabaya?! Je haombi toba na msamaha kwa Mola wake!? Kama tu wateule wa Mungu walikuwa wanamuomba Mungu tobacco na msamaha mara kibao sembuse Samia?! Acheni kujionesha kama mnajua Samia sio binadamu!

Mdude amekosea wapi!? Tatizo kila mtu anataka kuonekana ni kama mtume wa Samia! Ujinga wa kiwango cha lami kabsa. Kuna wahuni wanampatia heshima kubwa kuliko hata wazazi wao.​
 
Wewe ni hakimu wa mitandaoni?

SATIVA amemtaja Mafwele kama mmoja wa watesi wake na aliyetoa amri auawe. Mbona haujasema lolote kuhusu hilo?

Wewe unaashiria ni mmoja wa wanaoshangilia utekaji nyara na mauaji ya raia. Labda ni mmoja wa watekelezaji wa mpango huo.
 
Kumtaja tu mtu pasipo ushahidi haitoshi kumtia mtu hatiani.
 
Ushahidi wa tuhuma za za Mdude upo wapi? Au mtu ukijiamkia zako huko unaanza kuropoka ropoka Hovyo hovyo na kutuhumu watu bila ushahidi? Ndio democrasia hiyo? Ndio uhuru huo?
 
Jinsi damu itakavyozidi kumwagika hapa nchini mjue hata ninyi ha mtakuwa salama!
Hamkumbuki Nani alım piga risasi Karume na kwasababu gani? Samia ajue damu Hii inayomwagika haiendi bure itakuja kumlilia .
 
Acheni ujinga wa kuropoka ropoka vitu Ndivyo na ushahidi navyo .kwa lengo la kutafuta umaarufu na sifa tu za kijinga jinga tu
 
Ushahidi wa tuhuma za za Mdude upo wapi? Au mtu ukijiamkia zako huko unaanza kuropoka ropoka Hovyo hovyo na kutuhumu watu bila ushahidi? Ndio democrasia hiyo? Ndio uhuru huo?
Hoja kuu ilikuwa ni "Ni Kwanini Mdude Nyagali hakamatwi na Kuchukuliwi Hatua Kali Kwa Kuendelea Kumchafua Rais Samia Bila Ushahidi?"​

Naomba unisaidie kujibu hizi hoja mbili tu:
1. Mdude kuhoji kuhusu utendaji wa kazi wa Samia ni kosa!? Na kama ni kosa je kwaninj liwe kosa? Mdude amepata kuhoji udhaifu wa jeshi la polisi huku akionesha wazi namna ambayo maafisa polisi wakitumia chombo hicho kama familia zao ilihali wanalipwa na kodi zako! Je Mdude amekosea kuhoji jambo hili?!

2. Umezungumzia kuhusu uhuru na demokrasia, safi sana Mkuu, lakini unadhani Samia anatimiza kiapo chake cha kuheshimu na kulinda Katiba, katiba ambayo inatoa ruhusa ya kipekee ya kila raia kulindwa yeye na mali zake? Au Mdude amekosea kuzungumza jambo hilo!??​
 
Mbona umejibu na kuandika nje kabisa na hoja yangu? Nimeuliza kwanini Mdude hakamatwi kwa uzushi na kutoa tuhuma za uongo na uchonganishi pasipo ushahidi? Umeona tuhuma alizozitoa ? Au umekuja tu kutoa maoni yako bila kujuwa kinachoendelea?
 
Uzushi upi au tuhuma zipi za uongo ambazo Mdude amezitoa! Tuanzie hapo Mkuu!
 
Kumtaja tu mtu pasipo ushahidi haitoshi kumtia mtu hatiani.
Ushahidi unatolewa mahakamani.
Mtu yeyote anaweza kutuhumiwa na ana haki ya kujitetea dhidi ya tuhuma zake.

Wewe na wenzako humu si mlianzisha tuhuma dhidi ya Boni Yai, Mnyika na Mbowe kuhusiana na kifo cha mzee Kibao? Je ukiombwa ukatoe ushahidi mahakamani upo tayari kuthibitisha uhusika wao?
 
Nenda KAMKAMATE!!
 
Kawaulize MAKABURU na NDULI kilichowapata.......vivaa na MOZAMBIKIESINS
 
Umepiga kwenye mshono
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…