Ni Kwanini Mdude Nyagali hakamatwi na hachukuliwi Hatua Kali Kwa Kuendelea Kumchafua Rais Samia Bila Ushahidi?

Yule jamaa naona kichwa chake hakipo sawa.
Swali fikirishi aliye mharibu akili ni nani?, Kwa wale ambao hawajui akili ya binadamu inavyofanya kazi nikwamba akili ya binadamu huihifadhi kumbukumbu ya kila kitu tunacho kiona, kusikia na kufunza, (life learning skills) na kufundishwa, binadamu ukikutana na jambo fulani ama changamoto ubongo hutafsiri kumbukumbu ulizo zihifadhi kukabiliana na changamoto uliyona nayo na kama huna ulicho hifadhi huwezi kukabiliana na changamoto.

Binadamu ndiye mara nyingi husababisha changamoto kwa wengine kwa makusudi ama bila kujua, hata yeye hujisabanishia Changamoto kwa uzembe uvivu ujinga na ushamba, uwezo wa binadamu kutafsiri kumbukumbu alizo zihifadhi kwa haraka na kupata suluhisho hutambuliwa kama mwenye akili sana
 
Ndugu zangu Watanzania,

Ikiwa tutaacha Taifa likajenga utamaduni wa watu wakatumia mitandao ya kijamii kuchafua viongozi wetu,kuwapaka matope, kuwadhalilisha, kuwatukana matusi bila kuchukuliwa hatua wala kukamatwa ili watoe ushahidi tutakuwa tunariharibu Taifa letu.tutakuwa tunaharibu maadili na utamaduni mzima wa kuheshimiana na kukosoana kwa staha.

Imeshakuwa kero sana kwetu wananchi kuona mara nyingi sana Mdude Nyagali akitumia mitandao ya kijamii kumtolea RAIS wetu lugha za matusi, kumdhalilisha ,pamoja na kumhusisha ,kumzushia tuhuma za uongo, uchonganishi na zenye lengo la kumchafua pasipo ushahidi wa aina yoyote ile.

Amekuwa akifanya hivyo mara nyingi sana.na kitendo cha kukaliwa kimya pasipo kuchukuliwa hatua za kukamatwa,kuhojiwa,kufikishwa mahakamani kumemfanya ajione yupo juu ya sheria,kujiona anaogopwa ,kujiona yeye anaweza kufanya lolote,kusema chochote, kumtukana yeyote, kumdhalilisha yeyote,kumvunjia heshima yeyote,kumzushia yeyote pasipo kuchukuliwa hatua wala kukamatwa wala kuhojiwa wala kukemewa.

Imefanya watu wabaki wanashangaa inakuwaje mtu huyu anayefanya kazi ya kumchafua Mheshimiwa Rais kila siku anaachwa bila kuchukuliwa hatua? Watu wanashangaa kwanini anafumbiwa macho muda wote? Wahusika mnasubiri mtu huyu aropoke au aseme nini au amchafue vipi na kwa kiasi gani Rais wetu ndipo mumchukulie Hatua? Je sheria zinatumika kwa baadhi ya watu na kufungwa pingu kwa wengine kutokutumika?

Kwanini hamumkamati na kumhoji ili atoe ushahidi wa tuhuma anazozitoa? Yeye ni nani katika Taifa hili? Hii haikubaliki wala kuvumilika kuona akimchafua Rais wetu Pasipo kuchukuliwa hatua kali za kisheria. ni lazima tufahamu ya kuwa hakuna uhuru usio na mipaka,hakuna uhuru au demokrasia kwa ajili ya kutukana , kudhalilisha,kuwashushia heshima wengine pamoja na kuwapaka matope wengine. Uhuru una kwenda sambamba na wajibu wa kuzingatia haki za watu wengine .

Soma Pia: Mdude Chadema: Hotuba ya Rais Samia jana ni hotuba mbovu zaidi kuwahi kutokea Tanzania

Huwezi ukawa unachafua watu wengine halafu ukasema ni demokrasia au uhuru.uhuru na demokrasia ina mipaka yake. Nawakumbusheni ya kuwa Mbali ya kuwa RAIS Samia ni Mama mwenye watoto, wajukuu lakini kubwa ni kuwa Ni Rais wetu ,ni kiongozi wetu tunaye muangalia na anayegusa Maisha yetu moja kwa moja. Kwa hiyo hatufurahishwi wala kupendezwa kuona Rais wetu akichafuliwa na mtu au kuzushiwa mambo yasiyo na ushahidi wa aina yoyote ile.hii haikubaliki hata kidogo.

Ni lazima tabia hii mbaya na chafu inayofanywa na watu aina ya Mdude Nyagali waliokosa adabu na staha tuipinge,kuikemea ,kuishambulia na kuikataa kabisa hapa Nchini.ni lazima tuseme tunataka uhuru na demokrasia lakini siyo uhuru wa kuwatusi na kuwachafua wengine bila ushahidi wa aina yoyote ile.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Nashangaa hivyo vi kesi vidogo vidogo wanavyopewa, sijui DPP na na DCI wanakwama wapi,, kama ya Boniphace Jackob, hiyo nayo ni kesi kweli
 
Kwamba Mungu amekosa kazi?
Hakika ni Mungu tu anamlinda Mdude ndio maana yuko huru kueleza kwa uwazi hayo unayoyalalamikia. Miongoni mwa watu wengi wanaotukana kimoyomoyo, jasiri Mdude Nyagali yuko free ku express kilichopo moyoni mwake. Mungu wake anamlinda na hatakuja kupatwa na hayo unayoyataka.
 
umekurupuka kama mlevi

Unaweza kutukana lakini ujumbe wa Mdude Nyagali ulikuwa on point, na umefika Ikulu, umefika Mambo ya Ndani, umefika TISS, umefika most importantly, kwa wananchi.

Nyagali kasema Party Secretary Nchimbi was more presidential and statesmanlike in his remarks because he tried to unite a nation in turmoil and trepidation.

Samia akaja akapindua yote yaliyosemwa na Nchimbi, akachafua hali ya hewa aliyojaribu kuirekebisha Nchimbi.

Na Nchimbi alisema kada yeyote wa chama anaeongea "mambo ya kijinga" yeye toka aingie amekua "akiruka nae." Sasa tulitegema akija kuongea Mwenyekiti wa chama basi akazie pale Nchimbi alipoachia, sio kuliambia taifa wanaomlilia na kulaani kifo cha Kibao "ni makhulukutabu...kufa kupo... serikali yangu si ya samaki ....sing'oki kirahisi... kufa kwaja ... mabalozi wameongea ya kwao sio ya nchi zao... watoto wa polisi wapewe ajira polisi, huyu si wa kwanza kufa, kifo ni kifo."

Kama kifo ni kifo kwa nini juzi ulitoa statement ya Twitter ya kukemea mauaji ya Kibao ???

Soma spichi unazoandikiwa Mama Samia.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Ikiwa tutaacha Taifa likajenga utamaduni wa watu wakatumia mitandao ya kijamii kuchafua viongozi wetu,kuwapaka matope, kuwadhalilisha, kuwatukana matusi bila kuchukuliwa hatua wala kukamatwa ili watoe ushahidi tutakuwa tunariharibu Taifa letu.tutakuwa tunaharibu maadili na utamaduni mzima wa kuheshimiana na kukosoana kwa staha.

Imeshakuwa kero sana kwetu wananchi kuona mara nyingi sana Mdude Nyagali akitumia mitandao ya kijamii kumtolea RAIS wetu lugha za matusi, kumdhalilisha ,pamoja na kumhusisha ,kumzushia tuhuma za uongo, uchonganishi na zenye lengo la kumchafua pasipo ushahidi wa aina yoyote ile.

Amekuwa akifanya hivyo mara nyingi sana.na kitendo cha kukaliwa kimya pasipo kuchukuliwa hatua za kukamatwa,kuhojiwa,kufikishwa mahakamani kumemfanya ajione yupo juu ya sheria,kujiona anaogopwa ,kujiona yeye anaweza kufanya lolote,kusema chochote, kumtukana yeyote, kumdhalilisha yeyote,kumvunjia heshima yeyote,kumzushia yeyote pasipo kuchukuliwa hatua wala kukamatwa wala kuhojiwa wala kukemewa.

Imefanya watu wabaki wanashangaa inakuwaje mtu huyu anayefanya kazi ya kumchafua Mheshimiwa Rais kila siku anaachwa bila kuchukuliwa hatua? Watu wanashangaa kwanini anafumbiwa macho muda wote? Wahusika mnasubiri mtu huyu aropoke au aseme nini au amchafue vipi na kwa kiasi gani Rais wetu ndipo mumchukulie Hatua? Je sheria zinatumika kwa baadhi ya watu na kufungwa pingu kwa wengine kutokutumika?

Kwanini hamumkamati na kumhoji ili atoe ushahidi wa tuhuma anazozitoa? Yeye ni nani katika Taifa hili? Hii haikubaliki wala kuvumilika kuona akimchafua Rais wetu Pasipo kuchukuliwa hatua kali za kisheria. ni lazima tufahamu ya kuwa hakuna uhuru usio na mipaka,hakuna uhuru au demokrasia kwa ajili ya kutukana , kudhalilisha,kuwashushia heshima wengine pamoja na kuwapaka matope wengine. Uhuru una kwenda sambamba na wajibu wa kuzingatia haki za watu wengine .

Soma Pia: Mdude Chadema: Hotuba ya Rais Samia jana ni hotuba mbovu zaidi kuwahi kutokea Tanzania

Huwezi ukawa unachafua watu wengine halafu ukasema ni demokrasia au uhuru.uhuru na demokrasia ina mipaka yake. Nawakumbusheni ya kuwa Mbali ya kuwa RAIS Samia ni Mama mwenye watoto, wajukuu lakini kubwa ni kuwa Ni Rais wetu ,ni kiongozi wetu tunaye muangalia na anayegusa Maisha yetu moja kwa moja. Kwa hiyo hatufurahishwi wala kupendezwa kuona Rais wetu akichafuliwa na mtu au kuzushiwa mambo yasiyo na ushahidi wa aina yoyote ile.hii haikubaliki hata kidogo.

Ni lazima tabia hii mbaya na chafu inayofanywa na watu aina ya Mdude Nyagali waliokosa adabu na staha tuipinge,kuikemea ,kuishambulia na kuikataa kabisa hapa Nchini.ni lazima tuseme tunataka uhuru na demokrasia lakini siyo uhuru wa kuwatusi na kuwachafua wengine bila ushahidi wa aina yoyote ile.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

Yah right ..... Hawamkamati kwa vile wanajua anasema UKWELI ....!!
 
Mkamateni Mange Kimambi ata me simuelewi ila sumu ya nyigu kaa mbali

Ni mwanaharakati sio mchumia tumbo kama wengi wenu kazi moja tu kusifia ujinga
 
Back
Top Bottom