Ni kwanini Nyoka yoyote mwenye Sumu Kali akikutana na Mtoto Mchanga au Mdogo hawezi kumdhuru na atakuwa anacheza naye tu?

Ni kwanini Nyoka yoyote mwenye Sumu Kali akikutana na Mtoto Mchanga au Mdogo hawezi kumdhuru na atakuwa anacheza naye tu?

Mkuu sio nyoka tu hata wakati mwingine wanyama wakali ni mara chache kumdhuru mtoto,
Sababu zipo nyingi wengine wanasema mtoto ni malaika,
Wanasema mnyama yoyote mara nyingi anakushambulia kwa kujilinda hasa nyoka ambao hawawezi kukufanya kitoweo, yani nyoka wadogo wadogo hawa wakiuona huwa wanajilinda kwa kukuuma kwa hiyo mtoto huwa mara nyingi anakuwa hana madhara kwa nyoka ndio maana hang'atwi.
 
Kwa sisi ambao tumeishi maisha ya mchanganyiko tunajua ilo linatokea nimewai kuona kwa macho yangu.
Aaa wapi. Stori tu hizo au labda nyoka wa kwenye maonyesho na siyo hawa koboko na chatu wa huku Tabora. Mama akijichanganya akamuweka mtoto chini eti alime si ajabu akija kushtuka mtoto keshamezwa...
 
Hakuna ukweli kwenye hili. Mlete mwanao hapa Zoo kuna chatu mwenye njaa kali tuone kama watacheza.
Mkuu huyo anakufanya kitoweo 😂😂😂hana masikhara llakini nyoka ambae hawezi kufanya kitoweo wale wadogo wanweza wasimdhuru.
 
Aaa wapi. Stori tu hizo au labda nyoka wa kwenye maonyesho na siyo hawa koboko na chatu wa huku Tabora. Mama akijichanganya akamuweka mtoto chini eti alime si ajabu akija kushtuka mtoto keshamezwa...
Coment ya kwanza nimeweka bayana kwamba nyoka wakubwa hao wanakufanya kitoweo vizuri haijalishi umri lakini wale wadogo wanaeza kupita karibu na mtoto wakaenda zao..
Kuna nyoka sisi tunamuita Lipili ni mfupi mnene anabaka kama ya chatu na mtaratibu lakini anasumu kali akikuuma mguu lazima uwe kilema kama hutopata matibabu kwa haraka wanapenda kujificha chini ya majani kutafuta joto,
Kuna siku mtoto tulimuweka mahali shambani alilala mtoto nilivyomrudia pembeni yake tulimkuta huyo Lipili amijilaza karibu na mtoto akifaidi joto la mtoto mchanga nyama to nyama,
Wee taharuki yake sasa kila alivurugwa kwa jinsi nyoka alivyo na sumu kali.
 
Hizo huwa ni hadithi mkuu, nyoka ni kiumbe chenye laana, hakijawahi kuwa na urafiki na binadamu hata siku moja
Sio hadithi bali ni ukweli kabisa na ni suala la kisayansi zaidi, tafuta humu kuna uzi unazungumzia hilo suala ki undani zaidi, na utaelewa, na sio mtoto tu hata mtu mzima kama umelala hujamuona, anaweza kuja karibu hata kujizungusha kwenye mguu wako, na akaondoka, ila kama ukimuona sharti usishituke, kushituka kwako ndio utamfanya akung'ate.
 
Nyongeza anakung'ta kwa sababu anajilinda usimdhuru ni defence mecanism in biology.
 
Nyoka wanatofautishaj andunje na mtoto? Naomba jibu kwa sauti kuu🎚️🔈🔉🔊
WANATOFAUTISHA KWA SAUTI ANDUNJE SAUTI YAKE INAKOROMA MTOTO NI NYORORO, yani hapo nimejibu kwa sauti kubwa. 😂
 
Iko hivi viumbe wote wakali mfano: simba, chui, nyoka, mbwa n.k. humshambulia binadam pale anapoonekana anataka kuwadhuru. Hii huwa inatokea pale binadamu akiwaona naye kwa kuwa alishajua ni wanyama wakali basi hujenga hofu(fright) au ujasiri wa kupambana nao (fight). Hizo mechanism zote zinatokea pale adrenalin inapokuwa imezalishwa mwilini ( hii ni insulin inayompa mtu nguvu ya kupambana na hatari au nguvu ya kuikimbia hatari)

Hivyo bas baada ya hiyo insulin kuzalishwa mnyama yeyote mkali anaidetect moja kwa moja na hapo ndipo huamua kumshambulia binadamu ili asimdhuru.

Sasa kwa watoto kwakua hawana utambuzi wa vitu kuweza kujua kama hii ni hatar au lah bas wao huwa hawazalishi adrenalin hivyo kupelekea kutoshambuliwa ma viumbe hatar maana hawaonekani kama tishio kwa hivyo viumbe.
 
Nyoka hushambulia binadam kama anaona ni hatari, mnyama ambae hachukulii binadam kama chakula hawezi kumla mtoto maana si hatari kwake, ata nyoka anaweza kukupita umelala akasepa akaenda zake
Ila kwa wanyama kama simba au chui au chatu mwenye njaa anamla mtoto vizuri tu, hii ni kwasababu ya flow of energy,
Duniani wanyama wote huishi kwa law moja tu, either kitu ni adui, yani niuwe nikuue au kitu ni familia, yaan sio hatarishi
 
Back
Top Bottom