Ni kwanini Nyoka yoyote mwenye Sumu Kali akikutana na Mtoto Mchanga au Mdogo hawezi kumdhuru na atakuwa anacheza naye tu?

Ni kwanini Nyoka yoyote mwenye Sumu Kali akikutana na Mtoto Mchanga au Mdogo hawezi kumdhuru na atakuwa anacheza naye tu?

wanyama wanatumia system ya "destroy what destroys you" katika kujilinda! mtoto hawezi kumdhuru nyoka hivyo naye hawezi kudhuriwa na nyoka.
 
Aaa wapi. Stori tu hizo au labda nyoka wa kwenye maonyesho na siyo hawa koboko na chatu wa huku Tabora. Mama akijichanganya akamuweka mtoto chini eti alime si ajabu akija kushtuka mtoto keshamezwa...

Nakubaliana nawe katika hili kwa 100% kwani Miezi Michache limemtokea Mwana Mama Mmoja huko Mkoani Iringa na sasa hana Mtoto wake tena.
 
Iko hivi viumbe wote wakali mfano: simba, chui, nyoka, mbwa n.k. humshambulia binadam pale anapoonekana anataka kuwadhuru. Hii huwa inatokea pale binadamu akiwaona naye kwa kuwa alishajua ni wanyama wakali basi hujenga hofu(fright) au ujasiri wa kupambana nao (fight). Hizo mechanism zote zinatokea pale adrenalin inapokuwa imezalishwa mwilini ( hii ni insulin inayompa mtu nguvu ya kupambana na hatari au nguvu ya kuikimbia hatari)

Hivyo bas baada ya hiyo insulin kuzalishwa mnyama yeyote mkali anaidetect moja kwa moja na hapo ndipo huamua kumshambulia binadamu ili asimdhuru.

Sasa kwa watoto kwakua hawana utambuzi wa vitu kuweza kujua kama hii ni hatar au lah bas wao huwa hawazalishi adrenalin hivyo kupelekea kutoshambuliwa ma viumbe hatar maana hawaonekani kama tishio kwa hivyo viumbe.

Ndugu kwa hiki ulichojibu hapa kama ungekuwa ni Mwanafunzi na umejibu hivi katika Mtihani basi nisingekupa tu 100% bali ningekupa 200% zote.
 
Nachangia kwa kusema. Joto la mwili ndilo huamua. Kwani mtoto mdogo nyoka akimusogelea hata kujizungusha kwake mtoto Joto lake hubaki lile lile na mapigo ya moyo huwa hayabadiliki so nyoka Huwa hana hisia nzonzote na kuona Hakuna Hatari. Na kuto mzuru Mtoto
 
Mimi naonaga kama hayo uliyo yasema ni masimulizi tu ..

Hayana uhalisia wowote ule katika maisha tunayoishi
 
Mimi naonaga kama hayo uliyo yasema ni masimulizi tu ..

Hayana uhalisia wowote ule katika maisha tunayoishi
Sio simulizi ni kweli kabisa mimi nimeshashuhudia kwa macho yangu mawili.
 
Kuna kemikali inaitwa catecholamine hii inaachiliwa pale unapokutana na hatari au dharura, hii ndio inaweza kumtambulisha mnyama kwamba huyu ni adui. Kwa wale wanaopakwa dawa ili waweza kucheza na hao wanyama unakuta hizo dawa zinaondoa harufu ya hiyo hormone. Kwa mtoto mchanga hajawa na uwezo wa kutambua hatari bado hivyo hiyo hormone haiwi released. Lakini akitokea mtu aka irelease nyuka anajua yuko hatarini hivyo anatambua hawa ni maadui.
 
Hayo majaribio yako bora usijeyafanya kwa vitendo ishia kuwaza hivyohivyo tu kichwani la sivyo utamdhuru mwanao kwa kujitakia.
 
Huo ni upuuzi tu na kudanganyana nyoka is not that intelligent nyoka anakung'ata pale anapoona inafaa kufanya hivyo.Hata wale nyoka wasio na sumu ambao hukamata mawindo kwa kukaba na wenyewe wanang'ata
 
Back
Top Bottom