Biashara ya mafuta na gas iko kwenye mikono ya mabeberu na mabepari Ulaya na America huko, Sera zao ndio huamua upatikanaji au kutopatikana kwa ajira dunia ya tatu huku.
Makampuni ya mabeberu ndio mhimili wa hii biashara na ndio watengenezaji wa ajira na walipaji wa mishahara mikubwa.
Kabla ya awamu ya tano, makampuni mengi ya mabeberu yalimiminika Tanzania na kuanza kuchangamkia biashara ya vitalu pamoja na kutengeneza ajira nyingi na kulipa mishahara minono, Awamu ya Tano ya JPM ilikuja na sera iliyowaogopesha mabeberu na kuamua kufunga biashara wengi wao na kuondoka, hapa ajira za oil and gas zikafa.
USHAURI: Oil and gas inaajira nyingi sana uarabuni, Saudia, Oman, UAE, Kuwait, Qatar nk, kinachotakiwa ni vijana wetu kuzamia huko na kuzisaka fursa kwa kukubali kutaabika kwa muda ili watengeneze future kubwa binafsi, kuendelea kuwategemea wanasiasa watanzania walioshiba kuamua future yako ni kupoteza muda tu.