Ni kwanini serikali imeshindwa kuwaajiri wahitimu wa fani za mafuta na gesi pamoja na uchache wao?

Ni kwanini serikali imeshindwa kuwaajiri wahitimu wa fani za mafuta na gesi pamoja na uchache wao?

Ni Mara 1000 Nchi nzima iwe na mafundi kutakuwa na tija katika Taifa,ni lazima Nchi itengeneze ajira katika uzalishaji kuliko huduma.MTU akisoma VETA akiwa na ujuzi Fulani ataweka ujuzi wake katika uzalishaji wa moja kwa moja kuliko huyo wa fani ya sheria.
Heeeee za kuambiwa changanya na zako.
 
Fani za mafuta na gesi zilianza kufundishwa Tanzania mwaka 2013.

Mara serikali ikaanzisha shahada ya kwanza ya kemia ya petroli (BSc. Petroleum Chemistry) (wanafunzi 25), Shahada ya kwanza ya uhandisi wa petroli (BSc. Petroleum Engineering) (Wanafunzi 25) na Shahada ya kwanza ya jiolojia ya petroli (BSc. Petroleum Geology) (wanafunzi 15).

Mwaka 2017, wanafunzi wa kwanza wanahitimu. Lakini serikali inashindwa kuwaajiri pamoja na uchache wao.

Ajira zinatoka TPDC na PURA. Zinaajiri wahitimu wasiozidi sita kwa mwaka. Sasa najiuliza maswali ni jambo gani linazuia kuwaajiri wahitimu wote waliosomea fani hizo.

Ulikua ni mpango wa serikali wa kuandaa wataalamu wa fani hizo katika taifa letu. Tuweke ubinafsi pembeni tuwaajiri wahitimu wote mimi sidhani kama inashindikana. Sio halali mwanafunzi anapata division one ya 5 form six combination ya PCM, na chuo kikuu GPA ya 4.4 taifa linashindwa kumtumia anaamua kuwa auditor kwenye mambo ya uhasibu. Na kwa inavyoonekana ni wengi wala sio mmoja. Tunapaswa kuweka mikakati kama kuna sehemu tumefail tusisite kurudi nyuma na kuanza upya.

Lakini pamoja na kuajiriwa swala la kujiajiri kwa wahitimu wa fani yoyote ni la lazima na hicho ndio kipimo pekee cha kujua kama muhitimu alielewa darasani.

Huu ndio ukweli mhitimu ambaye hawezi kujiajiri maana yake hakuelewa darasani pengine alikua anakalili maarifa bila kuelewa.

Lakini kujiajiri kwa muhitimu kusiwe kisingizio chakutotengeneza ajira katika taifa letu. Bado sisi kama watanzania tunakazi ya kuhakikisha tunatengeneza ajira. Hicho ni kipimo cha ukuaji wa sekta yoyote. Sekta isiyoweza kutengeneza ajira maana yake imesimama kukua.

Hitimisho langu: Sekta ya mafuta na gesi imeshindwa kutimiza malengo iliyojiwekea. Imeshindwa kutengeneza ajira hasa za wahitimu wa gesi na mafuta. Waliokalia viti kwenye sekta ya mafuta na gesi bado hawajafanya kazi vya kutosha. Wanapaswa kuangalia walipoyumba na kufanya marekebisho.

Mwaka 2012 hadi 2013 makampuni ya mafuta na gesi yalijaa Tanzania na yalikua yanajaa vyuoni kuajiri wanafunzi hata kabla hawajamalza vyuo.
Kuna haja ya kubadili uongozi kwenye sekta ya mafuta na gesi ili kurudisha kasi ya kipindi cha nyuma.

Hizi ni baadhi ya hoja ambazo bunge letu lilipaswa kuzizungumzia bungeni na kuwahoji wakuu wa taasisi zinazohusika na mnyororo mzima wa sekta hii. Bunge halipaswi kukaa kimya na kukubali matokeo kasi ya sekta inapokua inashuka.
Mtu anaacha civil kwa kupenda misifa anakimbilia Petroleum na gas😅😅😅
 
Waajiliwe wapi sasa?serikali haichimbi mafuta wala gesi,tipper imejaa watunga sera tu,hakuna exproration yeyote inayofanywa,
Makampuni yanayochimba gesi na mafuta,ni ya nje,yanakuja na wataalamu wao,sasa hawawezi kuchukua Hawa ambao hawana hata uzoefu,kwa kijana wa bongo,nyakati hizi anza kutafuta kazi nje ya mipaka,enzi hizo naanza kazi,nilikuta kaka zangu wapo vodacom,Tena wazee,lakini mpaka leo wapo voda huko,wanazidi kupanda vyeo,sasa wewe kijana utapata nafasi wapi,
Nilikuwa SA,Kwenye makampuni ya Scania,Emerson,caterpillar nilikuta wakenya,Nigeria,na wacongo kibao,
Mkenya haoni shida kuzamia SA akaoa mwenyeji Ili apate uhuru wa Kupiga Mishe Mishe zake,mbongo mgogo ukimuambia aende akaishi na kuoa Mtwara,au kagera anaona tabu
Mbongo anapenda asili kumtoa kwao afate fursa ni kazi kweli kweli
 
Back
Top Bottom