Ni kwanini serikali imeshindwa kuwaajiri wahitimu wa fani za mafuta na gesi pamoja na uchache wao?

Serikali haikutakiwa kuwa muajiri mkuu kwa hao vijana, service companies, drilling contractors na operators hilo ndio jukumu lao. Serikali waharakishe kusaini mkataba wa LNG, ili operators waendelee na uchimbaji wa gesi Mtwara.
 
Nyerere pamoja na akili zake zote alishindwa kuacha Katiba nzuri.

Cha kushangaza akasema kwa Katiba hii akioatikana kiongozi kichwa ngumu anaweza kuwa dikteta, sasa kwanini aliamua tuwe na Katiba ya namna hii?
 
Kuna jamaa mmoja pia kapiga hiyo course pale UDSM, lakini mpaka leo kaishia kuwa mwalimu wa tuition pale Mwanza.


Jamaa ni mjuzi sana ila ndohivyo, bongo nyosso.
Dah! Na kuna siku atakamatwa na Mratibu Elimu Kata na kumuhoji kama anayo taaluma ya Ualimu.

Walimu huwa wanaringia taaluma yao sema wahuni town wanapeta na Tuit kama pale Mchikichini, mapambano, Buguruni n.k watu wanakula Namba kama mizimu vile!
 
Kuna kozi bongo sio za kusoma.

Unasoma kozi za mafuta kwani Tanzania ina mafuta ama inachimba mafuta? Hizo fani ni dili sana huko uarabuni ila bongo ni kupoteza muda wako.

Unasoma unakuja kusubiri uajiriwe na serikali.

Ilikua kidogo niuvae ama niingie cha kike kusoma kozi za kisiasa.

Shemeji yangu aliuvaa mkenge wa kisiasa akasoma kozi inaitwa law enforcement pale UD, hadi sasa anauza juice ya miwa mtaani maana sio mwanasheria sio nani.

Kozi kama hizo za kisiasa na procurement sio za kusoma tena sasa ulimwengu huu.

Tuhamie kwenye IT, Finance(sio accounting) Investment, Projects, Electronics, Electrical, Civil engineering, Architect, Law, Computer nk.

Mimi kwa sasa simshauri mtu kusoma kozi nje ya hizo.
 
Mkuu hii mada umekua ukiianzisha kila mara, haipiti miezi 6 hujarudia hii mada naamini wewe ni mhanga mmoja wao ambae umepotezewa muda na wanasiasa. Pole sana.
 
Mkuu hii mada umekua ukiianzisha kila mara, haipiti miezi 6 hujarudia hii mada naamini wewe ni mhanga mmoja wao ambae umepotezewa muda na wanasiasa. Pole sana.
Hapana boss ni mwanasiasa chipukizi nikijianda kupeperusha bendera 2025; hili ni moja la tatizo nililolichagua kulitatua katika taifa letu either kwa uwezo wangu mwenyewe au kwa uwezo wa uongozi kama nitafanikiwa kuchaguliwa kuingia kwenye majengo ya hapa Dodoma.
 
Ina maana Einstein alijiajiri kwanza?
Kujiajiri ni kipaji na pia inatokana na mipango na malezi ya wazazi.
Don't expect mtu ambaye hajui maana ya biashara ila Yuko vizuri sana kwenye engineering akajiajiri, kwanza vifaa tu ni bei kubwa sana, alaf pili, nchi yetu haina teknolojia inayoruhusu baadhi ya kozi kujiajiri.
That's the reality.
Kushindwa kujiajiri is not a measure of intelligence.
 
Biashara ya mafuta na gas iko kwenye mikono ya mabeberu na mabepari Ulaya na America huko, Sera zao ndio huamua upatikanaji au kutopatikana kwa ajira dunia ya tatu huku.

Makampuni ya mabeberu ndio mhimili wa hii biashara na ndio watengenezaji wa ajira na walipaji wa mishahara mikubwa.

Kabla ya awamu ya tano, makampuni mengi ya mabeberu yalimiminika Tanzania na kuanza kuchangamkia biashara ya vitalu pamoja na kutengeneza ajira nyingi na kulipa mishahara minono, Awamu ya Tano ya JPM ilikuja na sera iliyowaogopesha mabeberu na kuamua kufunga biashara wengi wao na kuondoka, hapa ajira za oil and gas zikafa.

USHAURI: Oil and gas inaajira nyingi sana uarabuni, Saudia, Oman, UAE, Kuwait, Qatar nk, kinachotakiwa ni vijana wetu kuzamia huko na kuzisaka fursa kwa kukubali kutaabika kwa muda ili watengeneze future kubwa binafsi, kuendelea kuwategemea wanasiasa watanzania walioshiba kuamua future yako ni kupoteza muda tu.
 
Mbona mnaruka sehemu muhimu ya mada. Nikuulize ukipata nafasi ya kushika usukani kwenye sekta ya mafuta na gesi utayajibu maswali kwa mtindo huo?
 
Narudia Tena, njaa itakuua
 
Nakumbuka miaka hiyo wanasiasa waliwaambia mabaharia wa kitanzania watapata ajira kwenye uchimbaji mafuta huku wakijua hakuna kozi za Offshore Practical Training nchini. Katibu mkuu ilibidi awaambie ukweli kama hujasoma kozi hizo huwezi kupata kazi, na vyuo vilikuwa South Africa
 

kuna kipindi wanasiasa na hata watalaam wa kitanzania huwa tunapotoshana sana.

unakuta mtu ni AB ana cheti cha STCW95 pale DMI anadanganywa atapata kazi kwenye Drill ship, jackup rig au hata hizi za exporation na kwenye operation za ROV..
Kazi nyingi kwenye Oil and gas ni proffessional's zinazohitaji proffesionals personnel wenye either experience na oil and gas operations au wenye uzoefu na kazi zenye kufanana na hizo kama watu waliofanya kazi kwenye mining field, au uchukue fresh graduates wa oil and gas, mining engineering, geologists, mechanical engineers, electrical engineers, electromechanical engineers, nk then uwatrain wafit kwenye kitu unachotaka.

Hata meli za kisasa zinataka mtu proffessional kwanza then uingie uchaguliwe kwenye area ambayo wewe unautalaam nalo, sio kama zamani unaweza kuokota mtu yeyote ukamfanya kuwa "Oiler" AB nk... dunia yasasa inataka watu proffesional zaidi kwenye marine industry na sio waogeleaji..

Hizi field kwasasa zimejaza sana Cheap labor kutoka ufilipino, India na Indonesia ambako wako wengi na ni very cheap, wachapakazi, waaminifu na wanajua kiingereza tofauti na manpower kutoka Africa ambayo inachangamoto kidogo.
 
Unazungumzia kozi za offshore kama zipi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…