Ni kwanini tunashindwa kufuata sheria za barabarani?

Kanyawela

Senior Member
Joined
Aug 22, 2015
Posts
183
Reaction score
203
Wakuu nimekuwa najiuliza tuna shida gani sisi watumia barabara hasa kwenye mataa (Trafic lights).

Mara nyingi nimeona taa zinaruhusu magari na wakati yanaanza kuondoka wanatokea watembea kwa miguu wanakatiza barabara ambayo ni hatari kwao.

Pia nimeona baadhi ya wenye magari kusimamisha magari kupisha watu wakati taa zimewaruhusu na hapo hapo zimewazuia waenda kwa miguu ili magari yapite.

Hoja yangu ni kwamba kuna uzembe tunafanya sisi waenda kwa miguu na waendesha magari.

Tunahitaji umakini kwa kuheshimu alama na taa za barabarani kuepusha ajali.
 
Hasa boda boda hua najiuliza wao sheria za barabara haziwahusu!Kwenye taa wanapita nduki tu ukija kwenye zebra hata km gari zimesimama ili watu wavuke boda boda wao watapita nduki tu na ndo ajali nyingi zinasababishwa na hawa.Mm naomba serikali itoe mwangalizo kwa boda yeyote atakae pita wakati taa haijaruhusu ama kutosimama kwenye zebra wakati watu wanapita akikamatwa piki piki yake ikikamatwa ni kupiga mnada.
 
Sheria za barabarani zilipaswa zitoe adhabu (faini) kwa waendesha vyombo pamoja na eatembea kwa miguu.
Na rushwa ingekua haichukuliwi na hawa ndugu zetu, nadhani watu wangeheshimu na kutii sheria na ajali zingepungua kwa walau 750%
 
Sheria ya 50/kmp imekaa kisiasa sana. Yaani kuna maeneo mengine hakuna sababu ya hicho kibao! Lakini dereva unatakiwa kutii sheria bila shuruti!

Potelea mbali, wacha tuendelee tu kuwapa rushwa hawa mchwa wenye njaa kali.
 
emergency, mazoea,ulimbukeni, na mwisho n kwamba watu wamechanganyikiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…