Amani Msumari
JF-Expert Member
- Aug 21, 2016
- 1,830
- 972
Awali ya yote, napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza ndugu Bernard Camilius Membe na ndugu wakili msomi Tundu Antipas Lissu kwa kuaminiwa na kuteuliwa kupeperusha bendera za vyama vyao katika kinyang'anyiro cha urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, 2020. Ni rasmi sasa watachuana na Rais Magufuli.
Uchaguzi ni uchaguzi na hakuna uchaguzi rahisi. Hatahivyo, Rais Magufuli na CCM kwa ujumla watashinda kwa kishindo. Twende pamoja:
1. Rais Magufuli na chama chake, CCM wana ajenda mahususi za uchaguzi mkuu. CCM chini ya Magufuli wanataka kukamilisha kazi kubwa waliyoianza. Hapa hapatakuwa na matumizi ya nguvu bali nguvu ya hoja. CCM wataonesha walichokifanya ndani ya miaka 5 na watawaomba watanzania waendelee kuwaamini kwa miaka 5 ijayo. Kwavile kazi imefanyika kweli na watanzania wameona, basi hakutakuwa na tabu. Upande wa pili, wapinzani hawana hoja wanayoisimamia kwa Sasa.
Naomba niwakumbushe kuwa katika nchi zinazoendelea Kama Tanzania, ajenda kubwa huwa ni maendeleo, na CCM chini ya Magufuli wamefanikiwa kwenye ajenda hii. Wapinzani wataleta ajenda ipi? Huko kupinga kila kitu? Watanzania wameamka.
2. Uimara wa vyama. CCM ni chama imara chenye mizizi mpaka ngazi ya shina. Vyama vingine vipo mijini tuu. Pamoja na rekodi yake nzuri, mgombea wa CCM ambaye ni ndugu Magufuli atabebwa na ukubwa wa chama chake, mapenzi ya wananchi walio wengi kwa CCM na ile hali ya ukweli kuwa imekita mizizi mpaka ngazi za chini.
3. Kushindwa kwa wapinzani kuungana. Kwanza niweke wazi, hata wapinzani wakiungana, bado kura zao hazitaweza kufikia kura za Rais Magufuli lakini angalau wangepata kura kadhaa. Kitendo cha kutoungana kinaonesha hawaaminiani hivyo watachafuana wenyewe kwa wenyewe na watadhoofishana kabla ya kufikia sanduku la kura. Inashangaza eti inakuwa jambo kubwa kwa mpinzani kuhamia upinzani. Yaani huu ndio ule mchezo wa sifuri kugeuza O. Wajifunze kwa mataifa yaliyoendelea. Wanahitaji wawe na chama kimoja cha upinzani chenye nguvu. Ni dhahiri ujio wa Membe utapunguza kura za CHADEMA
4. Wananchi wengi kupoteza imani yao kwa vyama vya Upinzani. Pamoja na ukweli kuwa kuunga mkono jitihada za mh Rais ni jambo jema lakini wananchi waliowachagua madiwani na wabunge wa upinzani na kuwaacha CCM walihuzunika sana kuona viongozi hao wakitimkia CCM. Sasa wengi wao wanaona bora tuu nao waunge juhudi kwa kura zao na wale wachache wanaobaki wanasema hatupigii tena upinzani kwani hawaaminiki na hatuipigii CCM vilevile. Hawa ni rahisi kuwashawishi wakaipigia CCM na ikitokea hawakupiga basi wapinzani ndio wanaopata hasara kwani wapiga kura wa CCM hawajabadilika zaidi sana wameongezeka
5. Watu wengi wanaounga mkono upinzani walisusa kujiandikisha/kuhakiki taarifa zao katika daftari la kudumu la wapiga kura. Hawa hawataweza kuwachagua viongozi wao. CCM ilifanya vizuri kwa kuhakikisha wananchama wake wamejiandikisha.
#tukutaneoktoba
Amani