Uchaguzi 2020 Ni kwanini upinzani utashindwa vibaya na CCM Itashinda kwa kishindo?

Uchaguzi 2020 Ni kwanini upinzani utashindwa vibaya na CCM Itashinda kwa kishindo?

CCM itashinda kwa asilimia zaidi ya 90. Hili halina ubishi.

LAKINI watachaguliwa (watapigiwa kura) na watu wasiozidi asilimia 10

Sababu za Ushindi

1. NEC ya kwao
2. Polisi wa kwao
3. Wakurugenzi wa kwao
4. Watendaji wa kata wa kwao
5. Ushamba wa muheshimiwa
Cha kushangaza hayo yote yanajulikana lakini bado mmeingia kwenye ushindani wakati mnajua CCM wana sababu za ushindi kwanini msikomae hadi mkahakikisha hayo yanayowabeba CCM yanaondolewa, mnatafuta visababu vya kuja kilia lia hapa... sijui kwanini ukiwa Chadomo unakuwa kama zuzu unachojua ni domokaya.
 
Mimi mkazi wa mkoa wa shinyanga naomba nitajiwe mambo makubwa mawili aliyoifanyia shy ili kura yangu nisimpe tundu lissu

Swali zuri sana mimi pia wa Heru Juu Manyovu Kasulu mkoani Kigoma CCM Mpya wanieleze yale ma-bombadier, flyovers za baharini, kipande kifupi cha SGR Reli Dar -Moro kinachoendelea kujengwa, Stiegler's gorge yamenigusa vipi mimi mkaazi wa Manyovu? Sana sana wametuulia kilimo na masoko yake kwa kusahau sekta hii ya maharage, pamba, korosho, uvuvi wa dagaa na samaki.

Kura yangu nampa Tundu Antipas Lissu maana chama cha Demokrasia na Maendeleo ya Watu kinanivutia na kunipa matumaini kuliko sera za Maendeleo ya Vitu.
 
Swali zuri sana mimi pia wa Heru Juu Manyovu Kasulu mkoani Kigoma CCM Mpya wanieleze yale ma-bombadier, flyovers za baharini, kipande kifupi cha SGR Reli Dar -Moro kinachoendelea kujengwa, Stiegler's gorge yamenigusa vipi mimi mkaazi wa Manyovu?

Kura yangu nampa Tundu Antipas Lissu maana chama cha Demokrasia na Maendeleo ya Watu kinanivutia na kunipa matumaini kuliko sera za Maendeleo ya Vitu.
Hata majjrani wa mkoa wa simiyu, tabora na mwanza wameuliza swali hili hili tunaomba jamaa atupe majibu!
 
Nini bara barani hata kwenye runway kule airport waingie tu na ndege zitaruka
 
Halafu bado naendelea kujiuliza, naomba mwenye jibu ajitokeze. Ukiishadadia CHADEMA wee mzalendo Ila ukiisemea mema CCM we unajipendekeza. Hii Ni dhambi ya ubaguzi. Hatahivyo, hapa kwangu mtasema mpaka mtabloo mafigo, katu sitaacha kuyasema mema ya Rais, serikali yake. Mimi Sina nchi nyingine. Mimi ni mtanzania halisi
Una dalili zote kuwa wewe ni mshamba!
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
CCM itashinda kwa asilimia zaidi ya 90. Hili halina ubishi.

LAKINI watachaguliwa (watapigiwa kura) na watu wasiozidi asilimia 10

Sababu za Ushindi

1. NEC ya kwao
2. Polisi wa kwao
3. Wakurugenzi wa kwao
4. Watendaji wa kata wa kwao
5. Ushamba wa muheshimiwa
Umesahau kuwa upinzani wengi tulisusa kijiandiisha
 
Yote umeandika pumba tu
Sababu ni moja tu
Wataiba kura.
Awali ya yote, napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza ndugu Bernard Camilius Membe na ndugu wakili msomi Tundu Antipas Lissu kwa kuaminiwa na kuteuliwa kupeperusha bendera za vyama vyao katika kinyang'anyiro cha urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, 2020. Ni rasmi sasa watachuana na Rais Magufuli.

Uchaguzi ni uchaguzi na hakuna uchaguzi rahisi. Hatahivyo, Rais Magufuli na CCM kwa ujumla watashinda kwa kishindo. Twende pamoja:

1. Rais Magufuli na chama chake, CCM wana ajenda mahususi za uchaguzi mkuu. CCM chini ya Magufuli wanataka kukamilisha kazi kubwa waliyoianza. Hapa hapatakuwa na matumizi ya nguvu bali nguvu ya hoja. CCM wataonesha walichokifanya ndani ya miaka 5 na watawaomba watanzania waendelee kuwaamini kwa miaka 5 ijayo. Kwavile kazi imefanyika kweli na watanzania wameona, basi hakutakuwa na tabu. Upande wa pili, wapinzani hawana hoja wanayoisimamia kwa Sasa.

Naomba niwakumbushe kuwa katika nchi zinazoendelea Kama Tanzania, ajenda kubwa huwa ni maendeleo na CCM chini ya Magufuli wamefanikiwa kwenye ajenda hii. Wapinzani wataleta ajenda ipi? Huko kupinga kila kitu? Watanzania wameamka.

2. Uimara wa vyama. CCM ni chama imara chenye mizizi mpaka ngazi ya shina. Vyama vingine vipo mijini tuu. Pamoja na rekodi yake nzuri, mgombea wa CCM ambaye ni ndugu Magufuli atabebwa na ukubwa wa chama chake, mapenzi ya wananchi walio wengi kwa CCM na ile hali ya ukweli kuwa imekita mizizi mpaka ngazi za chini.

3. Kushindwa kwa wapinzani kuungana. Kwanza niweke wazi, hata wapinzani wakiungana, bado kura zao haziwezi kumfikia Rais Magufuli lakini angalau wangepata kura kadhaa. Kitendo Cha kutoungana kinaonesha hawaaminiani hivyo watachafuana wenyewe kwa wenyewe na watajodhoofisha kabla ya kufikia sanduku la kura. Inashangaza eti inakuwa Jambo kubwa kwa wapinzani kuhamia Upinzani. Yaani huu ndio ule mchezo wa sifuri kugeuza o. Wajifunze kwa mataifa yaliyoendelea. Wanahitaji wawe na chama kimoja cha Upinzani chenye nguvu. Ni dhahiri ujio wa Membe utapunguza pakubwa kura za CHADEMA.

4. Wananchi wengi kupoteza imani yao kwa vyama vya Upinzani. Pamoja na ukweli kuwa kuunga nkono jitihada za mh Rais ni jambo jema lakini wananchi waliowachagua wadiwani na wabunge wa Upinzani na kuwaacha CCM walihuzunika sana kuona viongozi hao wakitimkia CCM. Sasa wengi wao wanaona bora tuu nao waunge juhudi kwa kura zao na wale wachache wanaobaki wanasema hatupigii tena Upinzani kwani hawaaminiki na hatuipigii CCM vilevile. Hawa Ni rahisi kuwashawishi wwkaipigia CCM na ikitokea hawakupiga basi wapinzani ndio wanaopata hasara kwani wapoga kura wa CCM hawajabadilika zaidi sana wameongezeka.

5. Watu wengi wanaounga mkono upinzani walisusa kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura. Hawa hawataweza kuwachagua viongozi wao. CCM ilifanya vizuri kwa kuhakikisha wananchama wake wamejiandikisha.

#tukutaneoktoba
 
1. Elimu bure kwa kweli ipo kwenye makaratasi tu, hili ili lieleweke vizuri lingisemwa hivi magufuli karuhusu watoto wa wanyonge kwenda kuzurura na kushinda bure ktk majengo ya serekali yanayoitwa shule, wazazi wanahaha kuzibua vyoo na kuchoma mahindi ili wapeleke watoto shule za private wakapate elimu ya kweli
Hilo sasa ndio tatizo lenu lilipo na watanzania watawalipa kwa kumpa Magufuli kura nyingi na kumchagulia madiwani na wabunge Kama wote wa kumsaidia.
Tunajua zipo changamoto katika utekeleza was sera ya elimu ya nwaka 2014 ambayo imetoa fursa tmya watoto wetu kusoma bila ya kulipa ada na michango mbalimbali lakini changamoto hizo haziifanyi jitihada za serikali kuingiza bilioni 23 kila mwezi kuwa kazi bure
 
Chadema.. hawana vya dijitali.. eti wataqeka ya wananchi wanunue hisa.. kiganjani.. hata wa vijijini.. uchumi ukue..😃😃😃😃 vituko vya kuwemo.. ndani ya futi sita.. ndotooooo
Charity begins at home & actions speak louder than words. Wajenge kwanza ofisi ya makao makuu inayofanana na:
Ruzuku wanayopata
Michango ya lazima ya milioni moja wanayowakata wabunge wao
Misaada na hisani kutoka kwa watu wanaojulikana
 
4. Usambazaji umeme hizi credit kwa kweli ziende tu kwa mkwele asilimia 90 ya umeme shy kasambaza kikwete so kwa porojo zako hizi sisi wanashinyanga kwa pamoja kura zetu tunampa tundu lissu
Karibu CCM, karibu chama kubwa.
Asante sana kwa hizo credits
 
3. Majengo yanayoitwa zahanati kwa kweli yapo tangia utawala wa kikwete na hayana madaktari wala wauguzi ngazi za manesi kama ni huduma za kutalii majengo ya zahanati pongezi nazipeleka kwa kikwete ila kwa upande wa quality zile zahanati ni majengo bila huduma
Akina mama wajawazito, wazee na wagonjwa wanajua kazi iliyofanyika. Wewe endelea kubeza.
 
Back
Top Bottom