Uchaguzi 2020 Ni kwanini upinzani utashindwa vibaya na CCM Itashinda kwa kishindo?

Uchaguzi 2020 Ni kwanini upinzani utashindwa vibaya na CCM Itashinda kwa kishindo?

Mm mkazi wa mbulu mkoani Manyara niambieni hayo aliyoyafanya Magufuli
Kwa mwananchi wakawaida kama mm
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nimepitia posti mbalimbali, wengi wanataka kujua ni nini serikali ya Tanzania chini ya Magufuli imemfanyia.

Ninetembea sehemu nyingi Tanzania Ila ninaomba mniwie radhi, sina takwimu za kila sehemu, nitatoa majibu ya jumla. Ninaomba wale waliopo kwenye maeneo ya hawa ndugu zetu wanisaidie kuwapa majibu mahususi.

Usambazaji wa umeme vijijini unafanyika nchi nzima
Elimu bila malipo kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha nne - nchi nzima
Ujenzi wa barabara za lami - maeneo Mengi ya Tanzania na kuunganisha wilaya na mikoa
Ujenzi wa vituo vya afya na kuimarisha upatikanaji wa madawa na vifaa tiba - nchi nzima
Nidhamu serikalini hivyo kuimarisha huduma za serikali kwa wananchi - nchi nzima
Uimarishaji wa hospitali za mikoa kwa kuzikarabati na kuongeza wataalam - nchi nzima
Ndege zinaongeza mapato serikalini kwa kuimarisha na kurahisha shughuli za usafiri na usafirishaji. Hii ni moja ya hatua za kukuza utalii wa ndani na nje.
Ujenzi wa flyovers ni kupunguza foleni na kurahisha shughuli za usafiri na usafirishaji. Hapa kiuchumi unaporahisha shughuli za usafiri na usafirishaji kwa kuokoa muda, basi unaokoa fedha nyingi kwani huduma zinaboreka wafanyakazi na wafanyabiashara wanafanya vizuri na kuongeza kipato. Pia ni kivutio kimoja wapo cha utalii.
Stiglers gorge ikikamilika itatupa umeme mwingi, wa uhakika na nafuu. Utasambazwa majumbani na viwandani. Uneme huu unaweza pia kuuzwa nje ya Tanzania. Pato la serikaoi litakuwa, ajira zitaongezeka na gharama za uzalishaji zitapungua.

Kipato imara cha serikali ndio kinawezesha kujenga barabara, hospitali za wilaya na zahanati, elimu bure, kulipa mishahara, mikopo ya elimu ya juu nchi nzima.

Najua zipo changamoto, ila Magufuli na serikali yake wamethubutu, taa ya kijani sasa imewaka. Twendeni pamoja.
 
Hilo sasa ndio tatizo lenu lilipo na watanzania watawalipa kwa kumpa Magufuli kura nyingi na kumchagulia madiwani na wabunge Kama wote wa kumsaidia.
Tunajua zipo changamoto katika utekeleza was sera ya elimu ya nwaka 2014 ambayo imetoa fursa tmya watoto wetu kusoma bila ya kulipa ada na michango mbalimbali lakini changamoto hizo haziifanyi jitihada za serikali kuingiza bilioni 23 kila mwezi kuwa kazi bure
changamoto hizo babu yenu zimemshinda tuna imani na lissu atazitatua ndani ya muda mchache
 
Chadema in
Awali ya yote, napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza ndugu Bernard Camilius Membe na ndugu wakili msomi Tundu Antipas Lissu kwa kuaminiwa na kuteuliwa kupeperusha bendera za vyama vyao katika kinyang'anyiro cha urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, 2020. Ni rasmi sasa watachuana na Rais Magufuli.

Uchaguzi ni uchaguzi na hakuna uchaguzi rahisi. Hatahivyo, Rais Magufuli na CCM kwa ujumla watashinda kwa kishindo. Twende pamoja:

1. Rais Magufuli na chama chake, CCM wana ajenda mahususi za uchaguzi mkuu. CCM chini ya Magufuli wanataka kukamilisha kazi kubwa waliyoianza. Hapa hapatakuwa na matumizi ya nguvu bali nguvu ya hoja. CCM wataonesha walichokifanya ndani ya miaka 5 na watawaomba watanzania waendelee kuwaamini kwa miaka 5 ijayo. Kwavile kazi imefanyika kweli na watanzania wameona, basi hakutakuwa na tabu. Upande wa pili, wapinzani hawana hoja wanayoisimamia kwa Sasa.

Naomba niwakumbushe kuwa katika nchi zinazoendelea Kama Tanzania, ajenda kubwa huwa ni maendeleo na CCM chini ya Magufuli wamefanikiwa kwenye ajenda hii. Wapinzani wataleta ajenda ipi? Huko kupinga kila kitu? Watanzania wameamka.

2. Uimara wa vyama. CCM ni chama imara chenye mizizi mpaka ngazi ya shina. Vyama vingine vipo mijini tuu. Pamoja na rekodi yake nzuri, mgombea wa CCM ambaye ni ndugu Magufuli atabebwa na ukubwa wa chama chake, mapenzi ya wananchi walio wengi kwa CCM na ile hali ya ukweli kuwa imekita mizizi mpaka ngazi za chini.

3. Kushindwa kwa wapinzani kuungana. Kwanza niweke wazi, hata wapinzani wakiungana, bado kura zao haziwezi kumfikia Rais Magufuli lakini angalau wangepata kura kadhaa. Kitendo Cha kutoungana kinaonesha hawaaminiani hivyo watachafuana wenyewe kwa wenyewe na watajodhoofisha kabla ya kufikia sanduku la kura. Inashangaza eti inakuwa Jambo kubwa kwa wapinzani kuhamia Upinzani. Yaani huu ndio ule mchezo wa sifuri kugeuza o. Wajifunze kwa mataifa yaliyoendelea. Wanahitaji wawe na chama kimoja cha Upinzani chenye nguvu. Ni dhahiri ujio wa Membe utapunguza pakubwa kura za CHADEMA.

4. Wananchi wengi kupoteza imani yao kwa vyama vya Upinzani. Pamoja na ukweli kuwa kuunga nkono jitihada za mh Rais ni jambo jema lakini wananchi waliowachagua wadiwani na wabunge wa Upinzani na kuwaacha CCM walihuzunika sana kuona viongozi hao wakitimkia CCM. Sasa wengi wao wanaona bora tuu nao waunge juhudi kwa kura zao na wale wachache wanaobaki wanasema hatupigii tena Upinzani kwani hawaaminiki na hatuipigii CCM vilevile. Hawa Ni rahisi kuwashawishi wwkaipigia CCM na ikitokea hawakupiga basi wapinzani ndio wanaopata hasara kwani wapoga kura wa CCM hawajabadilika zaidi sana wameongezeka.

5. Watu wengi wanaounga mkono upinzani walisusa kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura. Hawa hawataweza kuwachagua viongozi wao. CCM ilifanya vizuri kwa kuhakikisha wananchama wake wamejiandikisha.

#tukutaneoktoba
Chadema inatosha sana kuishinda ccm katika uchaguzi wa haki na huru hata bila kuungana na vyama vingine.
 
UKweli mchungu
 
1.Elimu bure kwa watoto wetu kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha 4.
2. Ujenzi wa barabara

Bonus points
3. Ujenzi wa vituo vya afya
4. Uimarishaji wa usambazaji wa umeme vijijini

Naomba watu wa Shytown wamuongezee
Akikurudia nitag
 
miundombinu hata mkoloni alijenga na bado walikataliwa na kutolewa nduki na jiulize kwa nini walin'golewa jibu sahihi utakalopata ndilo linakwenda kuitoa ccm madarakani kiufupi ccm awamu ya tano imegusa pabaya sana na si hapa tanzania tu popote pale duniani kiongozi mpumbavu ni yule anayechezea uhuru na, haki za watu. HAPA TZ SASA IMETOSHA KWA SABABU WATANZANIA NI WATU SI WANYAMA ." Hii ni nature si mimi"
 
Mimi mkazi wa mkoa wa shinyanga naomba nitajiwe mambo makubwa mawili aliyoifanyia shy ili kura yangu nisimpe tundu lissu
Tundu lissu amefanya mambo gani makubwa achilia mbali madogo huko Shinyanga hadi umchague?
 
We kweli ccm mpya 😂😂😂😂😂😂
 
Swali zuri sana mimi pia wa Heru Juu Manyovu Kasulu mkoani Kigoma CCM Mpya wanieleze yale ma-bombadier, flyovers za baharini, kipande kifupi cha SGR Reli Dar -Moro kinachoendelea kujengwa, Stiegler's gorge yamenigusa vipi mimi mkaazi wa Manyovu? Sana sana wametuulia kilimo na masoko yake kwa kusahau sekta hii ya maharage, pamba, korosho, uvuvi wa dagaa na samaki.

Kura yangu nampa Tundu Antipas Lissu maana chama cha Demokrasia na Maendeleo ya Watu kinanivutia na kunipa matumaini kuliko sera za Maendeleo ya Vitu.
Kwa kweli kama hizi ndizo akili za hawa wanaojiita wapinzani (mbumbumbu) bora ccm iendelee tu kutawala miaka 100 ijayo.
 
changamoto hizo babu yenu zimemshinda tuna imani na lissu atazitatua ndani ya muda mchache
Kama tu ofisi ya chama imewashinda kujenga hadi mnapanga kwenye nyumba ya mgongo wa tembo huko mtaa wa ufupi kwa zaidi ya miaka 25 mtaweza kweli kujenga nchi?
 
Kwa hiyo wakiingia wapinzani watatoa ajira?? Mbona sasa hatuoni hata wakitoa hizo ajira kwenye vyama vyao tu, ili iwe mfano?
Anadhani tundu lisu ana bohari ya ajira ameifungia miaka yote hiyo ili akipewa uraisi afungue bohari hiyo aanze kugawa ajira kama wanavyogawa chakula kwenye sherehe za kijamii
 
Tundu lissu amefanya mambo gani makubwa achilia mbali madogo huko Shinyanga hadi umchague?
kikomo cha elimu yako ni darasa la ngapi kwanza? Make kwa hili swali hadi nimekuonea aibu
 
Kama tu ofisi ya chama imewashinda kujenga hadi mnapanga kwenye nyumba ya mgongo wa tembo huko mtaa wa ufupi kwa zaidi ya miaka 25 mtaweza kweli kujenga nchi?
nyerere alikomboa hii nchi ofisi za tanu zikiwa chini ya muembe nini nyumba ya mgongo wa tembo? Kwanza hata ccm ofisi zake zote ilinyanganya majengo ya wahindi na mabeberu kwa nguvu
 
Umeandika kama unakimbizwa...mwaka huu mtakiona cha moto yaani iwe kwa sanduku la kura ama kwa damu!
 
Back
Top Bottom