Nimepitia posti mbalimbali, wengi wanataka kujua ni nini serikali ya Tanzania chini ya Magufuli imemfanyia.
Ninetembea sehemu nyingi Tanzania Ila ninaomba mniwie radhi, sina takwimu za kila sehemu, nitatoa majibu ya jumla. Ninaomba wale waliopo kwenye maeneo ya hawa ndugu zetu wanisaidie kuwapa majibu mahususi.
Usambazaji wa umeme vijijini unafanyika nchi nzima
Elimu bila malipo kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha nne - nchi nzima
Ujenzi wa barabara za lami - maeneo Mengi ya Tanzania na kuunganisha wilaya na mikoa
Ujenzi wa vituo vya afya na kuimarisha upatikanaji wa madawa na vifaa tiba - nchi nzima
Nidhamu serikalini hivyo kuimarisha huduma za serikali kwa wananchi - nchi nzima
Uimarishaji wa hospitali za mikoa kwa kuzikarabati na kuongeza wataalam - nchi nzima
Ndege zinaongeza mapato serikalini kwa kuimarisha na kurahisha shughuli za usafiri na usafirishaji. Hii ni moja ya hatua za kukuza utalii wa ndani na nje.
Ujenzi wa flyovers ni kupunguza foleni na kurahisha shughuli za usafiri na usafirishaji. Hapa kiuchumi unaporahisha shughuli za usafiri na usafirishaji kwa kuokoa muda, basi unaokoa fedha nyingi kwani huduma zinaboreka wafanyakazi na wafanyabiashara wanafanya vizuri na kuongeza kipato. Pia ni kivutio kimoja wapo cha utalii.
Stiglers gorge ikikamilika itatupa umeme mwingi, wa uhakika na nafuu. Utasambazwa majumbani na viwandani. Uneme huu unaweza pia kuuzwa nje ya Tanzania. Pato la serikaoi litakuwa, ajira zitaongezeka na gharama za uzalishaji zitapungua.
Kipato imara cha serikali ndio kinawezesha kujenga barabara, hospitali za wilaya na zahanati, elimu bure, kulipa mishahara, mikopo ya elimu ya juu nchi nzima.
Najua zipo changamoto, ila Magufuli na serikali yake wamethubutu, taa ya kijani sasa imewaka. Twendeni pamoja.