Ni kwanini walimu wanadharaulika sana mitaani?

Leo hii mnawasema, mnawachambua na kuwadharau Walimu lakini niwakumbushe tu hata huu uwezo wa kuandika haya maadishi ni msaada wa mwalimu ndiyo unakufanya uweze kuandika na kusoma.

Mwalimu ndiyo anazalisha Doctors, engineer, lawyers na kada nyingine. Lakini hao hao watu waliopitia kwa mwalimu na kupata taaluma zao wanarudi kumtukana na kumkejeli mwalimu.

Yaani mtu aliyepambana katika kukupatia Elimu leo hii unaanza kumuona mshamba, hajui kuvaa, hajui kutembea! Really??? Ni mtu mpumbavu pekee ambae anaweza kumdharau mwalimu kwa hali yoyote ili lakini mtu mwenye akili timamu hawezi kumdharau na kumkashfu mwalimu kwasababu anajua umuhimu wa mwalimu katika maisha yake.
 
Mbona vyuoni mnasomea ualimu,juzi zimetangazwa nafasi 7000 mmeomba zaidi ya 100,000.Mnaombaje kazi isiyolipa?wanafiki nyie
 
Ni ukweli mtupu umeongea, kisheria tunasema umeprovide material fact. Ila kumbuka yafuatayo.

1.Kuwa na gari sio maendeleo hiyo ni liability not an asset.

2.Hao vijana unaowaona ni smart, ni wale checkbob ambao ndowanalawiti wanafunzi nakuwakatili kingono, rejea kesi ya yule mwalimu wa global international school.

3.Kukopa kupo kwa kila mtu, shida inakuja kuhimili huo mkopo na maisha yako ya kila siku. Hata wabunge wanamadeni ila sasa tunakuja kuangalia je hilo deni litaendelea kumfanya awe comfortable?, usiwe unakopa ukashindwa hata kuvaa nguo nzuri mwishowe ukajinyonga kwa madeni kama yule jamaa wa shinyanga.

4.Basic salary ya mwalimu ni aibu, taasisi zingine zinamishahara inayojali utu na inakidhi mahitaji. Sasa nikiwaambia mishahara yao ni duni inabidi serikali ifanye marekebisho wao wananijia juu.

5.Yote kwa yote walimu ni potential sana tena sana kwenye jamii zetu hilo lipo wazi, ndio maana nawaambia wasikubali kuwa kituko kwenye macho ya viongozi inabidi wawe chachu ya mabadiliko. Inabidi wafanye strike maana wana makato mengi sana na hayo makato yanaishia kwa wapiga dili.
 
Hao hao wanaodharaulika ndio waliotoa wengine wakawa Marais, mawaziri, mainjinia, madaktari, kwa hiyo uonayo ni IQ ndogo. Wewe unaonekana smart na hao walimu primitive... Lakini walikufundisha namna ya kupenga kamasi na kuondoa tongotongo usoni. Ni primitive sawa lakini wanaondolea watoto wetu primitivity. Mimi niwashukuru walimu kwa kazi njema isiyo na shukrani . Sisi wazazi hatuwezi kazi zenu, Mungu awabariki , awalinde muendelee kuhudumia taifa. Mti uzaao matunda ndio upigwao mawe.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
2 tunakufungulia mashitaka umemkashifu kiongozi wa nchi
 
Watumishi wa Umma kwa idadi yao inajulikana, Walimu ndio wengi kwa idadi yao kwahiyo ni rahisi mno kuwaona mtaani na siku za mishahara ni jambo la kawaida kila mtu kwenda kuchukua haki yake.

Kuhusu uliyoandika kuwahusu Walimu na akili zao, kila mwenye akili timamu atakubaliana na mimi kuwa wewe ni mtoto mdogo uliyekosa maarifa na adabu au kama una umri mkubwa basi ni miongoni mwa watu wa hovyo wanaopatikana katika jamii yetu.

Kwa maelezo yako wewe hata kama utakuwa Engineer, Daktari, Mhasibu...bado ukiwa ofisini utawadharau wale wenye elimu ya cheti au vibarua.

Na haya unayoandika ni dalili za mtu aliyekosa ajira kwahiyo anahisi ajira za Walimu ni upendeleo wakati yeye alichokisoma hakijapewa kipaumbele.

Kuhusu Walimu kushiriki shughuli za kitaifa kama wasimamizi na sio kada nyingine hujajiuliza, hata hao wengine hawajakatazwa na wanashiriki kuanzia Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Wakurugenzi na Polisi. Sasa kama ulitaka Walimu wakawe walinda usalama kwenye sensa au wakawe madaktari ili hizo kada nyingine zikafanye kazi ya kuandika majina utakuwa mtu wa ajabu kweli.

Kwenye uchaguzi au Sensa au jambo lolote lile la kitaifa kila kada ipo, Engineers wapo kwenye mifumo, Watu wa mahesabu na takwimu wapo, Watu wa Sera na mipango wapo, Jeshi na Polisi wapo pia.

Kuhusu maisha yao na akili zao umechukua sample yako ukaifanya kuwa jibu, mishahara ya Walimu na kada nyingine inajulikana, kinachotofautisha ni mianya ya WIZI tu na sio ukubwa wa mishahara.
 
Tunakufungulia mashitaka ya kuvunja ndoa za watu,Sheria ya 1979 kifungu cha 14
 
Nasema naanza kupata mashaka na uelewa wako. Hoja zote nilizoandika hayo ndio majibu yako?? Are u serious??

Hebu soma tena kwa makini nilichoandika then njoo na majibu yanayoeleweka bandiko lako lilionesha hawa ni watu ambao hawajiwezi nimekupa mfano wana magari unaanza kusema hiyo ni liability.

Issue sio asset or liability ni uwezo wa kuafford. Na huo uwezo wanao.

Kuhimili deni nimesema nashindwa kudisclose some info but reality ni wengi wapo kama hao waalimu acha kulisha watu upepo.
 
Hakuna wafanyakazi wa Serikali ambao kichwani ni weupe kama waalimu ni haki yao kudharauli.

1. Imagine ...Mtu aliyemaliza sekondari ya kata kafanyiwa mchakato tu huko na ndugu na jamaa kwa sababu kaonekana kichwani hamna kitu ...Kapelekwa Kondoa Teachers college Ili aje akufundishie mtoto wako awe Pilot! Hivi mnanielewa?


2. Nimebahatika kuwa na Shemeji Mwalimu
Alikuwa anakuja na maswali aliyoulizwa na watoto shuleni kuja nimpe majibu Ili awapelekee kesho yake ....aliyaweka pending [emoji3] Huwa anawaambia watoto kwa sababu ya muda tutaendelea kesho fanyeni hiyo kazi hapo ubaoni kwanza[emoji23]

Mtoto alimuuliza Mwalimu kwa Nini Tanzania na Rwanda zinapishana lisaa limoja dakika zile zile
Mtoto alisikia kwende Taarifa ya habari ya saa saba mchana DW ya ujerumani
Shemeji anasema siku Ile watoto wengi walisubiria hilo jibu sana
Anakuambia hakuna siku ilikuwa ngumu kama Ile

3. Kazi ya Ualimu ni laana ..Ukiona mtu anajivunia mkopo wa Serikali ambao anakatwa kwenye mshahara wake na kumfanya aishi maisha magumu na wengine tunaona hadi wanajiuza miili yao elewa kuna tatizo mahali flani

SWALI LANGU NAJIULIZA KILA SIKU

Hivi Serikali inanufaika Nini
Watu wasio na sifa ndio wategemewe kuzalisha Viongozi wa nchi?
Okay Iko hivi angalia Hali ya ufahamu wa mwalimu then kesho kutwa usikie kazalisha waziri wa Nishati unategemea nini? asanteni.
 
Baadhi ya watu wana uelewa na busara ndogo sana inabidi tuwaache tu
 
Aya bhana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…