Ni kwanini walimu wanadharaulika sana mitaani?

Ni kwanini walimu wanadharaulika sana mitaani?

Leo hii mnawasema, mnawachambua na kuwadharau Walimu lakini niwakumbushe tu hata huu uwezo wa kuandika haya maadishi ni msaada wa mwalimu ndiyo unakufanya uweze kuandika na kusoma.

Mwalimu ndiyo anazalisha Doctors, engineer, lawyers na kada nyingine. Lakini hao hao watu waliopitia kwa mwalimu na kupata taaluma zao wanarudi kumtukana na kumkejeli mwalimu.

Yaani mtu aliyepambana katika kukupatia Elimu leo hii unaanza kumuona mshamba, hajui kuvaa, hajui kutembea! Really??? Ni mtu mpumbavu pekee ambae anaweza kumdharau mwalimu kwa hali yoyote ili lakini mtu mwenye akili timamu hawezi kumdharau na kumkashfu mwalimu kwasababu anajua umuhimu wa mwalimu katika maisha yake.
 
Mbona vyuoni mnasomea ualimu,juzi zimetangazwa nafasi 7000 mmeomba zaidi ya 100,000.Mnaombaje kazi isiyolipa?wanafiki nyie
 
Baada ya kusoma huu uzi ninegundua yafuatayo:
Bado kuna baadhi ya wana JF wana uelewa mdogo sana katika kuchambua vitu wanaendeshwa na upepo wa hoja na sio current realistic situation.

1. Unadhifu:
Kusema walimu sio nadhifu nakataa kabisa kwa walimu wengi tunaowaona kwa sasa ni vijana and in most cases they are smart. Tuache wale wanaoenda kustaafu (wazee)

2. Madeni:
Siwatetei walimu ila kwenye swala la madeni sio waalimu pekee taasisi tulizopo tunapokea watu wa kila kada na ofcourse ukiangalia SP zao madeni ni ya kutosha km walimu tu, tatizo ni kwamba walimu ni wengi kidogo kuliko kada nyingine that's why wanaonekana wana madeni sn. Sitaki kwenda deep kwa hili coz its not allowed to disclose customers info. (Ila hata wale wa kada smart[emoji23] wana madeni sana. Shida hawana walimu tu naomba ieleweke hivyo)

3. Elimu:
Recently walimu wenye bachelor wameanza kupelekwa kufindisha hadi watoto wa shule za msingi. Pia kuna kada kama nursing naona kwenye matangazo ya TV wanasema mhusika awe form four leaver na awe na D mbili au tatu. (Hawa nao vip?) Kwanin wahanga ni walimu tu?? Mtoa mada anipe jibu?

4. Kipato:
It's obvious mkiwa wengi share lazima itakuwa ndogo but Recently walimu wana drive tena wa shule za msingi. Wengine wamefungua maduka ya dawa na wemewaajiri wale wa kada smart[emoji846][emoji23]. Naongea haya sababu tunayaona ukienda mashulen walimu wamepaki Mikebe wengine keyboard warriors tunasema wana hali mbaya na hatuna hata boda[emoji56][emoji56][emoji38]

5. Dharau:
Ni uelewa ule ule msaada wa walimu kwa mtoto wangu siwezi kuubeza kwa namna yeyote ile. Tupo bize na uzi kutafunana kimasihara na mkishafyatua watoto mnawakimbiza huko huko kwa hao mnaosema wamefeli[emoji1][emoji1] why usiwapeleke nje???

Way Forward:
Sisi ndio matokeo ya walimu kuwa wengi sababu tunazaana mno na serkali yetu haiwezi kuhudumia wingi huu km vile tunavyotaka la tupunguze kuzaana na tuache kusoma ule uzi wenu pendwa[emoji39][emoji2960].

Mnatoa mifano walimu wa ng'ambo kuwa they are highly educated & their paychecks are awesome ila mnasahaua wanahudumia idadi ndogo sana ya wanafunzi (Wazungu uzazi wa mpango ndio life style yao) kulinganisha na sisi huku Africa ambapo kwa utamaduni wetu watoto wengi ndio mtaji na ufahari. Why hatutumii akili kuona haya??

Nilifikiri badala ya mtoa uzi au mada kudhihaki waalimu ambao naamini hata yeye amepita kwenye mikono yao (Labda km kusoma nje). Angesema mini hasa kufanyike badala ya kebehi tusidharau mchango wa walimu hata kidogo. Juzi ilitokea Corona, shule zikafungwa kwa kweli tulitafutana sasa zingefungwa mwaka hata sijui ingekuwaje[emoji23][emoji23][emoji23]

These people need special treatment and respect they do more than what they put in their pockets.

Respect Sir. [emoji1812]
Ni ukweli mtupu umeongea, kisheria tunasema umeprovide material fact. Ila kumbuka yafuatayo.

1.Kuwa na gari sio maendeleo hiyo ni liability not an asset.

2.Hao vijana unaowaona ni smart, ni wale checkbob ambao ndowanalawiti wanafunzi nakuwakatili kingono, rejea kesi ya yule mwalimu wa global international school.

3.Kukopa kupo kwa kila mtu, shida inakuja kuhimili huo mkopo na maisha yako ya kila siku. Hata wabunge wanamadeni ila sasa tunakuja kuangalia je hilo deni litaendelea kumfanya awe comfortable?, usiwe unakopa ukashindwa hata kuvaa nguo nzuri mwishowe ukajinyonga kwa madeni kama yule jamaa wa shinyanga.

4.Basic salary ya mwalimu ni aibu, taasisi zingine zinamishahara inayojali utu na inakidhi mahitaji. Sasa nikiwaambia mishahara yao ni duni inabidi serikali ifanye marekebisho wao wananijia juu.

5.Yote kwa yote walimu ni potential sana tena sana kwenye jamii zetu hilo lipo wazi, ndio maana nawaambia wasikubali kuwa kituko kwenye macho ya viongozi inabidi wawe chachu ya mabadiliko. Inabidi wafanye strike maana wana makato mengi sana na hayo makato yanaishia kwa wapiga dili.
 
Hili sio uongo lipo wazi kabisa moja ya watumishi wa serikali wanaodharaulika kwenye jamii ni hili kundi la walimu. Hata muonekano wao umekuwa ni too primitive huku wakijidifence eti ni dressing code ya mwalimu lakini nguo zao huwa ni zilezile Shati kubwa ndefu na suruali iliyopwalaruka. Hata wakiwa wanatembea wamejawa na msongo wa mawazo wananuka madeni kila kona utakuta wanadaiwa kila duka mala kakopa dagaa, kakopa sukari, kakopa Unga, kakopa Mchele, mafuta na kila aina ya takataka dhamana yake ni kazi aliyonayo kwahiyo mda wote anaangalia tarehe ya mshahara ikifika tu ndowanakuwa wa kwanza kujazana benki yani siku hiyo panakuwa hapatoshi ni kero tupu, siku za mshahara almost zipo sawa kwa kila mtumishi wa umma ila walimu ikifika net day of salary yupo benki nadhani ni kutokana na madeni aliyonayo pamoja na ukata wa nyumbani maana hawa watu wanalisha Familia kubwa, ya kwake na ndugu zake.

Hii tabia imekuwa ikinifanya nakwazika nakuwaonea huruma pia. Fedheha nyingine nikuwa walimu wengi wanaenda wenye hakili ndogo au waliofeli hili hata Samia alilisema zanzibar, hali hii imekuwa ikipelekea ongezeko kubwa la walimu mitaani wasionaajira bahati mbaya hawana skills zakujiajiri kutokana na low IQ waliyonayo kwahiyo matazamio yao ni kusaka huruma za watawala ili wawaajiri.

Mifano iko wazi, hizi ajira za juzi zilizotangazwa na tamisemi za afya na walimu, idadi kubwa ya walioomba ni walimu, waliomba zaidi ya laki moja wakigombania nafasi elfu tisa lakini afya hawakuzidi elfu thelasini kwa nafasi elfu saba. Hapo unaweza ukaona urahisi una gharama zake, ualimu ni ajira za watu wenye level ndogo ya uelewa darasani lakini udaktari sio program ya kitoto hiyo wanaoenda ni PCB smart hakuna matapitapi ya HKL wala wenye four za form six.

Njaa za walimu zimezidi mipaka. Kwanza hawana subira, angalia tu hizi ajira walizotoa tamisemi, walimu wanasumbua hadi aibu naona mimi, ukiingia kwenye mitandao ya kijamii wanatia huruma hadi kinyaa. Utasikia toeni pdf, mda wote utasikia toeni majina hawajui wizara Ina kazi nyingi za kufanya halafu majina yakitoka siku hiyo hiyo kero inaanza wa naanza kuuliza ajira za walimu mnatoa lini.

Mimi nadhani hii sekta ya walimu kama wizara mnaidekeza sana ndio mana mnawageuza kama cheap labor kwenye kazi za kitaifa kama sensa na uchaguzi mkuu maana mnajua wanalipika kwa pesa ya mrenda. Mbona hamuwachukui madaktari na watu wa TRA au TPDC tuone kama watakubali viajira vya sensa. Sasa mtazamo wangu walimu waanze kwenda wenye ufaulu mzuri kama kada zingine, hii itasaidia kupunguza idadi kubwa ya walimu wenye njaa njaa wanalia saaana,

Walimu waanze kupigwa interview kama kada zingine za utumishi ili kubaini vilaza na smart. Hii hali itapunguza mlundikano wa hawa watu kwenye competition za ajira. Wapigwe oral na written interview ili akili ziwakae sawa. Mbona tuliosoma kada zingine tunakaa mitaani miaka zaidi ya minne nahatusikii ajira zimetangazwa na hata zikitoka hatuanzi kero za kudai majina kwa haraka kama tunakimbizwa. Walimu hawana uvumilivu.

Sina Nia mbaya ila haya mawazo niliyotoa kama yatafanyiwa kazi basi walimu wataanza kuheshimika kama wafanyakazi wengine wa serikalini. View attachment 2271988
Hao hao wanaodharaulika ndio waliotoa wengine wakawa Marais, mawaziri, mainjinia, madaktari, kwa hiyo uonayo ni IQ ndogo. Wewe unaonekana smart na hao walimu primitive... Lakini walikufundisha namna ya kupenga kamasi na kuondoa tongotongo usoni. Ni primitive sawa lakini wanaondolea watoto wetu primitivity. Mimi niwashukuru walimu kwa kazi njema isiyo na shukrani . Sisi wazazi hatuwezi kazi zenu, Mungu awabariki , awalinde muendelee kuhudumia taifa. Mti uzaao matunda ndio upigwao mawe.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Mada zako
 
Attachments

  • Screenshot_20220626-085445.jpg
    Screenshot_20220626-085445.jpg
    40.9 KB · Views: 8
2 tunakufungulia mashitaka umemkashifu kiongozi wa nchi
Screenshot_20220626-085537.jpg
 
Watumishi wa Umma kwa idadi yao inajulikana, Walimu ndio wengi kwa idadi yao kwahiyo ni rahisi mno kuwaona mtaani na siku za mishahara ni jambo la kawaida kila mtu kwenda kuchukua haki yake.

Kuhusu uliyoandika kuwahusu Walimu na akili zao, kila mwenye akili timamu atakubaliana na mimi kuwa wewe ni mtoto mdogo uliyekosa maarifa na adabu au kama una umri mkubwa basi ni miongoni mwa watu wa hovyo wanaopatikana katika jamii yetu.

Kwa maelezo yako wewe hata kama utakuwa Engineer, Daktari, Mhasibu...bado ukiwa ofisini utawadharau wale wenye elimu ya cheti au vibarua.

Na haya unayoandika ni dalili za mtu aliyekosa ajira kwahiyo anahisi ajira za Walimu ni upendeleo wakati yeye alichokisoma hakijapewa kipaumbele.

Kuhusu Walimu kushiriki shughuli za kitaifa kama wasimamizi na sio kada nyingine hujajiuliza, hata hao wengine hawajakatazwa na wanashiriki kuanzia Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Wakurugenzi na Polisi. Sasa kama ulitaka Walimu wakawe walinda usalama kwenye sensa au wakawe madaktari ili hizo kada nyingine zikafanye kazi ya kuandika majina utakuwa mtu wa ajabu kweli.

Kwenye uchaguzi au Sensa au jambo lolote lile la kitaifa kila kada ipo, Engineers wapo kwenye mifumo, Watu wa mahesabu na takwimu wapo, Watu wa Sera na mipango wapo, Jeshi na Polisi wapo pia.

Kuhusu maisha yao na akili zao umechukua sample yako ukaifanya kuwa jibu, mishahara ya Walimu na kada nyingine inajulikana, kinachotofautisha ni mianya ya WIZI tu na sio ukubwa wa mishahara.
 
Tunakufungulia mashitaka ya kuvunja ndoa za watu,Sheria ya 1979 kifungu cha 14
Screenshot_20220626-085503.jpg
 
Ni ukweli mtupu umeongea, kisheria tunasema umeprovide material fact. Ila kumbuka yafuatayo.

1.Kuwa na gari sio maendeleo hiyo ni liability not an asset.

2.Hao vijana unaowaona ni smart, ni wale checkbob ambao ndowanalawiti wanafunzi nakuwakatili kingono, rejea kesi ya yule mwalimu wa global international school.

3.Kukopa kupo kwa kila mtu, shida inakuja kuhimili huo mkopo na maisha yako ya kila siku. Hata wabunge wanamadeni ila sasa tunakuja kuangalia je hilo deni litaendelea kumfanya awe comfortable?, usiwe unakopa ukashindwa hata kuvaa nguo nzuri mwishowe ukajinyonga kwa madeni kama yule jamaa wa shinyanga.

4.Basic salary ya mwalimu ni aibu, taasisi zingine zinamishahara inayojali utu na inakidhi mahitaji. Sasa nikiwaambia mishahara yao ni duni inabidi serikali ifanye marekebisho wao wananijia juu.

5.Yote kwa yote walimu ni potential sana tena sana kwenye jamii zetu hilo lipo wazi, ndio maana nawaambia wasikubali kuwa kituko kwenye macho ya viongozi inabidi wawe chachu ya mabadiliko. Inabidi wafanye strike maana wana makato mengi sana na hayo makato yanaishia kwa wapiga dili.
Nasema naanza kupata mashaka na uelewa wako. Hoja zote nilizoandika hayo ndio majibu yako?? Are u serious??

Hebu soma tena kwa makini nilichoandika then njoo na majibu yanayoeleweka bandiko lako lilionesha hawa ni watu ambao hawajiwezi nimekupa mfano wana magari unaanza kusema hiyo ni liability.

Issue sio asset or liability ni uwezo wa kuafford. Na huo uwezo wanao.

Kuhimili deni nimesema nashindwa kudisclose some info but reality ni wengi wapo kama hao waalimu acha kulisha watu upepo.
 
Hakuna wafanyakazi wa Serikali ambao kichwani ni weupe kama waalimu ni haki yao kudharauli.

1. Imagine ...Mtu aliyemaliza sekondari ya kata kafanyiwa mchakato tu huko na ndugu na jamaa kwa sababu kaonekana kichwani hamna kitu ...Kapelekwa Kondoa Teachers college Ili aje akufundishie mtoto wako awe Pilot! Hivi mnanielewa?

2. Nimebahatika kuwa na Shemeji Mwalimu
Alikuwa anakuja na maswali aliyoulizwa na watoto shuleni kuja nimpe majibu Ili awapelekee kesho yake ....aliyaweka pending [emoji3] Huwa anawaambia watoto kwa sababu ya muda tutaendelea kesho fanyeni hiyo kazi hapo ubaoni kwanza[emoji23]

Mtoto alimuuliza Mwalimu kwa Nini Tanzania na Rwanda zinapishana lisaa limoja dakika zile zile
Mtoto alisikia kwende Taarifa ya habari ya saa saba mchana DW ya ujerumani
Shemeji anasema siku Ile watoto wengi walisubiria hilo jibu sana
Anakuambia hakuna siku ilikuwa ngumu kama Ile

3. Kazi ya Ualimu ni laana ..Ukiona mtu anajivunia mkopo wa Serikali ambao anakatwa kwenye mshahara wake na kumfanya aishi maisha magumu na wengine tunaona hadi wanajiuza miili yao elewa kuna tatizo mahali flani

SWALI LANGU NAJIULIZA KILA SIKU

Hivi Serikali inanufaika Nini
Watu wasio na sifa ndio wategemewe kuzalisha Viongozi wa nchi?
Okay Iko hivi angalia Hali ya ufahamu wa mwalimu then kesho kutwa usikie kazalisha waziri wa Nishati unategemea nini? asanteni.
 
Hao hao wanaodharaulika ndio waliotoa wengine wakawa Marais, mawaziri, mainjinia, madaktari, kwa hiyo uonayo ni IQ ndogo. Wewe unaonekana smart na hao walimu primitive... Lakini walikufundisha namna ya kupenga kamasi na kuondoa tongotongo usoni. Ni primitive sawa lakini wanaondolea watoto wetu primitivity. Mimi niwashukuru walimu kwa kazi njema isiyo na shukrani . Sisi wazazi hatuwezi kazi zenu, Mungu awabariki , awalinde muendelee kuhudumia taifa. Mti uzaao matunda ndio upigwao mawe.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Baadhi ya watu wana uelewa na busara ndogo sana inabidi tuwaache tu
 
Watumushi wa Umma kwa idadi yao inajulkana, Walimu ndio wengi kwa idadi yao kwahiyo ni rahisi mno kuwaona mtaani na siku za mishahara ni jambo la kawaida kila mtu kwenda kuchukua haki yake.
Kuhusu uliyoandika kuwahusu Walimu na akili zao, kila mwenye akili timamu atakubaliana na mimi kuwa wewe ni mtoto mdogo uliyekosa maarifa na adabu au kama una umri mkubwa basi ni miongoni mwa watu wa hovyo wanaopatikana katika jamii yetu.
Kwa maelezo yako wewe hata kama utakuwa Engineer, Daktari, Mhasibu...bado ukiwa ofisini utawadharau wale wenye elimu ya cheti au vibarua.
Na haya unayoandika ni dalili za mtu aliyekosa ajira kwahiyo anahisi ajira za Walimu ni upendeleo wakati yeye alichokisoma hakijapewa kipaumbele.
Kuhusu Walimu kushiriki shughuli za kitaifa kama wasimamizi na sio kada nyingine hujajiuliza, hata hao wengine hawajakatazwa na wanashiriki kuanzia Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Wakurugenzi na Polisi. Sasa kama ulitaka Walimu wakawe walinda usalama kwenye sensa au wakawe madaktari ili hizo kada nyingine zikafanye kazi ya kuandika majina utakuwa mtu wa ajabu kweli.
Kwenye uchaguzi au Sensa au jambo lolote lile la kitaifa kila kada ipo, Engineers wapo kwenye mifumo, Watu wa mahesabu na takwimu wapo, Watu wa Sera na mipango wapo, Jeshi na Polisi wapo pia.
Kuhusu maisha yao na akili zao umechukua sample yako ukaifanya kuwa jibu, mishahara ya Walimu na kada nyingine inajulikana, kinachotofautisha ni mianya ya WIZI tu na sio ukubwa wa mishahara.
Aya bhana.
 
Back
Top Bottom