Ni kwanini walimu wanadharaulika sana mitaani?

Ni kwanini walimu wanadharaulika sana mitaani?

Shida ni moja wao Kama wao wanategemea mshahara kuendesha maisha Sasa hapo ni shida bt Sasa ivi nawaona wameanza kujishugulisha na Mambo mengine ya kuwaingizia kipato
Wanajishughulisha na nini?, hakuna chamaana zaidi ya kuuza vitumbua na ubuyu wa rangi mashuleni
 
Mpaka zoezi la sensa liishe walimu watapata shida Sana ya maneno machafu. Vijana wengi wasio na ajira chuki zao nyingi wameelekeza kwa walimu,kisa uwezekano wa wao kupewa kipaumbele.

Kwa hiyo hilo ni kizingiti.
 
Inategemea na mazingira uliyopo. Na aina ya walimu unaowafahamu.
Kama uko kijijini sana usitegemee kumuona mwalimu akiwa tofauti.
Hata watu wa kada nyingine wako hivyohivyo. Inategemea na mazingira.

Darasa limejaa vumbi, barabara hakuna full kukanyaga umande, salon hakuna, usafiri shida, unategemea huyo mtu ataonekana smart kweli?

Serikali iboreshe mazingira yabufundishaji na ujifunzaji, itoe transport allowances utaona tu mabadiliko. Hata walioko Dar, anaefanya kazi mjini -posta hawezi kuwa sawa na wa mbagala.
Yeah sure, umeongea Dada well done
 
Hili sio uongo lipo wazi kabisa moja ya watumishi wa serikali wanaodharaulika kwenye jamii ni hili kundi la walimu. Hata muonekano wao umekuwa ni too primitive huku wakijidifence eti ni dressing code ya mwalimu lakini nguo zao huwa ni zilezile Shati kubwa ndefu na suruali iliyopwalaruka. Hata wakiwa wanatembea wamejawa na msongo wa mawazo wananuka madeni kila kona utakuta wanadaiwa kila duka mala kakopa dagaa, kakopa sukari, kakopa Unga, kakopa Mchele, mafuta na kila aina ya takataka dhamana yake ni kazi aliyonayo kwahiyo mda wote anaangalia tarehe ya mshahara ikifika tu ndowanakuwa wa kwanza kujazana benki yani siku hiyo panakuwa hapatoshi ni kero tupu, siku za mshahara almost zipo sawa kwa kila mtumishi wa umma ila walimu ikifika net day of salary yupo benki nadhani ni kutokana na madeni aliyonayo pamoja na ukata wa nyumbani maana hawa watu wanalisha Familia kubwa, ya kwake na ndugu zake.

Hii tabia imekuwa ikinifanya nakwazika nakuwaonea huruma pia. Fedheha nyingine nikuwa walimu wengi wanaenda wenye hakili ndogo au waliofeli hili hata Samia alilisema zanzibar, hali hii imekuwa ikipelekea ongezeko kubwa la walimu mitaani wasionaajira bahati mbaya hawana skills zakujiajiri kutokana na low IQ waliyonayo kwahiyo matazamio yao ni kusaka huruma za watawala ili wawaajiri.

Mifano iko wazi, hizi ajira za juzi zilizotangazwa na tamisemi za afya na walimu, idadi kubwa ya walioomba ni walimu, waliomba zaidi ya laki moja wakigombania nafasi elfu tisa lakini afya hawakuzidi elfu thelasini kwa nafasi elfu saba. Hapo unaweza ukaona urahisi una gharama zake, ualimu ni ajira za watu wenye level ndogo ya uelewa darasani lakini udaktari sio program ya kitoto hiyo wanaoenda ni PCB smart hakuna matapitapi ya HKL wala wenye four za form six.

Njaa za walimu zimezidi mipaka. Kwanza hawana subira, angalia tu hizi ajira walizotoa tamisemi, walimu wanasumbua hadi aibu naona mimi ukiingia kwenye mitandao ya kijamii wanatia huruma hadi kinyaa. Utasikia toeni pdf, mda wote utasikia toeni majina hawajui wizara Ina kazi nyingi za kufanya halafu majina yakitoka siku hiyo hiyo kero inaanza wa naanza kuuliza ajira za walimu mnatoa lini.

Mimi nadhani hii sekta ya walimu kama wizara mnaidekeza sana ndio mana mnawageuza kama cheap labor kwenye kazi za kitaifa kama sensa na uchaguzi mkuu maana mnajua wanalipika kwa pesa ya mrenda. Mbona hamuwachukui madaktari na watu wa TRA au TPDC tuone kama watakubali viajira vya sensa. Sasa mtazamo wangu walimu waanze kwenda wenye ufaulu mzuri kama kada zingine, hii itasaidia kupunguza idadi kubwa ya walimu wenye njaa njaa wanalia saaana,

Walimu waanze kupigwa interview kama kada zingine za utumishi ili kubaidi vilaza na smart. Hii hali itapunguza mlundikano wa hawa watu kwenye competition za ajira. Wapigwe oral na written interview ili akili ziwakae sawa. Mbona tuliosoma kada zingine tunakaa mitaani miaka zaidi ya minne nahatusikii ajira zimetangazwa na hata zikitoka hatuanzi kero za kudai majina kwa haraka kama tunakimbizwa. Walimu hawana uvumilivu.

Sina Nia mbaya ila haya mawazo niliyotoa kama yatafanyiwa kazi basi walimu wataanza kuheshimika kama wafanyakazi wengine wa serikalini. View attachment 2271988
Umefanya nifanye ufukunyuzi kidogo kwa jambo uliloandika!
Mpnz wangu(tunaishi pamoja japo hatujafunga ndoa, ila tuna mtoto) ni mwalimu, (shahada), ana miaka 9 kazini, basic salary yake ni 1,235,000/=

Alikopa ili kujenga kwao, aliponiambia habari za kukopa afanye maboresho ya nyumbani kwao nilimuunga mkono, akafanya hivyo....

Nanunua mahitaji yote ya nyumbani, lakini mara nyingi tu hutumia pesa yake kununulia mahitaji ya hapa na pale, sasa haya maisha ya sijui kukopa kila kitu yanahusu walimu wa jnamna gani?

Maana pamoja na kukopa anabaki na ka sh.570k kwa matumizi yake madogo madogo, na kama usingekuwa mkopo angekuwa anakunja zaidi ya 900k kila mwezi, japo si nyingi lakini sio ya kumfanya mtu akope dagaa na mafuta ya kula kwa mangi...

Mimi mshahara wangu hauna tofauti kubwa na wa mpnz wangu, lakini kwetu semina, safari posho na turushwa tunatunisha mifuko na kufanya tuheshimike kidogo kitaa!

Lakini tofauti na rushwa, na hizi seminar + safari hakika nakwambia hali ingekuwa mbaya mnooo, wote tungekuwa tunaugulia ukata!

Kizuri ni kwamba watanzania wanatupa heshima kutokana na rushwa wanazotupa wao wenyewe...

Screenshot_20220625-212016~3.jpg
 
View attachment 2272097
Hasa laki tano inatosha kuishi standard life kwa mujibu wa human development index??
 
Back
Top Bottom