Ni kwanini walimu wanadharaulika sana mitaani?

Shida ni moja wao Kama wao wanategemea mshahara kuendesha maisha Sasa hapo ni shida bt Sasa ivi nawaona wameanza kujishugulisha na Mambo mengine ya kuwaingizia kipato
Wanajishughulisha na nini?, hakuna chamaana zaidi ya kuuza vitumbua na ubuyu wa rangi mashuleni
 
Mpaka zoezi la sensa liishe walimu watapata shida Sana ya maneno machafu. Vijana wengi wasio na ajira chuki zao nyingi wameelekeza kwa walimu,kisa uwezekano wa wao kupewa kipaumbele.

Kwa hiyo hilo ni kizingiti.
 
Yeah sure, umeongea Dada well done
 
Umefanya nifanye ufukunyuzi kidogo kwa jambo uliloandika!
Mpnz wangu(tunaishi pamoja japo hatujafunga ndoa, ila tuna mtoto) ni mwalimu, (shahada), ana miaka 9 kazini, basic salary yake ni 1,235,000/=

Alikopa ili kujenga kwao, aliponiambia habari za kukopa afanye maboresho ya nyumbani kwao nilimuunga mkono, akafanya hivyo....

Nanunua mahitaji yote ya nyumbani, lakini mara nyingi tu hutumia pesa yake kununulia mahitaji ya hapa na pale, sasa haya maisha ya sijui kukopa kila kitu yanahusu walimu wa jnamna gani?

Maana pamoja na kukopa anabaki na ka sh.570k kwa matumizi yake madogo madogo, na kama usingekuwa mkopo angekuwa anakunja zaidi ya 900k kila mwezi, japo si nyingi lakini sio ya kumfanya mtu akope dagaa na mafuta ya kula kwa mangi...

Mimi mshahara wangu hauna tofauti kubwa na wa mpnz wangu, lakini kwetu semina, safari posho na turushwa tunatunisha mifuko na kufanya tuheshimike kidogo kitaa!

Lakini tofauti na rushwa, na hizi seminar + safari hakika nakwambia hali ingekuwa mbaya mnooo, wote tungekuwa tunaugulia ukata!

Kizuri ni kwamba watanzania wanatupa heshima kutokana na rushwa wanazotupa wao wenyewe...


 
Hasa laki tano inatosha kuishi standard life kwa mujibu wa human development index??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…