Ni kwanini walimu wanadharaulika sana mitaani?

Ni kwanini walimu wanadharaulika sana mitaani?

Ukiwa na D nne tu form four unakuwa na sifa ya kusoma kozi Nyingi tu Kwa ngazi ya Diploma 3 years,ila ualimu bila division three mpaka one huendi.Sasa hapo wapi wanachukuliwa wenye ufaulu wa chini?
Clinical officer wakiwa wakina na D nne wanasoma ualimu siku hizi mwisho three ya 25
 
Siwezi kuwasema vibaya walimu kwa sababu naheshimu sana mchango mkubwa kwangu.
Nimeishi kwa walimu darasa la sita hadi la saba.

Kama kuna mapungufu yanayoonekana kwao basi ni kutokana na wao kuwa binadamu tu, lakini si kwa sababu ya ualimu wao.
 
Hili sio uongo lipo wazi kabisa moja ya watumishi wa Serikali wanaodharaulika kwenye jamii ni hili kundi la walimu.

Hata muonekano wao umekuwa ni too primitive huku wakijidifence eti ni dressing code ya mwalimu lakini nguo zao huwa ni zilezile shati kubwa ndefu na suruali iliyopwalaruka.

Hata wakiwa wanatembea wamejawa na msongo wa mawazo wananuka madeni kila kona utakuta wanadaiwa kila duka mala kakopa dagaa, kakopa sukari, kakopa Unga, kakopa mchele, mafuta na kila aina ya takataka dhamana yake ni kazi aliyonayo.

Kwa hiyo muda wote anaangalia tarehe ya mshahara ikifika tu ndowanakuwa wa kwanza kujazana benki yani siku hiyo panakuwa hapatoshi ni kero tupu, siku za mshahara almost zipo sawa kwa kila mtumishi wa umma ila walimu ikifika net day of salary yupo benki nadhani ni kutokana na madeni aliyonayo pamoja na ukata wa nyumbani maana hawa watu wanalisha Familia kubwa, ya kwake na ndugu zake.

Hii tabia imekuwa ikinifanya nakwazika nakuwaonea huruma pia.

Fedheha nyingine nikuwa walimu wengi wanaenda wenye hakili ndogo au waliofeli hili hata Samia alilisema zanzibar, hali hii imekuwa ikipelekea ongezeko kubwa la walimu mitaani wasionaajira bahati mbaya hawana skills zakujiajiri kutokana na low IQ waliyonayo kwahiyo matazamio yao ni kusaka huruma za watawala ili wawaajiri.

Mifano iko wazi, hizi ajira za juzi zilizotangazwa na tamisemi za afya na walimu, idadi kubwa ya walioomba ni walimu, waliomba zaidi ya laki moja wakigombania nafasi elfu tisa lakini afya hawakuzidi elfu thelasini kwa nafasi elfu saba. Hapo unaweza ukaona urahisi una gharama zake, ualimu ni ajira za watu wenye level ndogo ya uelewa darasani lakini udaktari sio program ya kitoto hiyo wanaoenda ni PCB smart hakuna matapitapi ya HKL wala wenye four za form six.

Njaa za walimu zimezidi mipaka. Kwanza hawana subira, angalia tu hizi ajira walizotoa tamisemi, walimu wanasumbua hadi aibu naona mimi, ukiingia kwenye mitandao ya kijamii wanatia huruma hadi kinyaa. Utasikia toeni pdf, mda wote utasikia toeni majina hawajui wizara Ina kazi nyingi za kufanya halafu majina yakitoka siku hiyo hiyo kero inaanza wa naanza kuuliza ajira za walimu mnatoa lini.

Mimi nadhani hii sekta ya walimu kama wizara mnaidekeza sana ndio mana mnawageuza kama cheap labor kwenye kazi za kitaifa kama sensa na uchaguzi mkuu maana mnajua wanalipika kwa pesa ya mrenda. Mbona hamuwachukui madaktari na watu wa TRA au TPDC tuone kama watakubali viajira vya sensa. Sasa mtazamo wangu walimu waanze kwenda wenye ufaulu mzuri kama kada zingine, hii itasaidia kupunguza idadi kubwa ya walimu wenye njaa njaa wanalia saaana,

Walimu waanze kupigwa interview kama kada zingine za utumishi ili kubaini vilaza na smart. Hii hali itapunguza mlundikano wa hawa watu kwenye competition za ajira. Wapigwe oral na written interview ili akili ziwakae sawa. Mbona tuliosoma kada zingine tunakaa mitaani miaka zaidi ya minne nahatusikii ajira zimetangazwa na hata zikitoka hatuanzi kero za kudai majina kwa haraka kama tunakimbizwa. Walimu hawana uvumilivu.

Sina Nia mbaya ila haya mawazo niliyotoa kama yatafanyiwa kazi basi walimu wataanza kuheshimika kama wafanyakazi wengine wa serikalini. View attachment 2271988
pamoja na kipato chao kidodgo,lakini waalimu wengi ata wakistaafu unakuta washajenga nyumba zaidi ya moja,wana mashamba na miradi midogodogo inayofanya waishi,bila kusahau wapangaji,lakini hao wanaojifanya wana fani marketable wengi wao wakistaafu wanatia huruma sana kwaajili ya bata,nakutokana style ya maisha wanawaharibu mpaka watoto wao,lakini walimu watoto wao nao wanakuja kuwasapoti,kwani mtoto wa mwlimu anafundishwa stadi za maisha,lakini hao wapiga pamba,wanawapeleka watoto wao kula bata,ni adimu sana kukuta mtoto wamwalimu ni shoga,mla unga au malaya kutokana na mkono wa chuma wa wazai wao,tukija swala la muda,mwalimu anawai kufika nyumbani kutokana na kumaliza majukumu yao mapema, pia anashindwa kwenda kula bata za gharama,ila sanasana ataingia kwenye ubanda na ka elf 5 yake na kunywa pombe za nafaka kama mbege au komoni ikiisha huyoo home,lakini hawa wapiga pamaba wanachelewa kutoka job kutokana na majukumu mengi,na akitoka hapo anaingia barna anaweza kumaliza ata lakini moja kwa siku akiwa na jamaa huku ajui kinachoendelea nyumbani,na akifanikiwa kujenga nyumba inafanyiw a finishing ya gharama mno,nje badala kupanda mbogamboga anapanda maua,kama anafuga mbwa na eni gharama sana kumtunza aisee na mara nyingi ni wachache sana wanawekeza kwenye ardhi,lakini mwalimu,nyumba yake akishapiga lip na kuezeka imeisha hiyo,mabanda ya uani kajaza mifugo,nje badala ya kupanda maua utakuta mbogamboga za kila aina....unaona buana!!!
 
kuna watu wanashangaza sana, Walimu na Madaktari wanaongoza kwenye hili, Yani wao wanafanywa kazi na kulipwa mishahar kabisa, Ila bado huwa wana demand heshima ya ziada kwa jamii. Ni wapuuzi kabisa

Kama wana hitaji kweli heshima basi hizo huduma wanazozitoa wakubali kuzitoa bila ya malipo hapo ndipo tutakapojua kama wao wapo kwa ajili ya kusaidia jamii.
 
kuna watu wanashangaza sana, Walimu na Madaktari wanaongoza kwenye hili, Yani wao wanafanywa kazi na kulipwa mishahar kabisa, Ila bado huwa wana demand heshima ya ziada kwa jamii. Ni wapuuzi kabisa

Kama wana hitaji kweli heshima basi hizo huduma wanazozitoa wakubali kuzitoa bila ya malipo hapo ndipo tutakapojua kama wao wapo kwa ajili ya kusaidia jamii.
Bora umenisaidia kuongea hili, heshima kwako
 
kuna watu wanashangaza sana, Walimu na Madaktari wanaongoza kwenye hili, Yani wao wanafanywa kazi na kulipwa mishahar kabisa, Ila bado huwa wana demand heshima ya ziada kwa jamii. Ni wapuuzi kabisa

Kama wana hitaji kweli heshima basi hizo huduma wanazozitoa wakubali kuzitoa bila ya malipo hapo ndipo tutakapojua kama wao wapo kwa ajili ya kusaidia jamii.
Anaongea mtu aliyeshindwa kulipa ada ya Sh 20k kuchangia elimu mpaka serikali ikaondoa, halafu anataka kutumia kigezo kingine mbali na pesa kutengeneza heshima kwenye mfumo wa kibepari.

Ukisikia mataifa wanapambana na Ujinga, wanamaanisha kuondoa kundi kama hili. [emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom