Ni kwanini wanasiasa wanaingilia utendaji kazi wa vyama vya wafanyakazi?

Ni kwanini wanasiasa wanaingilia utendaji kazi wa vyama vya wafanyakazi?

mmaroroi

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2008
Posts
4,635
Reaction score
2,271
CWT kama ilivyo kwa Vyama vingine vya wafanyakazi, imekuwa ikiingiliwa utendaji wake na Wanasiasa.

Je,!Sheria zinasemaje kuhusu hili? Imekuwa kawaida kushinikiza makada hasa wa CCM ndio wawe Viongozi wa vyama vya Wafanyakazi.

Ni muda muafaka sasa kwa wanasheria kuliangalia suala hili.
 
CWT kama ilivyo kwa Vyama vingine vya wafanyakazi, imekuwa ikiingiliwa utendaji wake na Wanasiasa. Je Sheria zinasemaje kuhusu hili? Imekuwa kawaida kushinikiza makada hasa wa CCM ndio wawe Viongozi wa vyama vya Wafanyakazi. Ni muda muafaka sasa kwa wanasheria kuliangalia suala hili.
Kwa sababu ualimu ni kazi yenye laana.
 
CWT kama ilivyo kwa Vyama vingine vya wafanyakazi, imekuwa ikiingiliwa utendaji wake na Wanasiasa. Je Sheria zinasemaje kuhusu hili? Imekuwa kawaida kushinikiza makada hasa wa CCM ndio wawe Viongozi wa vyama vya Wafanyakazi. Ni muda muafaka sasa kwa wanasheria kuliangalia suala hili.sawa k

Kwa sababu ualimu ni kazi yenye laana.
Siyo wanasiasa, ni serikali, baada ya kuona imevuruga mifuko ya hifadhi ya jamii, ili wafanyakazi wasiwe na nguvu ya kudai fedha zao,iliamua kuweka watu wake ili wawe viongozi ili wakubali kikokotoo!
Ni hadi siku watumishi watakapojitbua! Vya vya wafanyakazi vimetekwa na TISS, serikali inakaa mezani na watu wake kufanya maamuzi kuhusu maslahi ya watumishi!
 
CWT kama ilivyo kwa Vyama vingine vya wafanyakazi, imekuwa ikiingiliwa utendaji wake na Wanasiasa. Je Sheria zinasemaje kuhusu hili? Imekuwa kawaida kushinikiza makada hasa wa CCM ndio wawe Viongozi wa vyama vya Wafanyakazi. Ni muda muafaka sasa kwa wanasheria kuliangalia suala hili.
wanatafuta uungwaji mkono.
na ndio siasa yenyewe hiyo kuchangamana
 
Si vyama vya wafanyakazi pekee vinavyoingiliwa na dola. Dola hujipenyeza kwenye kila taasisi iwe ya michezo, sanaa, habari, asasi za kiraia n.k. hata kwenye uchaguzi wa askofu mkuu wa kanisa fulani kubwa dola lazima iingie
 
Lazima mkono wa serikali uwepo kwenye vyama vya wafanyakazi. Na hii ni karibia nchi zote zenye itikadi za kikomunisti. Lengo ni ku neutralize mambo . Kumbuka working class ni tabaka lililopo katikati baina ya rulling class na tabaka la chini. Kwa hiyo lenyewe linakuwa kama shock absorber
 
Si vyama vya wafanyakazi pekee vinavyoingiliwa na dola. Dola hujipenyeza kwenye kila taasisi iwe ya michezo, sanaa, habari, asasi za kiraia n.k. hata kwenye uchaguzi wa askofu mkuu wa kanisa fulani kubwa dola lazima iingie
Hadi TLS kipindi cha Lisu walipoamua kujivua koti la serikali kwa nguvu, serikali ikaamua kumwandalia tukio! Ila kwa vyama vya wafanyakazi, madhara yake ni makubwa sana! Bila udhaifu wa vyama vya wafanyakazi, serikali isingefikiria kuanzisha kikokotoo! Moto ungeanzia hukohuko kwenye vikao vyao!
 
Siyo wanasiasa, ni serikali, baada ya kuona imevuruga mifuko ya hifadhi ya jamii, ili wafanyakazi wasiwe na nguvu ya kudai fedha zao,iliamua kuweka watu wake ili wawe viongozi ili wakubali kikokotoo!
Ni hadi siku watumishi watakapojitbua! Vya vya wafanyakazi vimetekwa na TISS, serikali inakaa mezani na watu wake kufanya maamuzi kuhusu maslahi ya watumishi!
Ndio maana mfanyakazi akistaafu husumbuka sana kupata mafao yake. Lakini wanasiasa hulipwa haraka wanapostaafu.
 
Wanaowaingilia kimfumo ndiyo wanaowasaidia kutokuruhusu wanachama wenu kuondoka ndani ya chama chenu mpaka hivi sasa.
Chama hakina uhuru kutokana na historia ya kuanzishwa kwake.
Acha kulialia hapa kuhusu sheria wakati nyie wenyewe ni wababe wa unyonyaji na wavunjaji wa sheria nyingi za wafanyakazi.
 
Si vyama vya wafanyakazi pekee vinavyoingiliwa na dola. Dola hujipenyeza kwenye kila taasisi iwe ya michezo, sanaa, habari, asasi za kiraia n.k. hata kwenye uchaguzi wa askofu mkuu wa kanisa fulani kubwa dola lazima iingie
Hii ni ishara ya kutojiani na kutaka kuvuruga chaguzi zingine kama zinavyovurugwa chaguzi za Viongozi wa kitaifa.
 
Back
Top Bottom