Ni kweli Adam na Hawa waliishi miaka takribani 900?

Ni kweli Adam na Hawa waliishi miaka takribani 900?

Acha umbulula tafuta siri yakifo ndio uandike umbulula wako. Nia ya Mungu ilikuwa tuishi milele ila dhambi ikaleta mauti. Maisha ya binadam yamekuwa yakipungua kadri dhambi inaongezeka. Sasa hiv mwaka mmoja ni miaka mingi kuishi....
Kama dhambi walizianzisha adam na hawa kwanini wenyewe waliishi miaka 900 harafu ww uje uishi miaka 45 au 55 huo wastani wa tanzania.
Inamaa ww ulimkosea nini mungu hadi uishi miaka michache hivyo kutoka miaka 900 hadi miaka 55.
 
acha umbulula hizo ni hadithi za kusadikika.. na humohumo kwenye hizo hadithi bado kuna mapungufu..

kwa mfano mungu anamlamu binadamu kwa kula tunda, hapo anaepuka yeye kulaumiwa kwa kuweka mti wa maarifa katika bustani, sehemu ambayo ni very accessible..

hata information za serikali ambazo zipo CLASSIFIED huwa zinakuwa confidential sana na zinalindwa kwa ulinzi wa hali ya juu, mtu wa kawaida huwezi kuzi-access..

sasa watu kirahisi rahisi tu wakala matunda ya ule mti kana kwamba haukuwa na ulinzi wowote, na kwa uzito wa uwezo wa mti ule si rahisi ukae bila ulinzi, ina maana nyoka hakuyataka hayo maarifa? na angekula ingekuaje? hilo ni bumbuwazi mmepigwa.

kitu kingine cha kujiuliza, hivi mti wenye siri nzito kama ule mungu alishindwa kuuweka mbinguni mpaka akauweka duniani? mungu alikosa sehemu huko mbinguni ya kuweka huo mti ambao ni VERY SENSITIVE ISSUE?

Tuwe tunajiongeza tafadhali inatia hasira kuona watu hamfikirii..

hata babaako anakuficha vitu ambavyo vipo nje ya uwezo wako sasa huyu mungu wa biblia vipi?
Mkuu hawa watu ni tatizo.
 
inachekesha sana kumuona mfia dini anamlaani binadamu mwenzake..

hizo laana ungeanza kumlaani mwanasayansi ambae hamuamini mungu na bado akakutengenezea smartphone ili uendelee kumlaani vizuri..

hesabu wanasayansi wanalaaniwa na wakristo wangapi mpaka sasa hivi tunavyoongea, je wamerudi nyuma au wanazidi kusonga mbele? TB Joshua na flat screen zake zote zimetengenezwa na mwanasayansi ambae hamuamini mungu..

wachungaji wote wanaosafiri kwenda nchi za nje wanatumia ndege ambayo ni teknolojia ya mwanasayansi ambae haamini mungu..

YOUR WORDS ARE NONESENSE.
Hapo umewatandika za uso.
 
Lete hoja na wewe..... Sasa unafunga ili iweje
Hii inanikumbusha kuna mtu alianzisha Thread humu, kwamba haamini kama kuna Mungu... watu wengi waliishia kumnyooshea kidole kwamba hana hofu ya Mungu wengine walikemea kwamba ashindwe na alegee, walisahau kwamba kinachotakiwa ni wao kumueleza kwanini wao wanaamini Mungu yupo basi!!
 
Kwa hiyo mpango wa kula lile tunda pale bustanini edeni ulitokea kama bahati mbaya? This was planned,

This is how it was planned(mpangokazi)

Mungu kutengeneza bustani ya eden.

Mungu kamweka adam na hawa kwenye bustani.

Mungu kawaweka wanyama akiwamo nyoka katika bustani.

Mungu kaweka mti wa matunda ya uzima katikati ya bustani.

Nyoka kama mwerevu kuliko wanyama wengine katika bustani.

Nyoka kashawishi mwanamke kula tunda la mti wa kati wa bustani.

Mwanamke akampa mwanaume tuna nae, akala. Wote wakawa uchi.
Biblia ni kitabu cha hadithi
 
preach brother..

ati baada ya adam na eva kula tunda akawalaani na akawaambia hawataishi milele... kana kwamba alikua anataka mwanadamu aishi milele!!! na hata mwanadamu angeishi milele na kuendelea kuzaliana dunia ingetosha? maana hakuna ambaye angekufa.
Wakati hii dunia tukiacha kufa hata miezi 6 tu inaweza kujaa.
Na kama kungesipo kuwepo kufa inamaana hata sisi tusingekuwepo hapa.
 
Sasa inakuwaje mungu anaumba kitu ambacho kinaingiwa na tamaa harafu baadaye kinakuja kumuudhi mwenyewe.
chunguza maisha ya mwanadamu, kila changamoto tunayokutana nayo tunajaribu kuitafutia ufumbuzi na mwisho wa siku tunalipatia jibu.. kama binadamu ana utashi wa kutatua tatizo, mungu kilimshinda nini kutatua tatizo la dhambi?

kama sisi binadamu leo hii tunaambiwa tuungame ili dhambi zifutike, mungu kilimshinda nini kufuta dhambi ya adam na eva na maisha yaendelee kama kawaida?

hata mtoto akimkosea mzazi, mzazi husema nimekusamehe, USIRUDIE TENA.

yeye mungu hakusamehe, alimlaani binadamu na kumfukuza kabisa.. hivi ndivyo watu wanavyoishi? mungu gani hatoi second chance?

ina maana wanadamu tuna busara na ni waungwana kuliko mungu?
 
Mkuu usipingane na maandiko maana kuna maswal mengo unaweza ukajiuliza ukakosa majibu
 
Ahh! watu mna dhambi,yaani mama wa mungu alikua mama muuza?na mungu mwana nae alikua waiter?acha hizo bwana.

Umeyatoa wapi hayo? isije kua wewe mvinyo ndoo unaongea,maana avatar yako nayo inaweza kuwa inasadifu uloyaandika hapa.
hakuwa waiter,alikuwa akisaidia kubeba magudulia ya mvinyo toka home hadi kwenye sherehe,
in short mama alikuwa na catering service
 
Agenda kuu zilikuwa:

* Uhusiano baina ya Mungu Baba na Mungu Mwana sio tu kama Yesu aliyekuja katika mwili bali hata asili yake kabla. Walijiuliza Je Baba na Mwana ni wamoja kwa dhamira ya kimungu tu ama wao ni wamoja katika asili yao pia? Hili lilikuwa suala lililoibuliwa na Wakristo wa madhehebu ya ARIAN waliohoji juu uungu wa Yesu baina ya mambo mengine yaliyohusika.

Mkutano wa Nikea wa kwanza, ulitoa fasili ya kile kanisa linachokiamini juu ya Uungu wake Mungu. Kikao kiliweka mkazo kwa Wakristo kuamini katika Utatu Mtakatifu. Ulithbitisha kuwa Mungu Baba, Yesu Kristo na Roho Mtakatifu ni sehemu ya kitu kimoja. Japo wapo pekee wao watatu ni wamoja. Nimehitimisha.
angalau wewe kidogo sio mahututi kwa kujua kuwa yesu roho mt. na mungu baba ni miili mitatu tofauti, ila umungu wao mmoja upo katika dhamira.

kuna mwehu humu alisema mungu umbile analo, na umbile lake ni yesu!!! yani huo utatu mtakatifu bado ni bumbuwazi kwa wakristo..

kama nikisema niwakusanye wakristo niwape makaratasi kila mmoja anichoree picha ya mungu iliyopo kichwani mwake, na azionyeshe hizo nafsi tatu, watu watachora mambo ya ajabu sana.

ila ukumbuke hayo maamuzi ya utatu mtakatifu ni watu tu walikusanyika na kuamua kuutengeneza huo utatu mtakatifu na kuonekana kitu halali.
 
Mungu na shetani wanafahamiana.

Mungu ni mfalme wa mbinguni wakati shetani ni mfalme wa ulimwengu.

Wote wana maeneo tofauti ya kiutawala, pia hata utendaji.
lakini kwa mjibu wa biblia hawa hutembeleana,
shetani humtembelea mungu wakaongea na pia mungu humtembelea shetani,mfano pale bustan ya eden ,mungu alikuja ulimwenguni personaly na akawa anazunguka zunguka bustanini akiwatafuta kina adamu na hawa
 
lakini kwa mjibu wa biblia hawa hutembeleana,
shetani humtembelea mungu wakaongea na pia mungu humtembelea shetani,mfano pale bustan ya eden ,mungu alikuja ulimwenguni personaly na akawa anazunguka zunguka bustanini akiwatafuta kina adamu na hawa
na we unaamini kabisa mungu alikua anawatafuta? wakati biblia hio hio inakwambia hakuna jambo ulifanyalo mungu asilijue? sasa kama anajua kila nifanyalo manake anajua nipo wapi mda wote...

yani kama namuona bibi vile anavyonihadithia hii hadithi, halafu naitikia enhe.
 
Lakini ubishi wako utakufikisha mahala ambapo sipo. Enzi za Lutu na Nuhu Mungu alionyesha mpambano kwa mwanadamu lakini baadae akasema sitabishana na mwanadamu tena. Rejea maandiko Mwanzo 6:3. Na hapo ndipo aliposema umri huyu mwanadamu utakuwa miaka 120 badala ya ile ya wakati wa akina Nuhu
 
Kwani huwaoni mtaani kwako wazee wenye miaka mia na zaidi? Kwa mfano Mungu akaamua vijana wa sasa waishie miaka 20 harafu wakaja kuambiwa mababu zenu waliishi miaka mia bado hutaamini?
 
Kwani huwaoni mtaani kwako wazee wenye miaka mia na zaidi? Kwa mfano Mungu akaamua vijana wa sasa waishie miaka 20 harafu wakaja kuambiwa mababu zenu waliishi miaka mia bado hutaamini?
Hata saizi wapo wanaozaliwa na kufa siku hiyo hiyo. na wengine wanakufa hata kabla hawajazaliwa. inamaana na hao ni mungu anapanga?
 
Hata saizi wapo wanaozaliwa na kufa siku hiyo hiyo. na wengine wanakufa hata kabla hawajazaliwa. inamaana na hao ni mungu anapanga?
Mambo ya Mungu hayachunguziki ndugu yangu.. Maana biblia inasema hekima ya mwanadamu kwa Mungu ni upumbavu
 
Lakini ubishi wako utakufikisha mahala ambapo sipo. Enzi za Lutu na Nuhu Mungu alionyesha mpambano kwa mwanadamu lakini baadae akasema sitabishana na mwanadamu tena. Rejea maandiko Mwanzo 6:3. Na hapo ndipo aliposema umri huyu mwanadamu utakuwa miaka 120 badala ya ile ya wakati wa akina Nuhu
unaweza kunipa kipengele kinachozungumzia huo mpambano?
 
ww usirudie.tena kusema.biblia.ina uongo acha kukashifu utalaanika kile ni.kitabu kitakatifu take care kama uamin bible. be calm

Mbona matishio sana?...Huku ni kujengea watu hofu,na msingi wa imani uliojengeka kwenye hofu ni mufilisi,ni ya uongo...

Kwanini bible tu na kuna vitabu kibao vya dini mbalimbali kila mmoja ana-claim ni vitabu vitakatifu?Sijui unaweza ni prove uo "utakatifu" umetoka wapi?Mungu hajawahi andika kitabu,hana haja hiyo,ana uwezo wote,anaweza kutuingizia anachokitaka kwenye bongo zetu bila kuhitaji msaada wa mtu amsaidie kuandika,watu waende shule waje wasome ndio waokoke kwenye mbinguni,ukishindwa kusoma au kama huna akili kiasi hicho unaenda motoni,nonsense
 
Back
Top Bottom