Zee la madawa
JF-Expert Member
- Nov 28, 2022
- 1,895
- 4,478
Mdau ametufata inbox na kutoa dukuduku lake kama ifuatavyo:-
"Tamthilia ya Kituruki Ottoman, ambayo inaoneshwa kupitia Az@m Media, imekuwa gumzo kubwa miongoni mwa watazamaji wengi nchini Tanzania.
Licha ya kuvutia kwa hadithi yake ya kihistoria, baadhi ya watu wameanza kuhoji maudhui yake na ujumbe unaopitishwa.
Katika tamthilia hiyo, inaonekana wazi kuwa kuna mapambano kati ya Waislamu wakiongozwa na Othman na Wakristo wanaowakilishwa kama Waroma. Mapigano haya yanaoneshwa kuwa ni kwa ajili ya kusimika dini ya Uislamu, na katika kila pambano, upande wa Waislamu huonekana kushinda.
Wakati wa ushindi, mara nyingi husikika kauli kama “Allahu Akbar,” huku upande unaoshindwa ukiwasilishwa kwa alama za Kikristo kama misalaba na mavazi yenye maandishi ya Roma. Hali hii imeibua tafsiri kwa baadhi ya watazamaji kuwa kuna ujumbe unaolenga kuonyesha ubora wa dini moja dhidi ya nyingine.
Mbali na hilo, kumekuwa na maswali kuhusu tafsiri ya tamthilia mbalimbali zinazooneshwa. Watazamaji wengine wanasema kuwa hata filamu ambazo si za Kiislamu, tafsiri zake huingiza maneno kama “Assalamu Aleikum” au “Allah,” jambo ambalo linaongeza hisia za mwelekeo wa kidini kwenye maudhui yasiyokuwa ya asili hiyo.
Kutokana na hali hii, baadhi ya watu wangu tunajiuliza:
Je, huu ni mkakati wa makusudi wa kuingiza propaganda ya kidini kupitia burudani?
Aidha, hoja nyingine inayojitokeza ni kuhusu uwiano katika nafasi za kazi ndani ya vyombo vya habari, ambapo tunahisi kuna upendeleo wa kidini unaoweza kuonekana au kuhisiwa"
MDAU AKAMALIZA HIVYO
(MAONI YETU SISI KAMA @JAMIIDIARY)
Ni muhimu kutambua kuwa tamthilia kama Ottoman ni kazi ya kihistoria inayotokana na utamaduni na historia ya Uturuki, ambapo Uislamu ulikuwa sehemu kubwa ya dola hiyo. Hivyo, baadhi ya maudhui yanaweza kuwa yanaakisi historia badala ya kudhani ni kampeni ya moja kwa moja ya kidini.
Kuhusu swala la uwiano wa kazi/ajira kwa kigezo cha dini sio swala la kujadili kwa kuwa tunaamini medias wanaajiri watu kutokana na CV au weledi.
USHAURI: Ni jukumu la vyombo vya habari kuhakikisha maudhui yanatolewa kwa uwiano, lakini pia watazamaji wanapaswa kuwa makini katika kutafsiri kile wanachokiona.