Ni kweli filamu ya Ottoman inaoneshwa Azam tv ili kuudhalilisha ukristo?

Mlaumu babu yenu wa Taifa Laanatullahi Nyerere kwa kuivamia Zanzibar na kutaka kuufuta uislamu kwa maagizo ya kanisa lako la kikatoliki
Hizo ni akili fupi sana , BBC wanaonyesha mpaka historia ya Yesu na Ukristo , angalia hapa kama utapenda kufuatilia ukweli


View: https://www.youtube.com/watch?v=OnNBLLcN-fY
 
Haya ni mambo ya kale,hivi ndivyo ilivyokuwa,hakuna haja ya kuumiza kichwaa.Enjoy the show enjoy the Moment.
It is part of past history.
Nadhani Ottoman inaonesha historia ya kuisimika dola ya ottoman kama dola yenye nguvu kubwa zaidi baada ya kuanguka kwa dola ya kirumi.

Na hizo zilikuwa ni holly wars za kusilimisha wakristu katika uislamu. Ila ukiangalia hii tamthilia ipo biased lakini pia walioitafsiri, wamejitahidi kuifanya iwe soft tofauti na ukisoma subtitles zake za Kiingereza

Hata hivyo hainisumbui japo Kwa concerns za watu ni kweli. Ni kama Azam alivyozileta tamthilia za turkey, lebanon na nyingine za nchi za kiarabu kwa sababu zina mifumo ya kiislamu japo ni kawaida tu maana tumekuwa tunaangalia telenovela zenye mifumo ya kikristu pia. Kwa hiyo ukiangalia kawaida hautokusumbua, ila ukiangalia kwa leni ya udini. Utapata udini. Chaguo ni lako
 
Wanao weza kuudhalilisha ukristo ni wakristo wenyewe, Wanao weza kuudhalilisha uisilamu ni waisilamu wenyewe.


Nje ya hapo ni kujitekenya na kucheka mwenyewe.
 
Ndio kuna viashiria vya kueneza udini kupitia hiyo tamthilia. Kwangu nilishapiga mafuruku kuangalia ikifika saa nne its either waangalie channel nyingine au wazime.

Nashukuru wote wameelewa ikishafika tu wanachange kwingine hata wao hawapendi sikuhizi.
 

Mm ndo leo nimejua kama kuna wakrisyo na waisilamu mule, japo hua naangaliaga vipande vichache nikikuta familia inaangalia.

Ukiona mtu kaona udini kwenye ile tamthilia kiasi cha kulalamika, ujue na yeye ni mdini.
 
Mm ndo leo nimejua kama kuna wakrisyo na waisilamu mule, japo hua naangaliaga vipande vichache nikikuta familia inaangalia.

Ukiona mtu kaona udini kwenye ile tamthilia kiasi cha kulalamika, ujue na yeye ni mdini.
Uwezi kujua kirahisi kwa sababu walioitafsiri, wameipooza. Mfano watasema "mwenyezi Mungu ni mkubwa " Badala ya Allahu Akbar,
Ama wazushi badala ya "Kaffirs"..

Kuna siku niliangalia ndio ikaonesha wazi vitu kama mkufu kama rosary na ishara za msalaba. Kuangalia subtitles nikaielewa

Japo toka mwanza nilijua Ottoman ilikuwa ni dola iliyotawala baada ya kuanguka kwa dola ya kirumi. Na hii pia ilichangia kusimika uislam huo ukanda.
 
Nchi inapotoka hiyo hiyo filamu ni ya kiislamu.

Channel azam tv ni ya kiislamu.

Huwezi kuitenganisha azam tv na uislamu.
 

labda hakuwa (Nyerere ) na jinsi, kuna mambo mengi tu hatuyafahamu lkn nielewavyo zanzibar ni mali ya english monarchy, na aliyejenga Kanisa la Kristo Zanzibar siyo Nyerere peace be upon him bali ni english monarchy hivyo peleka lawama kunakohusika, btw kwa nini sultani wenu alikimbilia uingereza na siyo kwao arabian desert?

Kanisa la Kristo zanzibar ...
 
Huna akili na tamthiria za namna hiyo zimeanza kurushwa na Azam tangu mwaka 2016 tangu magifuri yuko madarakani.
Filam zinazo onesha waisilam kama magaidi mbona hujawahi kulalamika zipingwe marufuku?
 
Sasa mkuu wapunguza vipi ukali wa maneno hali ya kuwa ndo tafisri ya maneno hayo?
Kwani kuna tafisri nyingine ya alaah akbar zaidi ya mungu mkubwa au kuna tafsiri nyingine ya kafri zaidi ya mkanushaji ?
 
Kuna vyombo vya habari vilivyosajiliwa moja kwa moja kama vya taasisi za kidini, lakini kuna vyombo vinasajiliwa kuwa siyo vya taasisi za dini ila vinaweza kuwa na muegemeo wa kidini.

Uamuzi ni wa kwako mtazamaji au msikilizaji. Kama mtazamaji umejiridhisha kuwa Azam TV ina muegemeo wa kidini, na muegemeo huo ni kikwazo kwako, achana nayo. Unaweza kuchukua king'amuzi cha DSTV, hutapungukiwa na chochote.

Hii ni sawa, na wale wanywaji wa pombe, ukiona pombe inakuwa ni kikwazo kwako katika kuyaishi maadili unayoyataka, achana nayo.

Na hiyo, ndiyo tafsiri ya lile andiko la kwenye biblia kuwa mkono wako ukikukosesha, uukate, jicho lako likikukosesha ling'oe. Mkono au jicho la kukukosesha, ni kitu chochote unachokiona ni kikwazo kwako katika kuyaishi maadili ya imani yako.

Kama wazazi ni muhimu sana kuhakikisha wanafamilia wako, na hasa watoto, wanaangalia na kusikiliza mambo yanayowajenga katika maadili ya kiimani. Kama utaona tamthiliya za Azam TV zinapotosha maadili yao ya kiimani, ni jukumu lako wewe mzazi kuwazuia kuitazama hiyo channel au kubadilisha kabisa king'amuzi. Watoto wasitazame chochote kinachoweza kuja kuwajengea chuki dhidi ya jamii yoyote ile. Ukristo ni upendo kwa wote. Tamthiliya zinazotengenezwa kwaajili ya kuchochea chuki miongoni mwa mwa makundi ya wanadamu, ni kinyume cha ukristo wa kweli.
 
Unataka kusema na movie za Hollywood zinaudhalilisha Uislamu kwenye scene zao nyingi zinazoonesha wao ni magaidi?!

Furahia mapigano, sio kila kitu uwe na deep thinking mkuu..!
 
Filamu za jinsi hiyo ni

Kuhusu Zanzibar ni swala la muda tu watalia na kusaga meno
 
MALCOM LUMUMBA hapa kuna jambo tunaomba ungetuandalia uzi utuelezee vizuri maana baadhi ya mabaazazi na madunya kuna vitu hawaelewi

Hio vita ni ya kweli na mimi niliwahi msikia Askofu wa Kanisa akiielezea tena yeye aliielezea vizuri zaidi na kweli hio vita Wakristo walifeli yaan walipigwa, sio kwamba inataka kufanya nini lakini pia ipo vita ambayo Waislamu walipigwa na Wakristo ni zamani hizo hayo ni mambo ya historia tu

Ila kwenye kusimulia kuna kitu kimoja nilijifunza kutoka kwa Waislamu baada ya hio vita kuisha na baada ya Wakristo kushindwa vita kuna jambo moja la kibinadamu ambalo Waislamu walilifanya, sitolitaja hapa

Pia kuna Mzee mmoja sina jina lake alikua anahojiwa kupitia hio hio Azam nae alielezea vizuri sana kuhusu hio vita kwa hio sio simulizi za kutunga ni historia ya kweli iliyowahi kutokea kabla na haipo kwa lengo la kufanya hivyo watu wanafikiri inataka kufanya sio kweli
 
Nadhan WATU kutokujua historia ya Dunia ndyo wanateseka sana

Hiz dola zilitamba Kila Moja kwa nyakat tofaut

Roman empire

Ottoman empire
Mongolian

Hiz dola tatu zilitamba na kupambana zenyewe kwa zenyewe ili kuitawala Dunia

Sasa kwa vile WATU tumeweka dini mbele tunashindwa kujua historia

Kuna mmoja humu kuna bas Toka kigoma limeandikwa TAKBIR akaanza kuliponda bas kwa mlengi wa dini badala ya huduma zitolewazo kama chombo cha usafir

ELIMU ELIMU elimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…