Sitaki kuandika mengi, tutakwenda kwa lugha ya Picha tu, tuwe makini na watu, ukione Picha kama hizi usitamani haya maisha utapelekwa shimoni.
Nilikuwa na conversation ya kuboost biashara zangu na jamaa Fulani ambaye tumefahiana kama mwaka sasa, nikashauriwa nitambulishwe kwenye brotherhood, kwanza Mimi ukiniambia tu neno brotherhood moja kwa moja nakumbuka filamu ya Nigeria Billionaires club ya Pete Edochie na Madon wenzake.
Nina story ndefu na ya kweli ila nawashauri wote tupambane na umaskini tuvumilie shida zina mwisho Mungu atatufanyia wepesi, hawa jamaa mwisho wa siku huwa wanataka kafara ya damu.