DOKEZO Ni kweli hali ya upatikanaji huduma ya maji ni mbaya kiasi hiki? Wizara ya Maji tuambieni ukweli wa video hii

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Precious Diamond

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
593
Reaction score
1,376
Salaam Wakuu,

Kuna video itambea sasa hivi ikionesha kiwango cha maji kuwa chini sana kuliko kawaida! Nina imani hili limeshawafikia Wizara ya Maji, DAWASA, ukweli ni upi? Hii ndio hali halisi ya kina cha maji sasa?

Ni bora tukaambiwa ukweli ili tuwe na mkakati haraka wa jinsi ya kukabiliana na hali hii. Maana mtaani majibu ni yale yale lakini huduma inazidi kuzorota kadri siku zinavyoenda!

aisee mtaan maji hamna sina nguo safi sina maji ata ya kwenda kuogea
 
Saudi Arabia na Qatar sehemu kubwa ya nchi hizi ni kame lakini hakuna uhaba maji.
 
Wizara imeshashindwa kazi, kuna siku nimemtembelea jamaa mmoja huko dar, chamazi kama sikosei
Hakuna maji ya idara husika, mtu mmoja anauza maji kwa raia, msela akikosa umeme maji hakuna
Akichafukwa maji hakuna
Ni aibu kwa jiji kama la dar kukosa maji ya uhakika miaka yote tangu mkoloni kuachia nchi, na kuna bahari 🙄
Ngozi nyeusi tuna shida,
Tamaa
Ubinafsi
Salaam Wakuu,

Kuna video itambea sasa hivi ikionesha kiwango cha maji kuwa chini sana kuliko kawaida! Nina imani hili limeshawafikia Wizara ya Maji, DAWASA, ukweli ni upi? Hii ndio hali halisi ya kina cha maji sasa?

Ni bora tukaambiwa ukweli ili tuwe na mkakati haraka wa jinsi ya kukabiliana na hali hii. Maana mtaani majibu ni yale yale lakini huduma inazidi kuzorota kadri siku zinavyoenda!

Salaam Wakuu,

Kuna video itambea sasa hivi ikionesha kiwango cha maji kuwa chini sana kuliko kawaida! Nina imani hili limeshawafikia Wizara ya Maji, DAWASA, ukweli ni upi? Hii ndio hali halisi ya kina cha maji sasa?

Ni bora tukaambiwa ukweli ili tuwe na mkakati haraka wa jinsi ya kukabiliana na hali hii. Maana mtaani majibu ni yale yale lakini huduma inazidi kuzorota kadri siku zinavyoenda!

Unaweza shangaa akajibu kafulila atakwambia mendeleo na takwimu zake kama kawaida yake.
 
Watu wa wilaya ya Ubungo Dar es salaam tulishazoea kabisa shida ya maji maana tumesema sana lakini hakuna anayetusikiliza .Ubungo hakuna kabisa maji ya dawasa zaidi tunaona waziri wa maji anakata mauno mbele ya bosi wake na kubadili mara Kwa mara V8GXR za milioni mia sita
 
Ajabu ni kuwa hata sie tuliopo kando ya ziwa nyanza tuna uhaba wa maji licha ya kuona ziwa lile pale
 
Sijajua hiyo video ni ya lini, ila nafahamu Kwa nyakati hizi za mvua hata ukipita hapo Ruvu utaona Maji ni mengi

Pamoja na kutokufahamu ukweli wa hiyo video, ila Maji Kwa Jiji la DSM ni changamoto sana, ndiyo maana Serikali imeamua kutumia zaidi ya bilioni 300 kujenga Bwawa la Maji Kidunda Mkoani Morogoro kwaajili ya kuleta Maji DSM.

Inawezekana ikawa ni project ya muda mrefu, lakini inaweza kusaidia kupunguza kama sio kuondoa tatizo la Maji.

Kupitia taarifa za Serikali, kuanzia Mwaka 2021 zilionesha Maji ya Chini ya Ardhi nayo yameanza kupungua kutokana na uharibifu wa Mazingira.

Ndiyo maana hata hali ya Joto imeongezeka miaka ya karibuni
 
Unasubiri uambiwe nini???!! Ninapoishi maji yanatoka mara mbili kwa wiki J3 & J4, hali ni mbaya. Kama unasubiri wizara au DAWA wakupi majibu endelea kusubiri.
 
Salaam Wakuu,

Kuna video itambea sasa hivi ikionesha kiwango cha maji kuwa chini sana kuliko kawaida! Nina imani hili limeshawafikia Wizara ya Maji, DAWASA, ukweli ni upi? Hii ndio hali halisi ya kina cha maji sasa?

Ni bora tukaambiwa ukweli ili tuwe na mkakati haraka wa jinsi ya kukabiliana na hali hii. Maana mtaani majibu ni yale yale lakini huduma inazidi kuzorota kadri siku zinavyoenda!

Inategemea unaishi wapi, kuna mahali maji yako kila leo, miaka nenda irudi
 
Mpaka yanafikia level hiyo wahusika walikuwa wapi? walichukua hatua gani? au ni yaleyale bora liende!
 
Wizara imeshashindwa kazi, kuna siku nimemtembelea jamaa mmoja huko dar, chamazi kama sikosei
Hakuna maji ya idara husika, mtu mmoja anauza maji kwa raia, msela akikosa umeme maji hakuna
Akichafukwa maji hakuna

Ni aibu kwa jiji kama la dar kukosa maji ya uhakika miaka yote tangu mkoloni kuachia nchi, na kuna bahari 🙄
Ngozi nyeusi tuna shida,
Tamaa
Ubinafsi
Unakuta huyo mtu mmoja sio mmoja kama unavyomuona, unakuta ni syndicate ya watu hata 10 wakiwemo maafisa wa DAWASA, wanatengeneza tatizo la maji kwa makusudi(sababu hakuna ufuatiliaji) hili wapige hela kwa kuwauzia maji raia hapo mtaani.

Huu mkoa na mamlaka zake ni wa ovyo sana..

Ukitoka kuona hilo tatizo la maji ni bandia, subiri wakati wa masika maji huwa yanatoka hata mwezi mzima mfululizo na hakuna cha kuharibika miundo mbinu wala nini.

Ovyo sana hii nchi.
 
kwani wakati mradi ule wa kigamboni unazinduliwa si walisema yatasaidia kupunguza uhaba wa maji dar es salaam?
 
Inategemea unaishi wapi, kuna mahali maji yako kila leo, miaka nenda irudi
Labda kama ni kwa 'waheshimiwa' wenyewe, sehemu kibao hakuna maji, si Dar wala mikoa mingine, ni vilio tu... kuna kitu hakipo sawa
 
Back
Top Bottom