Nikianza kuelezea hata sitamaliza [emoji2962].
Upendo wa Mungu umekuwa tiba. Amani niliyonayo si ya ulimwengu huu, hata ingekuwa yauzwa nisingeweza pata ya hii grade.
Biblia inasema 'Amani yangu nawapa. Amani hii si kama ulimwengu utoavyo' - (Agano jipya, sikumbuki ni kitabu au mistari ipi exactly)
Kuwezeshwa.
Neno la Mungu linasema 'Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu' - Filipi 4:13
Amekuwa uwezo wangu kwenye maeneo yote. Hata ambayo ungeshindwa kujua ufanyeje, ukisema 'Bwana Yesu naomba hekima katika haya', unapata jinsi ya kuhandle swala na likaisha vizuri. Hapo sijagusia uongozi bombastic wa Roho Mtakatifu, unaotupa hatua za kuchukua kwa kila tulifanyalo.
Ulinzi.
Neno la Mungu linasema 'Malaika wa Bwana hufanya kituo kuwazungukia wamchao na kuwaokoa' Zaburi 32:7
Aisee... Ungejua mara ambazo Roho wa Mungu huzungumza nasi (familia yetu) kututahadharisha na vifo, ugonjwa na hali sizizofaa...ungeona hichi ni kitu gani. Uwepo wa Ulinzi wa Mungu ni pamoja na kushtuliwa: Usiende hapa, pita hivi, acha huyu usieke ukaribu na mengineyo. (Vilevile Roho huwa nasi kutuambia tuombe vipi, kufikia lengo fulani).