Ni kweli Kanisa Katoliki wanatunza akiba ya fedha kutekeleza Sheria ya Jumapili?

Ni kweli Kanisa Katoliki wanatunza akiba ya fedha kutekeleza Sheria ya Jumapili?

Wasabato ndio waliomuua Yesu
Wakasema anavunja sabato
Wakasema anafanya kazi siku ya sabato
Wakamuua ijumaa halafu wakasema tutapumzika jumamosi bila Yesu
Kama Yesu alifufuka jumapili
Basi siku hiyo inafaa kukumbukwa zaidi maana ndiyo siku ya sabato(Yesu) kutupumzisha

Kwahiyo kama wasabato walimuua Yesu nadhani wao ndio wataleta Saturday law kutuua waabudu jpili tuliosalia(japokuwa Mungu tunamuabudu rohoni kila siku)
Unajibu kwa hisia au maandiko
 
Hivi bifu la SDA na RC lilianzaje? SDA wenye waumini 20m wanawezaje kupambana na RC yenye waumini 1.4b? Dunia ina watu 7b ambao ni 7000m. Ina maana Mungu atachoma viumbe wake 6980m kisa hawaabudi jumamosi kwenye makanisa ya SDA? Kama Mungu atachujua hayo maamuzi ina maana Kiranga atakuwa yuko sahihi.
 
Ipo nje ya mada kidogo

Kuna padre mmoja alishikwa na kasidemu kimoja hivi kilikua kinamfanyia usafi na kumpikia na Mambo mengine alikua ni mzungu Mzee

Demu alijenga bar, nyumba na akanunua Hadi gari haieleweki yule demu alimuwekea nini yule padre au alikua anampa Nini

Ni kwamba yule demu alikua akikohoa anashida na Pesa au sometimes alikua anajifanya anaumwa amelazwa padre anapigiwa simu Lazima atatuma Pesa t sijui yule manzi alimfanyia Nini yule padre na manzi mwenyewe alikua malaya wa kutupwa
Malaya ndio wanajua mambo mkuu...wanakuchanganyia ladha
 
Madai ya rafikiyangu msabato kuwa Kanisa Katoliki wanatunza akiba ya Fedha kutekeleza sheria ya jumapili yana ukweli? Wadau hamjamboni nyote?

Ni Madai ya rafiki yangu mmoja wa kisabato kuhusu maandalizi yanayofanywa na kanisa Katoliki kuelekea utekelezaji wa sheria ya jumapili - Sunday Law

Anadai kwamba Kanisa hilo limepunguza misaada kwa makanisa yake mbalimbali duniani. Kwamba huo ni mpango mkakati kuweka akiba ya kutosha. Kwamba linaweka akiba siyo kwakuwa limeishiwa Fedha ila ni mpango mkakati kuelekea utekelezaji wa amri ya jumapili

Kwamba Fedha husika pamoja na rasilimali nyinginezo zitatumika kuwashughulikia kikamilifu watakaopinga amri ya kuabudu jumapili yaani Sunday Law. Kwamba walengwa wakuu wa sheria hiyo ya Jumapili itakayotungwa na Catholic Kwa kishirikina na Marekani na Umoja wa Mataifa ni Wasabato ambao wanaabudu siku ya jumamosi.

Nimeshindwa kuelewa, kuamini na nimeshangaa sana huku nikikosa hata swali la kumuuliza.

Kwamba baada ya mateso hayo kupitia ndiyo Yesu Kristo atarejea na kuwachukua kwenda mbinguni.

Naombeni maoni yenu wasomi wa theolojia.

Karibuni.
Kwakuwa umesema uliambiwa na rafiki yako Msabato yatosha kuishia hapo,siongezi neno!!!
 
Sio Kweli!!!
1. Kwa miaka zaidi ya 100 Kanisa Katoliki Afrika na America kusini,India n.k Walikuwa wanategemea misaada toka kwa waamini wa nchi za Ulaya- hii imekuja kubadilika kutokana na Ukatoliki kupunguwa Huko Ulaya na hivyo misaada hiyo aipo tena.Kuna Nchi Makanisa yamegeuzwa Clubs, Makumbusho au majengo kwa kazi zingine.. Vijana wengi Ulaya awana time na Dini.
2. Kanisa Katoliki alina mpango wala alifikirii kutwaa Dola yeyote ile katika Dunia hii na wala aina Nia ya kufuta Usabato,Ulokole au Ukristu wowote ule-Bibilia ya Leo inayotumika na Wakristo wote ikiwemo wakatoliki na Wasabato imetokana Na Wakatoliki.Kanisa Katoliki lina hazina kubwa ya Maandiko na Vitabu zaidi ya milioni moja huko kwenye Hifadhi Vatican-Wasabato na madheebu mengi ya Kikristo yana shambulia sana Kanisa Katoliki- lakini Katoliki alina Muda wa malumbano au kujitangaza kama madheebu mengine. Wasabato wao waendelee tu na Mafundisho yao na wapambane na hali yao.. Picha- vitabu na nyaraka katika maktaba ya Vatican .Vitabu vingine vina zaidi ya miaka 2000
 
Attachments

  • IMG_1647.png
    IMG_1647.png
    103.1 KB · Views: 7
  • IMG_1650.png
    IMG_1650.png
    101.4 KB · Views: 5
  • IMG_1649.png
    IMG_1649.png
    105.5 KB · Views: 5
  • IMG_1648.png
    IMG_1648.png
    112.3 KB · Views: 8
  • IMG_1651.png
    IMG_1651.png
    88.4 KB · Views: 8
  • IMG_1652.jpeg
    IMG_1652.jpeg
    33.9 KB · Views: 4
  • IMG_1653.jpeg
    IMG_1653.jpeg
    30.7 KB · Views: 6
Hivi bifu la SDA na RC lilianzaje? SDA wenye waumini 20m wanawezaje kupambana na RC yenye waumini 1.4b? Dunia ina watu 7b ambao ni 7000m. Ina maana Mungu atachoma viumbe wake 6980m kisa hawaabudi jumamosi kwenye makanisa ya SDA? Kama Mungu atachujua hayo maamuzi ina maana Kiranga atakuwa yuko sahihi.
Hakuna Mungu.

Hizo zote ni siasa za watu tu wakipigana na hali zao.
 
Huyo muongo. Si lazima tuwe na siku moja special ya kusali. Unaweza kufanya ibadan siku yoyote au kila siku.
Haya mawazo yako ni akili za binadamu sio agizo la Mungu
Mungu amewaagiza waadamu wote waabudu na wapumzike siku ya 7 akaliita sabato
Kati ya amri 10 za Mungu sabato ni amri ya 4 soma kutoka 20
Hivyo hauwezi kwenda mbjnguni bila kuamini sheria 10 za Mungu ikiwemo na Sabato hivyo ni hitaji la agizo la Mungu kila mwanadmu awe pia msabato
 
Hao wasabato na hao waroma wote wapumbavu tu, kwa dunia hii ya leo yenye uhuru na haki ya kuabudu unachokitaka watamlazimisha nani afuate sheria fulani?

Sio wafuasi wa ukatolic tu hata wasio amini hiyo imani hakuna anayeweza kulazimishwa kuamini jambo analotaka mwengine, bahati mbaya wafia dini ni vilaza hawajiulizi haya mambo, dunia ya leo si ile ya miaka ya mababu walioendeshwa kifala kulazimishwa kuamini jambo fulani, leo hii hata zitumike sheria ngumu binadamu bado hawatozifuata.

Acheni kuamini uzushi, hao wakatolic na hao mnaowapa airtime za kijinga hawana hiyo nguvu ya kuamrisha watu wafanye nini, labda kwa waumini wao.

Hata hiyo sunday's law sijui takataka gani hawajaanza kuifanyia kazi leo wala jana bali muda mrefu wamekuwa wakiitumia lakini mambo yao yalibuma, walishajaribu muda mrefu kutaka kuicontrol dunia kupitia sheria zao za kipuuzi za kidini na kisiasa lkn hakuna lililofanikiwa,

kama kipindi cha ujinga na upumbavu wa miaka ya nyuma walishindwa kuitekeleza hiyo NEW WORLD ORDER basi kwa kizazi hiki cha ustaarabu, haki na uhuru hakuna watakaloliweza, acheni uoga na hayo mafundisho ya wachungaji wenu wanaowatishatisha, dunia haina mwisho, haitoisha leo wala kesho, hata hao mnaowaogopa kuwa wataitawala dunia bado hawajafikia nguvu hizo, ndio kwanza wanazidi kupoteza ushawishi katika jamii, ndiomaana wamebaki kueneza vitisho na propaganda kupitia vilaza wao ambao baadhi ni hao manabii wenu, wachungaji wenu na hata viongozi wakuu kutoka kanisa la sabato wako chini ya hao hao waliotunga hizi dini.
 
Hao Wasabato ndio waliotaka kusafiri kwenda ulaya bila passpport,viza wala tiketi ya ndege.
Akili zao zipo chini ya makalio yao(sorry for this)
 
Walikuwa na radio Marekani inaitwa Family Radio ilikuwa inatangaza kupitia masafa mafupi.
Ukisikiliza hiyo radio unaweza kuuza mali zako maana walikuwa wanakuja na ushahidi wa kuokoteza kwamba mwaka 2009 ni mwisho wa dunia.
Kuna mtangazaji alipostaafu VOA ndio akahamia huko kazi kututisha tu.
 
Haya mawazo yako ni akili za binadamu sio agizo la Mungu
Mungu amewaagiza waadamu wote waabudu na wapumzike siku ya 7 akaliita sabato
Kati ya amri 10 za Mungu sabato ni amri ya 4 soma kutoka 20
Hivyo hauwezi kwenda mbjnguni bila kuamini sheria 10 za Mungu ikiwemo na Sabato hivyo ni hitaji la agizo la Mungu kila mwanadmu awe pia msabato
Huwezi kwenda mbinguni kwa sababu kuu moja: USIPOMKIRI, KUMWAMINI NA KUMPOKEA BWANA YESU KRISTO KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO.

“Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
” Yohana 14:6

Yohana 5
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁶ Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwudhi Yesu, kwa kuwa alitenda hayo siku ya sabato.
¹⁷ Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi.
¹⁸ Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na hayo alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu. Basi Yesu akajibu, akawaambia, Amin, amin, nawaambia,
¹⁹ Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile.
 
Inamaana hiyo biblia hamjasoma maagizo kuhusu Amri za Mungu?
Ziko 10 ambazo ni usiue usizini usiseme uongo kumba siku ya sabato
Neno linasema ukivunja 1 umevunja yote
Yesu alitunza sabato Mungu kwenye uumbaji alifanya sabato kama pumziko.
Sasa maana ya kumwamini yesu ni kukubali ukombozi wake na kuamini ktk tabia yake
Sasa unataka umwaimini Yesu kisha uendelee na dhambi? Nakuambia wadhambi hawaingii Mbinguni ni wadhambi ni waliovunja amri za Mungu maana Mbinguni ibada ni Sabato

Sasa wewe bushana na Amri za Mungu mwisho utakuja kuwa kuni katika moto maana hata usiwe msabato wasabato wapo yaani kanisa la Musa la mitume la Mungu
 
Wasabato adui yao mkubwa sio Shetani bali ni Wakatoliki😆😆.Sijawahi kuona Wasabato wanashambulia mafundisho ya madhehebu mengine kwamfano Lutheran,Anglican,Assemblies of God,Moravian wao kila siku ni kuwapinga Wakatoliki tu🤣🤣
 
Haya mawazo yako ni akili za binadamu sio agizo la Mungu
Mungu amewaagiza waadamu wote waabudu na wapumzike siku ya 7 akaliita sabato
Kati ya amri 10 za Mungu sabato ni amri ya 4 soma kutoka 20
Hivyo hauwezi kwenda mbjnguni bila kuamini sheria 10 za Mungu ikiwemo na Sabato hivyo ni hitaji la agizo la Mungu kila mwanadmu awe pia msabato
Naona umefika mkuu
Kuna watu wanapinga sabato huku
 
Wasabato adui yao mkubwa sio Shetani bali ni Wakatoliki😆😆.Sijawahi kuona Wasabato wanashambulia mafundisho ya madhehebu mengine kwamfano Lutheran,Anglican,Assemblies of God,Moravian wao kila siku ni kuwapinga Wakatoliki tu🤣🤣
Ndio mama wa makanisa yote Mkuu (i.e mama wa makahaba)
 
Back
Top Bottom