Ni kweli Kanisa Katoliki wanatunza akiba ya fedha kutekeleza Sheria ya Jumapili?

Unajibu kwa hisia au maandiko
 
Hivi bifu la SDA na RC lilianzaje? SDA wenye waumini 20m wanawezaje kupambana na RC yenye waumini 1.4b? Dunia ina watu 7b ambao ni 7000m. Ina maana Mungu atachoma viumbe wake 6980m kisa hawaabudi jumamosi kwenye makanisa ya SDA? Kama Mungu atachujua hayo maamuzi ina maana Kiranga atakuwa yuko sahihi.
 
Malaya ndio wanajua mambo mkuu...wanakuchanganyia ladha
 
Kwakuwa umesema uliambiwa na rafiki yako Msabato yatosha kuishia hapo,siongezi neno!!!
 
Sio Kweli!!!
1. Kwa miaka zaidi ya 100 Kanisa Katoliki Afrika na America kusini,India n.k Walikuwa wanategemea misaada toka kwa waamini wa nchi za Ulaya- hii imekuja kubadilika kutokana na Ukatoliki kupunguwa Huko Ulaya na hivyo misaada hiyo aipo tena.Kuna Nchi Makanisa yamegeuzwa Clubs, Makumbusho au majengo kwa kazi zingine.. Vijana wengi Ulaya awana time na Dini.
2. Kanisa Katoliki alina mpango wala alifikirii kutwaa Dola yeyote ile katika Dunia hii na wala aina Nia ya kufuta Usabato,Ulokole au Ukristu wowote ule-Bibilia ya Leo inayotumika na Wakristo wote ikiwemo wakatoliki na Wasabato imetokana Na Wakatoliki.Kanisa Katoliki lina hazina kubwa ya Maandiko na Vitabu zaidi ya milioni moja huko kwenye Hifadhi Vatican-Wasabato na madheebu mengi ya Kikristo yana shambulia sana Kanisa Katoliki- lakini Katoliki alina Muda wa malumbano au kujitangaza kama madheebu mengine. Wasabato wao waendelee tu na Mafundisho yao na wapambane na hali yao.. Picha- vitabu na nyaraka katika maktaba ya Vatican .Vitabu vingine vina zaidi ya miaka 2000
 

Attachments

  • IMG_1647.png
    103.1 KB · Views: 7
  • IMG_1650.png
    101.4 KB · Views: 5
  • IMG_1649.png
    105.5 KB · Views: 5
  • IMG_1648.png
    112.3 KB · Views: 8
  • IMG_1651.png
    88.4 KB · Views: 8
  • IMG_1652.jpeg
    33.9 KB · Views: 4
  • IMG_1653.jpeg
    30.7 KB · Views: 6
Hakuna Mungu.

Hizo zote ni siasa za watu tu wakipigana na hali zao.
 
Huyo muongo. Si lazima tuwe na siku moja special ya kusali. Unaweza kufanya ibadan siku yoyote au kila siku.
Haya mawazo yako ni akili za binadamu sio agizo la Mungu
Mungu amewaagiza waadamu wote waabudu na wapumzike siku ya 7 akaliita sabato
Kati ya amri 10 za Mungu sabato ni amri ya 4 soma kutoka 20
Hivyo hauwezi kwenda mbjnguni bila kuamini sheria 10 za Mungu ikiwemo na Sabato hivyo ni hitaji la agizo la Mungu kila mwanadmu awe pia msabato
 
Sasa mleta mada hayo maongezi yake huyo jamaa, yanakusumbua nini?! 😄
 
Hao wasabato na hao waroma wote wapumbavu tu, kwa dunia hii ya leo yenye uhuru na haki ya kuabudu unachokitaka watamlazimisha nani afuate sheria fulani?

Sio wafuasi wa ukatolic tu hata wasio amini hiyo imani hakuna anayeweza kulazimishwa kuamini jambo analotaka mwengine, bahati mbaya wafia dini ni vilaza hawajiulizi haya mambo, dunia ya leo si ile ya miaka ya mababu walioendeshwa kifala kulazimishwa kuamini jambo fulani, leo hii hata zitumike sheria ngumu binadamu bado hawatozifuata.

Acheni kuamini uzushi, hao wakatolic na hao mnaowapa airtime za kijinga hawana hiyo nguvu ya kuamrisha watu wafanye nini, labda kwa waumini wao.

Hata hiyo sunday's law sijui takataka gani hawajaanza kuifanyia kazi leo wala jana bali muda mrefu wamekuwa wakiitumia lakini mambo yao yalibuma, walishajaribu muda mrefu kutaka kuicontrol dunia kupitia sheria zao za kipuuzi za kidini na kisiasa lkn hakuna lililofanikiwa,

kama kipindi cha ujinga na upumbavu wa miaka ya nyuma walishindwa kuitekeleza hiyo NEW WORLD ORDER basi kwa kizazi hiki cha ustaarabu, haki na uhuru hakuna watakaloliweza, acheni uoga na hayo mafundisho ya wachungaji wenu wanaowatishatisha, dunia haina mwisho, haitoisha leo wala kesho, hata hao mnaowaogopa kuwa wataitawala dunia bado hawajafikia nguvu hizo, ndio kwanza wanazidi kupoteza ushawishi katika jamii, ndiomaana wamebaki kueneza vitisho na propaganda kupitia vilaza wao ambao baadhi ni hao manabii wenu, wachungaji wenu na hata viongozi wakuu kutoka kanisa la sabato wako chini ya hao hao waliotunga hizi dini.
 
Hao Wasabato ndio waliotaka kusafiri kwenda ulaya bila passpport,viza wala tiketi ya ndege.
Akili zao zipo chini ya makalio yao(sorry for this)
 
Walikuwa na radio Marekani inaitwa Family Radio ilikuwa inatangaza kupitia masafa mafupi.
Ukisikiliza hiyo radio unaweza kuuza mali zako maana walikuwa wanakuja na ushahidi wa kuokoteza kwamba mwaka 2009 ni mwisho wa dunia.
Kuna mtangazaji alipostaafu VOA ndio akahamia huko kazi kututisha tu.
 
Huwezi kwenda mbinguni kwa sababu kuu moja: USIPOMKIRI, KUMWAMINI NA KUMPOKEA BWANA YESU KRISTO KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO.

“Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
” Yohana 14:6

Yohana 5
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁶ Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwudhi Yesu, kwa kuwa alitenda hayo siku ya sabato.
¹⁷ Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi.
¹⁸ Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na hayo alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu. Basi Yesu akajibu, akawaambia, Amin, amin, nawaambia,
¹⁹ Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile.
 
Inamaana hiyo biblia hamjasoma maagizo kuhusu Amri za Mungu?
Ziko 10 ambazo ni usiue usizini usiseme uongo kumba siku ya sabato
Neno linasema ukivunja 1 umevunja yote
Yesu alitunza sabato Mungu kwenye uumbaji alifanya sabato kama pumziko.
Sasa maana ya kumwamini yesu ni kukubali ukombozi wake na kuamini ktk tabia yake
Sasa unataka umwaimini Yesu kisha uendelee na dhambi? Nakuambia wadhambi hawaingii Mbinguni ni wadhambi ni waliovunja amri za Mungu maana Mbinguni ibada ni Sabato

Sasa wewe bushana na Amri za Mungu mwisho utakuja kuwa kuni katika moto maana hata usiwe msabato wasabato wapo yaani kanisa la Musa la mitume la Mungu
 
Wasabato adui yao mkubwa sio Shetani bali ni Wakatoliki😆😆.Sijawahi kuona Wasabato wanashambulia mafundisho ya madhehebu mengine kwamfano Lutheran,Anglican,Assemblies of God,Moravian wao kila siku ni kuwapinga Wakatoliki tu🤣🤣
 
Naona umefika mkuu
Kuna watu wanapinga sabato huku
 
Ndio mama wa makanisa yote Mkuu (i.e mama wa makahaba)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…