Ni kweli kipindi cha ujauzito mwanamke akianza kujifunza maarifa mapya na kucheza michezo ya akili, itamuongezea mtoto uwezo kiakili?

Ni kweli kipindi cha ujauzito mwanamke akianza kujifunza maarifa mapya na kucheza michezo ya akili, itamuongezea mtoto uwezo kiakili?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Yaani kama mtoto amezaliwa bila mama kufanya hivyo vitu anakuwa na akili lakini kama mama yake angefanya hivyo wakati wa uja uzito basi uwezo wa mtoto huyo kiakili ungekuwa mara mbili ama mara tatu ya uwezo wake alionao

Ni utamaduni ambao upo huko Israel mwanamke anapokuwa na uja uzito anaanza kujifunza vitu vipya kwenye vitabu na kucheza michezo ya kutumia akili ikiwemo kufanya hesabu mpya zinazohitaji awe mbunifu kupata jibu ama kucheza michezo kama chess, soduku, n.k.

Hapa nazungumzia mtoto aje kuwa anaweza kujifunza haraka, hata darasani, hata akiwa namba za kati ni sawa tu ilimradi anaweza kujifunza hara kuliko yule anaeshika nafasi ya kwanza kila muda anasoma kwasababu uwezo wake wa kujifunza haraka ni mdogo hivyo inabidi atumie muda mwingi sana kurudia rudia.

Kuwa na akili za uvumbuzi na namna ya kukabiliana na matatizo, n.k.
 
Moto anazaliwa akiwa na akili zake,
 
Kama wazazi ni viazi mtoto pia ni kiazi
Na mara nyingi sana wabongo wanakosea kupima uwezo wa akili wa mtu kwa kuhitimisha ni sile akili za darasani tu.

Mtu kuwa na uwezo darasani tena kwa kutumia nguvu kubwa sana ya kurudia rudia kusoma hakuwezi kuthibitisha uwezo wa akili. kwenye sekta hii labda ni wazazi wetu wa zamani walikuwpo wenye akili asilia maana hata waalimu kuingia darasani ni kwa mbinde, kitabu ni kimoja tu cha kujifunzia lakini kwenye mtihani mambo yanatoka mapya, hapo ndipo tulipojua watu wenye akili za darasani, swali ni jipya na hujawai kuliona inabidi utumie akili hapo, sio kurudia kulijibu.
 
Ni kweli mkuu. Kuna machapisho mengi katika majarida yanayoheshimika kuonyesha ukweli wa jambo hilo. Mama na mtoto ni kitu kimoja na cho chote kinachofanyika kwa mama kisaikolojia, kiroho na kimwili kinamwathiri pia mtoto
 
Kuna wale wakiwa na mimba wanatembeza mbususu kama kazi waliyoisomea,tuseme na watoto wakizaliwa wanakuwa vicheche?
 
Nipo nnatafiti mambo ya akili asee.

Ahsante kwa kuniongezea kitu.

Hili nnaona lina ukweli kwa maana ya mazingira mtoto anayokulia huathiri matumizi yake ya akili.

Uthibitisho upo kwa watoto waliokulia tumboni mwa wamama wenye stress kibao mwishoni wana uhatari wa kuwa watu wa stress tu maishani maana hormoni zimewalevya.

Ewe baba, ewe mama mjijali wakati wa ujauzito tengeneza mazingira ya Edeni nyumbani kwako kuwe na hali ya hewa ya furaha kihisia na kimwili. Udadisi ndo akili, masala kulangwa✌
 
Back
Top Bottom