Kwa huu ufisadi unaoendelea kwenye hii awamu yake, mapesa yanayoibwa wizarani, mifumo ya control number kuchepushwa, madili wanayopiga mawaziri kama Bashe huku mama Abdul akipata mgao wake kupitia mwanae, naamini hicho kiasi kinawezekana.
Kuna pesa nyingi sana zinachezewa huko serikalini, zile pikipiki zilizogaiwa kila mkoa, matangazo ya mama anaupiga mwingi kila mkoa, mapesa anayogawa Samia misikitini na makanisani, ni kielelezo kingine cha ufisadi unaoendelea awamu hii.
Hapo bado sijaziweka zile grand corruption [ rushwa kubwa] kama;
• Kuhonga bandari zetu Tanganyika kwa waarabu.
• Kutoa sehemu ya misitu yetu, karibia hekari 8000 kwa waarabu.
• Kutoa sehemu ya bahari yetu (kwa Malaysia kama sijakosea).
• Uwanja wa ndege wa KIA kupewa waarabu wakiendeshe.
Binafsi nitashangaa sana kama Samia atakuwa mgombea Urais kupitia CCM 2025, na kwa namna wakina Bashe, Mwigulu, na Abdul wanavyochota mapesa kwa hasira, ni kama vile wameshajua huyo mama yao hatagombea urais 2025.