Ni kweli kuna watu wanaroga ili mwenye nyumba asahau kumalizia ujenzi au kuhamia kwenye nyumba yake?

Ni kweli kuna watu wanaroga ili mwenye nyumba asahau kumalizia ujenzi au kuhamia kwenye nyumba yake?

Siyo tu hivyo unaweza hata kusahau kama ulianzisha ujenzi na unajenga labda kama mtu akuzindue watu waroga , kwa wale ambao hujenga kimyakimya bila kumshirikisha mtu wa karibu hata wa kukuzindua kama una ujenzi ndo basi tena 😀😀😀
 
Watu wabaya sana🤣😂😂😂
 
Wakuu kwema?

Nimisikia kuhusu hili na maeneo ya Mbezi Beach, Mikocheni na Masaki Masaki huko ni wahanga kweli.

Unajenga nyumba inaweza ikabaki kidogo au ukaimaliza kabisa lakini ukawa una sehemu nyingine ya kuishi, sasa hapo ambapo hujamalizia au ulipomalizia unaweka mtu wa kukulindia au mshkaji anakuomba akae hapo ukimaliza ujenzi au siku ukitaka kujamia atahama.

Lakini kila ikitaka kwenda kumalizia ujenzi unasahau, kila ukitaka ukaangalie nyumba yako unasahau, kumbe umepigwa kirogo usahau nyumba yako watu wajifaidie. Wanakaa hapo hadi wanapata wajukuu.

Bila ya kuwa vizuri kwenye mizimu yenu au ukaenda na mchungaji mkapiga maombi ndio imetoka hiyo, hakuna kuzinduka. Ndio ukute ulikuwa unajenga kisirisiri, ndio inakua imeisha hiyo.

Mzee wa mizimu hii imekaaje Mshana Jr? Ni kweli haya yanafanyika au stori tu za mtaani?

Afrika ni raha sana ndani ya roho. Yaani mwingine anaenda kwa nabii ili aliyemkopesha asahau. Huku wengine wakienda kwa sangoma ili mwenye nyumba asimalizie ujenzi ili waendelee kuishi hapo.
 
Kama kijijini mtu anarogwa anaacha mashamba anakimbilia mjini na harudi kwao mpaka anakufa, watu watashindwa kukutengeneza wewe usahau nyumba yako?
 
Viwanja hii dhana haihusiki? Maana nina maeneo kila nikitaka kwenda naahirisha yaani sijisikii tu kwenda na sina sababu. Mbaya zaidi napita kwenda kwingine mbali zaidi. Na leo nimepita 😇😇
Kama umeweka mtu alinde kiwanja basi mfukuze utashangaa kila wikiendi unaenda...very strange but ni ukweli...kabisa Nina experience zaidi ya moja ya hayo mambo
 
Mkuu nashukulu Kwa Kuni tagg
Nimeona hii mada kupitia wewe wacha nijibu Kwa nijuavyo na niliyo yaona🙏🏽.

Kuna dada mmoja anaishi morogoro alikuja akiwa amepata ajali aligongwa na gari la tanesco kwenye paja na gari ikapita juu ya paja lake ebu jast imagine iyo ajali ilikuaje 🤷🏽‍♂️ SI ya kuondoka mtu eeeh,haya tuendelee hospital alikaa miaka 2 anauguza paja kidonda kinatoa maji tu hakiskii dawa hatimae ma doctor wakamwambia apa sisi tumemaliza Kila kitu lakin Hali Yako Bado haibadiliki ivyo hili tatizo sio letu apa hospital nenda na upande wa pili wa tiba asili,ndo kukutana nae,n kwel Ile ajali ilikua ya mazingara tukapambana nae baada ya miez 4 mbele akapona kabisa kidonda chake na maisha mengine yakaendelea,baada ya miaz 2 mbele yule dada alirud kuja kunipa shukran Kwa kidonda (mguu wake)kupona kabisa.

Ila akanambia nyumbani kwao matombo bwakila juu uko Kwa wenyeji wa uko nadhan mnapafahamu, tuendelee na mada yetu kule ana nyumba yake Kila akijenga inafika adi linta ila inabomoka alafu ni kipindi Cha kiangazi ndo inadondoka anasema imeshaanguka mala 3 nzima,ikanibidi Mimi na yeye nitoke nilipo ad uko matombo kwenye huo mjengo wake ,niliingia mapema tu pale jion ila nikafikia guest mida ya Kaz sa sita usiku nikaenda kupaweka SAWA asubui mi huyoooo nikalud kwenye makazi yangu ya siku zote Kisha nikamwambia nenda kaendelee na ujenzi alifanya ivyo adi Leo anaitwa mama mjengo,ule mjengo haukudondoka tena ila nilimwambia adui Yako anae kufanyia ivi utamjua kwel kwao ukatokea msiba akaenda kufika kule mama yake mkubwa na mjomba wake walipo mwona tu bint kafika msibani waliongea maneno ya shiti sana kwamba yule Binti analinga+kujiskia nk na wakaondoka wakilia kwamba wanaumia na hawakulud tena msibani ad kesho yake watu wanazika wao hawakuonekana😂😂.

Mkasa wa pili.
Kuna police yupo Dodoma Kwa jina namuhifadhi,alinipigia sim kwamba ana kiwanja chake anakiuza pale mbezi malapa mawili ambacho ndo alinzia maisha wakati anapata Kaz alikiuza Kwa mda wa miaka 3 bila kupata mteja watu wanakuja kukiangalia kwenye malipo Waha onekani😂😂,Mimi uyooooo nikafunga safari kwenye bus naingia jijini dare salade nimefika sa 10 jion nikapokelewa na dada yake na uyo afande nikaset mambo yangu Kisha nikamwambia nipeleke site kufika site nikapiga mambo yangu safi,nikalud kupanda bus uyooo kwenye makazi yangu kuendelea na mambo yangu mengine,kile kiwanja alikua mwenyewe anakiuza million 33 lakin hakupata mteja akaja kuuza ad million 12 hakuna mteja,baada ya kufanya Mimi kazi ndani ya wiki alikiuza million 47 badala ya milon 33 😂😂😂 watu wabaya sana,na Alie Fanya Kaz iyo alikua dalali alikifunga Ili kisipate mteja yeye dalali ndo akiuze Kwa bei anayo itaka yeye ambayo afande alikua anaona kama anazulumika mana dalali anapata pakubwa kuliko yeye mwenye Mali,ivyo akagoma🤣🤣🤣.
NB: Sio madalali wote watundu msije kunichukia Bure ndugu zangu😂😂😂.

Ivyo Aya mambo ni yapo na yanawatesa sana watu,watu wanapoteza haki zao sababu ya ujinga wa watu wavivu kutafuta.

Nawakilisha hoja🙏🏽
Mkuu utawapata wengi sana. Jiandae tu kuvuna chenji.
 
Sefania 1:13

Watajenga nyumba lakini hawatakaa ndani yake.

Hii ni LAANA Mungu huruhusu Kwa wote wanaojaribu kufanya mambo bila kumtegemea Mungu, shetani hupata ruhusa kukwamisha hatua za mtu.

(Isaya 65:21)

Watajenga nyumba na kukaa ndani yake,

Hii ni baraka.

Uchawi unafanikiwa tukienda nje ya mapenzi ya Mungu, tukiwa ndani yake, hakuna uchawi juu yetu.

Tujifunze kulipa zaka kuepuka LAANA.
Zaka kivipi mkuu
 
Wakuu kwema?

Nimisikia kuhusu hili na maeneo ya Mbezi Beach, Mikocheni na Masaki Masaki huko ni wahanga kweli.

Unajenga nyumba inaweza ikabaki kidogo au ukaimaliza kabisa lakini ukawa una sehemu nyingine ya kuishi, sasa hapo ambapo hujamalizia au ulipomalizia unaweka mtu wa kukulindia au mshkaji anakuomba akae hapo ukimaliza ujenzi au siku ukitaka kujamia atahama.

Lakini kila ikitaka kwenda kumalizia ujenzi unasahau, kila ukitaka ukaangalie nyumba yako unasahau, kumbe umepigwa kirogo usahau nyumba yako watu wajifaidie. Wanakaa hapo hadi wanapata wajukuu.

Bila ya kuwa vizuri kwenye mizimu yenu au ukaenda na mchungaji mkapiga maombi ndio imetoka hiyo, hakuna kuzinduka. Ndio ukute ulikuwa unajenga kisirisiri, ndio inakua imeisha hiyo.

Mzee wa mizimu hii imekaaje Mshana Jr? Ni kweli haya yanafanyika au stori tu za mtaani?
Hyo kitu ipo sana
  1. Kuna wapangaji
  2. Walinzi wa nyumba
 
Kama umeweka mtu alinde kiwanja basi mfukuze utashangaa kila wikiendi unaenda...very strange but ni ukweli...kabisa Nina experience zaidi ya moja ya hayo mambo
Naahidi weekend ijayo naanza kutembelea. Hii si kawaida yangu.
 
Zaka kivipi mkuu
Zaka ni malipo ya 10% Kutoka kwenye Pato alilokupa Mungu.

Sasa ukijenga nyumba bila kulipa zaka, u atafuta matatizo maana wapagani au washirikina hawajengi bila Kutoa sadaka Kwa miungu Yao, iweje mwana wa Mungu ujenge KICHWA KICHWA Kwa kukurupuka?
 
Back
Top Bottom