Wenaya
Member
- Feb 28, 2015
- 14
- 9
Kwanza ishu ya Fiesta iko wazi sasa hivi Diamond ni Balozi wa Vodacom na Tamasha la Fiesta kwa Mwaka 2016 lilikuwa liko chini ya udhamini wa Tigo Tanzania kwa hiyo ilikuwa ni ngumu kwa Diamond kuperform kwenye Jukwaa la Fiesta kwa hiyo yeye kuwa Nigeria ni kwa ajili ya kukamilisha ratiba zake za Show maana list ya show atakazozifanya kwa mwaka huu ziko wazi kwa hiyo hata ile show aliyofanya nje ya Nchi wakati Fiesta inaendelea ilikuwa kwenye Ratiba.Je hilo swala ni la kweli kuwa diamond ameanza kuonyesha dalili za kumuogopa alikiba coz ukiangalia hata kwenye tamasha la fiesta alikimbili Nigeria pia kwenye tuzo za eatvaward kama kakimbia ivi coz nomination zimetajwa lkn cjaona jina lake ndo maana najiuliza je ameanza kuwa muoga anapoona dalili za king kuwepo????????
Mapovu yanaruhusiwa
Pili: Kuhusu tuzo za MTV EMA.
Nikurudishe nyuma kidogo Mwaka juzi Sauti Sol kutoka Kenya walichukua Tuzo hiyo ya Kundi Bora, Mwaka Jana Diamond akachukua Tuzo mbili za MTV EMA kama Best African Act na Worldwide ile ambayo ilijumuisha na India. Mwaka huu wa 2016 kwa Mujibu wa Diamond mwenyewe kupitia Kipindi cha The Playlist cha Times Fm kilichoko chini ya Ommary Tambwe Diamond alitoa sababu hii. Nanukuu " Mwaka huu Mimi sijawa nominated lakini Ally kawa Nominated hivyo watu tumpigie kura na tuzo ije kwetu na sababu ya Mimi kutokuwa nominated hawa MTV hawawezi kumuweka mtu ambae alichukua tuzo last time eti awanie wanakuwa na mashaka kuwa anaweza kuchukua tena so ikawa kama kuna upendeleo fulani.
Mwisho Diamond hamuogopi Alikiba wala Ally hamuogopi Diamond ila ushindani uliopo ni wa muziki kama Kazi ila katika Maisha ya kawaida wako kawaida ila kila mtu ana ratiba zake kwa hiyo ndio maana hata kugongana kwenye ratiba ni ngumu. So mwisho wa siku tuwapende wasanii wetu na kuthamini kila kitu wanachokifanya maana kwa muziki wa Tanzania Alikiba na Diamond kwa sasa hivi wametutangaza sana.
One love. Tanzania Moja. Afrika Moja.