Kupitia mitandao ya kijamii, hususan Facebook, kumekuwepo na ukurasa uliochapisha video inayowahamasisha wanaume kutofanya mazoezi, ikidai kuwa kufanya mazoezi husababisha watu kutokuwa na afya njema. Katika video hiyo, mhusika anarejelea zamani akisema kuwa watu wa kale hawakufanya mazoezi, na anawashauri wanaume waache kufanya mazoezi kwa madai kwamba wanaweza kuugua maumivu ya mgongo.
Je ni upi uhalisia chapisho hilo.
Je ni upi uhalisia chapisho hilo.
- Tunachokijua
- Kumekuwa na kipande cha video kinachomuonesha mtu anayeelezea kuwa mazoezi si mazuri kwa wanaume na hivyo ni vyema wanaume kuacha kufanya mazoezi.
Uhalisia wa madai hayo ni upi?
JamiiCheck imefuatilia na kubaini kuwa madai hayo ya kuwakataza wanaume kutokufanya mazoezi si sahihi.
Shirika la Afya duniani (WHO) linabainisha kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kufanya mazoezi kwa watoto, vijana, watu wazima, wazee, wajawazito, waliojifungua na wagonjwa wa magonjwa ya kuambukiza.
Tovuti ya Havard Health Publishing inaeleza kuwa ni muhimu kufanya mazoezi kila siku kama unaweza. Mazoezi kwa muda mfupi yanaweza kusaidia kudhibiti hamu ya kula, kuboresha hisia (Mood), na kuimarisha usingizi.
Mazoezi ya muda mrefu yanaweza kusaidia kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo, kiharusi, kisukari, shida ya akili (dementia), msongo wa mawazo (depression), na aina nyingi za saratani.