Ni kweli kuwa watu wote walioko kwenye ndoa au waliooana wanapendana?

Hahahaha! dada yangu bana...... Ulimpa nini huyu mtu mpaka akakuganda hivyo. Si lazima usemee hapa, twende kwenye PM.

mtu anapopoteza kitu ndio anapoona umuhimu wake, sasa huyu ikawa too late lakini akawa kama anataka kujitoa ufahamu vile.
 
nyamayao pole lakini hongera at the same time..........huh mwenzetu ushawahi kuwa na stalker wako binafsi! wenzio wanaitafuta bahati kama hiyo! lol

ndugu yangu ndoa sio nyepesi kihivyo, kila mtu anakutana na msalaba wake...................kama alivyosema dark city tuzidishe kuomba tu kwa mungu atuepushie vitu vyengine, yaliyopita hayana umuhimu sana katika ndoa, kuelekea mbele ndio kasheshe

sasa ni vijimambo kama hivyo nakuambia wewe umeviepuka, imagine hapo mr alinibadilikia ki namna gani, yaani ilikuwa kazi kweli kurudisha hali kama zamani, ilikuwa ishu haswa, na mbaya zaidi wivu umemtawala bac akical kidogo umechelewa kupokea na mpo labda job au mpo sehemu tofauti ni unaanza kuambia oohh ahhh mnarudi nyuma badala ya kwenda mbele...khaa....nakupongeza sana Gaijin.
 
Kama kwenye ndoa kuna Pendo na Penzi la kweli, kasheshe litatokea wapi? Talking to experience, mimi na ndugu zangu wanajua kuwa baba na mama yangu ni wapenzi wa kweli (mpaka nawaonea wivu). Sijawahi kushuhudia wakikosana, kugombana au kutukanana hadharani. Mama anamheshimu sana baba na baba anampenda upeo mama. Ndoa yao sasa inagonga miaka 40 sasa. Au labda mniambie kama bado kuna nafasi ya ndoa hii kupata kasheshe huko mbele ya safari. Mimi naamini ndoa iliyozaliwa kwa watu kupendana, haitaleta kasheshe sasa na hata baadaye.

Mi ya kwangu sasa inatafuta miaka kumi. Inawezekana ikawa bado ni changa kiasi kuwa itaweza kuzua kasheshe hapo baadaye? Siamini, naomba Mungu aepushie mbali hata hivyo.......
 
mtu anapopoteza kitu ndio anapoona umuhimu wake, sasa huyu ikawa too late lakini akawa kama anataka kujitoa ufahamu vile.
Ila na wewe sometimes huwa unakumbukia mambo flani... sema tu ukweli
 
Kumbe ina faida nyingi hivyo! itabidi sasa tuanze kupiga kampeni wasichana wasubiri mpaka ndoa ndio wafanye tendo.................unaonaje?
 
:mmph:
sasa ni vijimambo kama hivyo nakuambia wewe umeviepuka, imagine hapo mr alinibadilikia ki namna gani, yaani ilikuwa kazi kweli kurudisha hali kama zamani, ilikuwa ishu haswa, na mbaya zaidi wivu umemtawala bac akical kidogo umechelewa kupokea na mpo labda job au mpo sehemu tofauti ni unaanza kuambia oohh ahhh mnarudi nyuma badala ya kwenda mbele...khaa....nakupongeza sana Gaijin.

hapa nyamayao umegonga Ikulu ..sijui huwa wakoje wanadhani mtu umekuwa customer care
 
Mkuu Mbu binadamu tunapokuwa kwenye mapenzi mara nyingi huwa ni raha tupu. Binadamu tunazijua kasoro zretu ambazo wapenzi wanaweza kuzikubali na nyingine ambazo hawatakuwa tayari kuzikubali hivyo kipindi hicho cha mapenzi moto moto ni nadra sana kuzijua kasoro za umpendaye. Sasa unapoamua kuolewa naye au kumuoa basi ndiyo sasa anaanza kuonyesha makucha yake na kama nilivyosema kuna kasoro nyingine zinavumilika kabisa maana hakuna binadamu ambaye yuko perfect. Kwangu binafsi sipendi uongo, uchafu, wizi, uhuni, ulevi, dharau, kutokubali makosa na kusema samahani , kutojua kupika, uvivu wa kupita kiasi. Hizi kwa kweli si rahisi kuvumilika kabisa ukiuingia mkenge kama huu ni bora kujinasua haraka sana kabla ya kukumbana na matatizo utakayoyajutia kwa miaka mingi baadaye.

Babu kwa kweli nimegundua wewe ni perfectionist, kumpata mtu wa namna yako inahitaji muujiza wa Mungu. Mimi nakataa katu huwezi kkuwa na mwanamke atakayekosa kasoro hata moja ya hizo ulizozitaja. Hakuna na hakuna. Na kwangu mimi kufanya kosa ni ubinadamu, na kusamehe ni uungu. mungu alianzisha hii taasisi ya ndoa ili watu wajifunze unyenyekevu na kusameheana, na kuchukuliana mizigo. Hakuna mtu mkamilifu, wale wanaodhani kuwa watapata mke asye na udhaifu ndio wale wanaokaa muda mrefu bila kuoa.
 
Kumbe ina faida nyingi hivyo! itabidi sasa tuanze kupiga kampeni wasichana wasubiri mpaka ndoa ndio wafanye tendo.................unaonaje?

ndio mpaka wawe nazo bac, mana nao wana haraka ya kuzitoa kweli kwa ahadi za kununuliwa cmu.
 
:mmph:

hapa nyamayao umegonga Ikulu ..sijui huwa wakoje wanadhani mtu umekuwa customer care

haa kwa wakati huo mgumu kwangu nilijirekebisha, yaani hata nikiwa jikoni nitaiweka kwenye eproni ili imradi kunusuru matatizo/maneno...lol
 
chrispin mpaka sasa nna miaka miwili ya ndoa sijakutana na kasheshe lakini hivyo ndio tunavyoambiwa kuwa makasheshe kwenye ndoa yapo.

mfano umesikia kuwa mume ametoka na bar maid ..............lol (kakosea tu lakini kusamehe kwa siku moja ni ngumu)

au mwanamme ameanza tabia ya kukaa saana nje na wewe huipendi..................ukimkosoa anakasirika.

au mwanamke kaanza kushiriki marafiki sana....................wewe hupendi lakini ukimwambia hakuelewi.

vipo vitu vinatokea vya kukera japo kwa hao wazee wetu walioishi miaka 40 pamoja, lakini vilitokea zamani na wameshavisahau ndio maana hatuvijui, au walijitahidi kumaliza mambo yao ndani mwao tu. Ndoa zilizo smooth bila ya kukwaruzana ni chache mno kama zipo.
 
Ila na wewe sometimes huwa unakumbukia mambo flani... sema tu ukweli

kweli cmkumbuki kabisa, mana aliniacha na maumivu bado anataka kunuharibia mambo yangu, kwanza najutaga sana cku nilipokutana nae.
 
mie niliulizwaga mwanzoni kabisa..bfnd/galfrnd, lakini nilipokuwa ndani sasa, yule mwanaume alieniacha(mana niliachwa) ikatokea tupo mji mmoja kwenye kutafuta maisha, akaanza usumbufu wa hapa na pale, mpaka mr akahic kitu fulani hivi, nikasema ngoja nijitoe kimasomaso kumwelezea kwamba mhucka alikuwa ni huyu na sasa anaanza kusumbua fulani hivi(lilikuwa kosa kubwa kusema) nilikuwa siendi mahali bila mr/mtu wa ziada, nilikuwa cna uhuru/amani kabisa, mpaka ikatokea cku moja ishu imeniletea kasheshe, mana alieniacha alikuwa anacctiza mie nilikuwa chaguo lake sema shetani alimpitia so kwa gharama yoyote ananirudisha kwenye himaya yake, sasa hapo ilikuwa nikitoka ofcn huyu hapa, cku moja natokea supermarket mie cjui kama mtu ananiwinda mara huyu hapa kaanza kunivuta akitaka apate hata dk chache tuongee kdgo, mr yupo parking anaona kila kitu...nickuelezee kilichotokeaa, ctaki kukumbuka kabisa.

Pole sana dada. Ila kama umeshashinda huo mtihani ujue mambo mswano. Kanyaga moto twende. Huyo ex BF alitaka kukuharibia tu. Hongera sana na udumu kwenye ndoa yako hadi Mungu aamue!

Lunch njema.
 
chrispin mpaka sasa nna miaka miwili ya ndoa sijakutana na kasheshe lakini hivyo ndio tunavyoambiwa kuwa makasheshe kwenye ndoa yapo.

mfano umesikia kuwa mume ametoka na bar maid ..............lol (kakosea tu lakini kusamehe kwa siku moja ni ngumu)

au mwanamme ameanza tabia ya kukaa saana nje na wewe huipendi..................ukimkosoa anakasirika.

au mwanamke kaanza kushiriki marafiki sana....................wewe hupendi lakini ukimwambia hakuelewi.

vipo vitu vinatokea vya kukera japo kwa hao wazee wetu walioishi miaka 40 pamoja, lakini vilitokea zamani na wameshavisahau ndio maana hatuvijui, au walijitahidi kumaliza mambo yao ndani mwao tu. Ndoa zilizo smooth bila ya kukwaruzana ni chache mno kama zipo.

piga sala sana kuepusha hilo, lilinikuta hilo mie, haaa jamani mwanamke kweli kazi anayo.
 
chrispin mpaka sasa nna miaka miwili ya ndoa sijakutana na kasheshe lakini hivyo ndio tunavyoambiwa kuwa makasheshe kwenye ndoa yapo.

mfano umesikia kuwa mume ametoka na bar maid ..............lol (kakosea tu lakini kusamehe kwa siku moja ni ngumu)

au mwanamme ameanza tabia ya kukaa saana nje na wewe huipendi..................ukimkosoa anakasirika.

au mwanamke kaanza kushiriki marafiki sana....................wewe hupendi lakini ukimwambia hakuelewi.

vipo vitu vinatokea vya kukera japo kwa hao wazee wetu walioishi miaka 40 pamoja, lakini vilitokea zamani na wameshavisahau ndio maana hatuvijui, au walijitahidi kumaliza mambo yao ndani mwao tu. Ndoa zilizo smooth bila ya kukwaruzana ni chache mno kama zipo.
Gaijin Darling,

Kama kweli unampenda utamlinda.............. UPENDO HUVUMILIA YOTE!!!!
 
Nyamayao .............nakupa hongera kwa kutumia nguvu na jitihada ya kulinda ndoa yako. manake naona mambo yalikuandama.

inafaa uandike kitabu...................unaweza kuokoa ndoa za wengine
 
haya maneno yako yana ukweli . Muhimu kuvumilia ili kulinda pendo lenu.

mtu asiingie kwenye ndoa akafikiri itakuwa nyepesi mwanzo mwisho, ajue kama Pendo linaweza kuhimili chochote
 
Mwenye masikio na ASIKIE,kwa wote ambao ni ma-bachelors na ma-spinsters wote,msijesema badae kuwa mlisahau HAYA yote yanaelezwa hapa.
 
Nyamayao .............nakupa hongera kwa kutumia nguvu na jitihada ya kulinda ndoa yako. manake naona mambo yalikuandama.

inafaa uandike kitabu...................unaweza kuokoa ndoa za wengine

unajua niliolewa mdogo kwa kweli, na nilikuwa cna akili ya ziada ya kujua ndoa haswaa, nimeng'ang'ania nampenda kijana! nimeingia nikaanza na kashikashi za kifamilia(mara wifi, mara mama mkwe)...nilikomalia hapo, nilipambana/nitaendelea kupambana, cpo tayari kumpoteza kwa sababu zisizo na kichwa wala miguu.....sasa hivi nimepumua sana baada ya kumaliza hizo ghasia haaa!
 
Back
Top Bottom